Pre GE2025 Luhaga Mpina: Nchi sita za Afrika zilizopindua Serikali zao zilikuwa sahihi

Pre GE2025 Luhaga Mpina: Nchi sita za Afrika zilizopindua Serikali zao zilikuwa sahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanaodai Katiba Mpya ndio hao hao wanatumia Rushwa na ngumu kuchaguana ,mpaka hapo hao wanataka madaraka ya Umma Kwa malengo binafsi.

Mwisho Katiba Mpya haijawahi leta ugali walakutatua shida za watu ila ni njia ya Wanasiasa walioko Nje ya serikali kuingia humo wapate ulaji
Kazi ya Katiba ya nchi siyo kuleta chakula mezani pa mtu yoyote yule. Watu wenye mawazo kama haya ni wale Watu ambao wana akili kiduchu, akili ndogo, wenye akili fupi au akili-mbilikimo.
Je, nchi gani hasa hapa duniani ambayo ina Katiba yenye kuleta chakula mezani kwa Wananchi wake?
 
Hapo kwenye wizi wa kura Tanzania itahusika soon kama CCM wasipoacha uharamia wao kwenye sanduku la kura.
Na siku zote nimesema kuwa kama nchi hii itakujaingia kwenye machafuko na umwagaji damu basi chanzo ni CCM kwa kupindua maoni na matakwa ya wananchi kupitia sanduku la kura kwa tabia yao iliyokubuhu ya wizi wa kura.
 
Kazi ya Katiba ya nchi siyo kuleta chakula mezani pa mtu yoyote yule. Watu wenye mawazo kama haya ni wale Watu ambao wana akili kiduchu, akili ndogo, wenye akili fupi au akili-mbilikimo.
Je, nchi gani hasa hapa duniani ambayo ina Katiba yenye kuleta chakula mezani kwa Wananchi wake?
Sasa hiyo Katiba yenu itatusaidia nini?
 
Salaam, Shalom!!

Akiongea kupitia press aliyoitisha nje ya Bunge amedai kuwa UMOJA wa Afrika haupasi kuzisimamisha uanachama Nchi SITA zilizopindua Serikali zao Kwa sababu Watawala waliopinduliwa hawakujali sauti na matakwa ya wananchi.

Amedai kuwa RUSHWA ikitamalaki, ukiukwaji wa HAKI za binadamu ukiota mizizi, Wizi wa kura ukitamalaki, wizi wa Raslimali za umma ukitamalaki, dhuluma ikizidi katika JAMII, hakuna njia ingine wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kupindua Serikali zao Kwa njia mbalimbali.

Ndugu Mpina ameitaka Serikali ya Rais Samia Kutoa tamko kushauri Nchi hizo zisizuiliwe uanachama katika ushirika wa AU.

Chanzo: Uhondo Tv.

Mungu ambariki ndugu Mpina,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

HAKI ikatawale katika Taifa. Amen

Karibuni 🙏
Ninaungo mikono hoja.
 
Waliopindua mbona wanaendelea kufanya hayo hayo anayoyasema Mpina?

Utawala upi wa Kijeshi ambao jmewaletea Neema Wananchi? Na mbaya zaidi wanajeshi huwezi walalamikia kwamba umekosa Haki unapigwa tuu.

So hakuna uhalali wa kupindua Wala haijawahi kuwa na faidia popote zaidi ya kuongeza umaskini Kwa watu
Gadaffi alivyopindua serikali, watu wake waliishi vema
 
kwa maoni na mtazamo wake, ni haki na uhuru wake kuona mapinduzi yale kama alivyosema kwenye maoni yake,

lakini hayawezi kiathiri wala kudhoofisha kwa namna yoyote ile msimamao wa Tanzania, sambamba na msimamo wa umoja wa Africa...

taasisi hiyo kubwa barani Africa, inaendeshwa kwa kanuni, taratibu na sheria za kimataifa walizo kubaliana kiziheshimu na kuzifuata collectively wanachama wote....

hata hivyo,
nchi hizo haziwezi kufungiwa nje ya umaja huo daima. Yapo mazungumzo yanaendelea hivi sasa miongoni mwao, hatimae kurejea kwenye utawala wa kiraia. Matumani ni makubwa nchi hizo kurejeshewa uanachana wao wa AU, ulio sitishwa au kusimamishwa kwa muda........

Mataifa mbalimbali ulimwenguni, mathalani Russia wanakusidia kufungua balozi zao katika nchi hizo hivi karibuni :BASED:
Kimataifa yapi? Ya Afrika ama ya nchi za Magharibi? Ie; Ulaya, Marekani nk?


Na kwanini hiyo Taasisi inafanya unafiki wa kudeal na matokeo ya matatizo na sio matatizo na vyanzo vyake?

Hivi, yakitokea Mapinduzi Uganda sasa hivi ama Rwanda, nao watatengwa kwanza? Hawaoni kinachoendelea sasa hivi kabla Mapinduzi hayajatokea?
 
Back
Top Bottom