Luhaga Mpina: Mfumuko wa bei umetengenezwa. Ataka uchunguzi kilichojificha Symbion na mikataba mibovu ikafutwe bungeni

Luhaga Mpina: Mfumuko wa bei umetengenezwa. Ataka uchunguzi kilichojificha Symbion na mikataba mibovu ikafutwe bungeni

Jamaa namuelewa ana pointi nyingi za msingi sana, ameamua kuweka maslahi ya taifa mbele hata kama yatagharimu ubunge wake mbele ya safari, huyu kwangu ndie mzalendo.

Watakaompinga nawashauri wampinge kwa kujibu hoja zake, sio zile kelele za wakati wake alifanya nini, kuendelea kujidumaza kwa majibu mepesi kama hayo ni kuliangamiza hili taifa.
You don't know him. Hizo ni hasira za kukosa Uwaziri. Tena ashukuru Mungu yuko huko mjengoni sababu alikosa ubunge 2020. Ule uchafuzi ndiyo umemuweka hapo. Hata Mwendazake alitamka hadharani hicho kitu. La mwisho kabisa ana bifu na February Marope tangu wapo Mazingira.
 
Asante wewe umeongea ukweli, ifike mahala, sio kila mwana CCM anayetofautiana na mamlaka akaitwa sukuma gang, sababu hii inawapa nguvu sana wapigaji na wale wote wenye nia mbaya na hii nchi.
Kwa taarifa yako Mpina ni Sukuma Gang hasa na hampendi SSH. Mbaya zaidi alivyokosa Uwaziri kipindi cha Mwendazake na SSH kumteua February ndiyo chuki hasa ilipoanza.
 
Na huko Kenya, France, Marekani, UK n.k ambako kunaripotiwa mfumuko wa bei mkubwa kuwahi kushuhudiwa toka 2008, pia huo mfumuko umetengenezwa?

Vipi kuhusu wananchi Ulaya kutoruhusiwa kununua mafuta ya kula zaidi ya chupa moja nako kumetengenezwa na January Makamba na washirika wake?

Huyu mpuuzi Mpina si ndio inasemekana aliharibu maisha ya wavuvi wengi na kujimilikisha ekari nyingi kinyume na sheria hapo Morogoro? Huu uchungu na wananchi ameutoa wapi ghafla bin vuu?

Asifikiri anaweza kugombanisha wananchi na serikali halafu arukie kwenye hicho chama chao cha Umoja Party!

Huyu mjinga better he is reminded waliopo madarakani saivi wamekulia kwenye corridors of power. Wanajua mchezo wake wa mbuni kuficha kichwa chini huku kiwiliwili kikiwa nje!

View attachment 2217827
Mjinga sana huyo. Atawa-fool wasiomfahamu pimbi yule
 
Akichangia hotuba ya waziri wa viwanda na biashara, mbunge Kisesa, Luhaga Mpina ameongelea mambo mbalimbali ikiwemo uhusiano kati ya sekta binafsi na umma, mikataba mibovu ukiwemo wa Tanesco na Symbion, bilioni 70 za mkataba wa maendeleo ya tehama Tanesco na Mahindra ya India, mkataba mpya unaokuja TPA, bei ya mafuta nchini na mfumuko wa bei.

=======

Luhaga Mpina: Suala la uwekezaji wa Serikali na sekta binafsi linahitaji kuangaliwa kwa makini sana, mikataba mingi tuliyoingia inanyonya mapato ya nchi, uchumi wa nchi, inahamisha rasilimali, inapora ajira za watanzania.

Sasa hivi TPA nae ameanza kutafuta mbia, mikataba ya namna hii lakini ipo mikataba inayotusumbua mpaka sasahivi ya TRA na sicpa. Ipo mikataba tumeingia majuzi ya India Mahindra na Tanesco zaidi ya bilioni 70 kwaajili ya kuendeleza mifumo ya Tehama wakati wataalamu wa tehama tunao hapa wa kila aina wanaoweza kudevelop mifumo ya Tehama. Vijana wetu wamedevelop mifumo kama GPG, POS na hata Maxmalipo, leo unaenda kutafuta mfumo India kwaajili ya kufanya nini?

Sasa hivi naskia symbion wanapigiwa chapuo tuilipe bilioni 356 lakini inapigiwa hili chapuo wakati huohuo hatuambiwi alieingia mkataba huo na kutusababisha tuwe na mkataba ambao hatuwezi ku-exit hata kama mkataba unatuingizia hasara, amechukuliwa hatua gani?

Wabunge tukataeni mikataba ya namna hii lakini tukataeni hata kulipa hizi fedha, uchunguzi ufanyike kilichojificha nyuma ya Symbion.

Mikataba yote ambayo tunaitambulisha kama mikataba mibovu iitishwe hapa bungeni tuweze kuifuta.

Mwisho Luhaga Mpina ameongelea mfumuko wa bei nchini na kusema pamoja na Covid na vita lakini mfumuko umechangiwa na kukosekana uadilifu na usimamizi makini.

Mpina amesema upangaji holela wa bei kinachoshangaza kwanini wahusika hawajachukuliwa hatua. Amedai waziri anawajua waagizaji wa mafuta nje ya nchi, ngano na anawajua wazalishaji wa ndani ya nchi.

View attachment 2217807
Huyu poyoyo aniponda India kwenye IT?

Haelewi kuwa kampuni zote kubwa duniani za IT zinawatumia wataalaam wa kutokea aindia, na nyingi zaidi zina "outsource" kutoka India.

Hivi mbunge kama huyu anapataje ubunge?


Dunia nzima mfumuko wa bei iliutengeza Tanzania? hovyo kweli huyu jamaa.
 
Nimemsikiliza mbunge Mpina asubuhi hii Bungeni.

Amenifurahisha binafsi sana kwa kutaja dalili za nia mbaya ya Serikali ya Samia kutoka kusimamia uadilifu na kukuza ufisadi.

Kwa mfano ni dalili za kuipigia chapuo kampuni ya Symbion kutoka Marekani kulipwa mabilion eti fidia wakati mkataba ulisimamishwa na walikaa kimya bila shaka kwa kukubaliana na hoja za kuvunjiwa mkataba.

Kuwalipa Symbion kwanza itakuwa kufungua pandora box kwa mikataba ya kifisadi iliyovunjwa kuanza kuidai nchi kama ile iptl kampuni ya iliyochezesha rumba nchi muda mrefu hadi Hayati Magufuli alipoingia madarakani au ile kampuni ya Richmond iliyosumbua hadi ikafikia kujiuzulu Waziri Mkuu.

Lingine ni hili la TANESCO kuingia mkataba na kampuni ya wahindi eti wao kuweka mfumo wa computer kusimamia management.

Tangu January Makamba aingie uwaziri kila mzalendo muamini wa falsafa ya kijamaa hajafurahia. Ila sio hilo ila ni mashaka na uadilifu wake au mtazamo wake.

Nchini kuna ujuzi mkubwa wa kuunda mifumo ya computer sasa kukimbimia wahindi bila shaka ni maslahi ya kifisadi tu.

Kwanza hasara ya kutumia mfumo wa wahindi ni kutoa fursa kwa wahindi kutuhujumu mipango yetu ili tuendelee kuwa tegemezi.
Huyo hana lolote ni sukuma gang tu.
 
Nasisitiza ni wanafiki tu hao .Huyu kuna kitu anakitafuta, akipata atakaa kimya kama wenzake.
Afu bado tu kuna punguwani wanaamini kwa akili hizi ipo siku Chadema wataongoza nchi hii [emoji848][emoji19]

Hata kipofu anaelewa kabisa kuwa ninyi ni mawakala tu wa serikali husika mnaopigania matumbo yenu basi [emoji28]

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
We muulize swali dogo tu uone kama atakujibu yeye mbona mpaka Leo anawasikiliza viongozi wa chadema wakati viongozi wake waliwahi kusema Lowassa ni fisadi na ushahidi wanao lakini hao hao wakampa ugombea wa Uraisi Lowassa na wakasema ni msafi Huu nao tuna uwitaje

Yeye mwenyewe ni fisi tena lafi sana!
Kumzidi JPM? Acha maskhara bwana
 
Back
Top Bottom