Luhaga Mpina kudaiwa kudhulumu ardhi ya Kijiji ekari 1000 Morogoro, Wizara ya Ardhi iingilie kati

Ndio maana huwa nasema ndani ya Ccm hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole.
Wote ni wachafu.
 
MNAPOMWANDAMA mh.MPINA msimsahau na MAKONDA Viwanja vya Wahindi vya Alivyojimilikisha
 
Hii ni sheria, Serikali ya Kijiji haiwezi kugawa ardhi yenye ukubwa wa ekari zaidi ya 50! Wizara ya ardhi, Mpina anasema kapewa ekari 1000 na Kijiji, japo Kijiji wanakataa kumpa ardhi ya ukubwa huo!

Sheria zisimamiwe, huyu amevunja sheria, anyanganywe hiyo ardhi iliyozidi ekari 50, arejeshe ekari 950!

Wizara ya ardhi iingilie kati kuokoa ardhi ya Kijiji!
 
Subiri aje awalipue bungeni
 
Aoneshe muhtasari wa kikao na majina ya wajumbe waliopitisha huo umiliki
 
Leta hiyo Sheria hapa tuisome wote.
 
Huyu atajua hajui tu. Wanakijiji juzi wamekaa kikao na kutoa maazimio maalum kumuomba Rais awarudishie ardhi yao.
 
Duh...!. Sasa ndio mnaanza kufurumua ya Mpina kwasababu tuu amemsema JM?. Siku zote mlikuwa wapi?!.
P
 
Tulisha jua kwamba sasa mpina anaanza kutafutwa na chawa wa watu fulani
 
Tulisha jua kwamba sasa mpina anaanza kutafutwa na chawa wa watu fulani
Anatafutwa kwa lipi sasa? Kama amepora ardhi na mashamba ya wananchi, aachwe! Kwa sababu anabwatukia watu Bungeni?

Mwache ajitetee mwenyewe. Na kama ni kweli anaimiliki hilo eneo kihalali, ajitokeze hadharani na vielelezo.
 
Hilo eneo kaanza kulimili mara tu baada ya kusema madhaifu ya wizara ya makamba ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…