Luhaga Mpina: Deni la Serikali lapaa kutoka Trillion 62.4 mwaka 2021, Hadi kufikia Trillion 96.9 mwaka 2024 !!

Luhaga Mpina: Deni la Serikali lapaa kutoka Trillion 62.4 mwaka 2021, Hadi kufikia Trillion 96.9 mwaka 2024 !!

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Sawa na Ongezeko la Trillion 32.4 .

"katika mwaka 2020/2021 mashauri ya malimbikizo ya kodi za makinikia yaliamuliwa katika mahakama za rufani za kodi yenye thamani ya shilingi Trilioni 5.595 na mahakama kuagiza kufanyika mazungumzo kati ya Serikali na walipa kodi ambayo ni North Mara gold mine, Pagea minerals limited, Buryanghuru gold mine, Abg exploration na kuweka utaratibu wa namna ya kulipa"

"Pia kiasi cha shilingi Trilioni 343.5 iliondolewa katika mahakama ya rufani na kurudiwa kusikiliza na TRA.Mwaka 2021 serikali ilieleza kuwa madai hayo yalifutwa kutokana na makubaliano yaliyofanyika baina ya serikali na makampuni ya madini. Hii ni kinyume cha sheria kwakuwa Waziri wa Fedha na TRA hawana mamlaka kisheria kufuta madeni ya nchi bila ridhaa ya bunge."

"Nashauri Tume ya Rais ya ya maboresho ya kodi kushinikiza madai ya malimbikizo ya kodi kwa makampuni ya madini makinikia na hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa."


View: https://www.youtube.com/live/rwIdf9x54HE?si=7DqEJdRObXwam_J4



View: https://www.youtube.com/live/N7-htfoVO6I?si=cKQ2XwIHyQWwd-Mr
 
1738168233681.png
 
Mgombea uRais kupitia Chadema 🐼😂
Kosa la Mpina ni lipi hapo mkuu?

Miaka 4 unakopa Trilioni 33plus.

Akipewa mingine 5, deni litakua Trilioni 150.

Kizazi kijacho kitatushangaa sana tuliongozwaje na watu wa namna hii?

Mikopo inaenda kwenye pikipiki nchi nzima, samia legal aid(unajiuliza rais tena unatoa msaada wa kisheria, si ubadili sheria ama uboreshe sheria tu?)

Hiyo mikopo ndio inaenda kwenye mara samia scholarship, sasa bodi ya mikopo ipo ya nini? Inaenda kugharamia mamilioni wanayopewa kina Mwamposa(mwamposa alipaswa kua jela mwaka 2020 aliua watu Moshi na bado yuko uraiani)

Serikali haitaki kusimamia ukusanyaji kodi, inaona ikope kuliko kuhimiza kulipa kodi.

Unajiuliza miaka 5 ya Samia hakuna ufisadi mkubwa mkubwa Tanzania, watanzania wote wameokoka, mbona hakuna fisadi hata mmoja alieshitakiwa ama mafisadi wote waliokoka kipindi hiki cha Samia?

Hii nchi chini ya vegetables haiwezi kwenda mahala popote.
 
Back
Top Bottom