Luhaga Mpina ataka Katiba mpya inayolinda Rasilimali za Nchi

Wakati wa Mabadiliko ukifika hakuna wa kuyazuia.

Tundu Lissu aliposema Umuhimu wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi vilaza wa CCM walianza kumjibu kwa kukurupuka bila kujua kumbe hata huko CCM wenye akili timamu wanasema Katiba Mpya ni sasa.

Asante sana Luhaga Mpina. Ni vizuri wana CCM wengi wanaoangalia maslahi mapana ya nchi na sio ya chama na mtu mmoja mmoja kuzidi kujitokeza na kudai Katiba Mpya sasa.

Asante Tundu Lissu. Nyoka wameanza kutoka pangoni.

Hapa tu retreat ya Chadema haijafanyika, ikifanyia sipati picha inzi wa kijani watakuwa kwenye hali gani?

#NoReformNoElection
 
Msimamo wa mpina tangu zamani unajulikana.
 
HUYU MPINA NDO YULE MZEE AMBAE HAKUSIMAMA KUSHANGILIA ULE USHUZI WA VITANO TENA AU MWINGINE??
 
Kama CCM wangekuwa wanajali maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla, hayo uliyoyaandika wangeyazingatia.

Tatizo la msingi ni kuwa CCM sio chama cha siasa tena, ni genge la wanyang'anyi wanaotumia siasa kushibisha matumbo yao na ya familia zao.

Chukua Chako Mapema (CCM).
 
Lumumba ipi hiyo?!!
Mh.Luhaga Mpina si msemaji wa CCM wala wanalumumba....

Watanzania walio wengi hawaihitaji katiba mpya....wanaohitaji ni wanasiasa wachache akina Lissu.....

Katiba si mali ya wanasiasa peke yake.....

#Nchi Kwanza!
#Katiba iliyopo ni bora !!
 
Katiba ni takwa la msingi, tunaitaka sasa
 
Mbona Mpina tangu muda tu anajulikana msimamo wake kabla hata ya Lisu kuwa mwenyekiti
 
Sasa ccm Katiba yao wanaipuuza itakuwa Katiba ya nchi?
Mwenyekiti wenu bi kiboko alishasemaga katiba ni kitabu tu hakina maana yoyote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…