Luhaga Mpina usiondoke CCM, pambania huko huko ndani ya chama chako kuleta mabadiliko

Ndio, aende mahakamani kukwamisha kufukuzwa.
Nawe unaamini kikatiba, chama kikikufukuza Kwa kutumia Katiba Yao, mahakama unaweza kuzuia kufukuzwa kwako?

Jifunze hata kwenye mpira, Wambura Mwanasheria alipotimuliwa TFF, hakutoboa mahakamani.
 
CCM ndio kwanza inakaribia chorus(kolasi) ya muziki wa kuongoza nchi, sasa piga picha ikianza nzawisha
Umenena vyema,

Ni kama tu Ramaphosa wa SA, anawapigia magoti WAPINZANI wake Ili wasaidiane kuongoza nchi.

Huo ulevi wenu ukitoka vichwani, mtajua kifo chenu kimewadia.
 
Mmoja hatawasumbua kabisa Cartels bali wanahitajika hata 10
Hata marehemu alishindwa kwa sababu alikuwa one man gang
Kuwarudisha watu kwenye mstari kwa tabia walizozizoea ni ngumu sana peke yako ni kama unahangaika tu
 
Namkubali sana mpina, ila kwenye sukari kakosea viwanda vilikiwa vimeshakuwa cartels jambo ambalo naliona limeshakuwa kawaida kwenye mitandao ya simu ,nimejaribu line za simu tatu vifurushi ni vile vile lakini hakuna anaye jishughulisha na nape kama waziri kwa kushindwa kumoderate hawa watu,
 
Luhaga Mpina umekuwa machachari sana kuiwajibisha serikali ya chama chako tofauti na wabunge wenzako wengine wote wa chama chako. Kama utaendelea na mwendo huo unaweza kuleta mabadiliko makubwa mno ukiwa ndani ya CCM kuliko nje yake.

Wewe sasa hivi unachukuliwa kama nembo ya ujasiri ndani ya chama chako kama vile alivyokuwa Benard Membe. Tofauti na wakati wa Membe sasa mazingira ya kufanya siasa yameboreka kiasi na ndio maana mpaka sasa hujaitwa na kamati ya maadili na hakuna dalili za kukufukuza kutoka ndani ya chama au kuundiwa zengwe lolote.

Usizifuate njia za Lowassa, Slaa, Nyalandu na Membe za kuhama chama, wananchi wengi wamezichoka siasa za aina hiyo, utawapoteza kujitoa katika chama chako.
LUHAGA MPINA katika Ubora wake, amethibitisha Ule msemo unaosema NATURE DOES NOT ALLOW VACUUM
 
This guy is overrated
Mkuu ujasiri wa kukiuka kasumba ya “zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi” sio swala la mchezo mchezo ujue

Issue kubwa ni UJASIRI wa kuikososa CCM ukiwa ndani ya CCM tena ukiwa na nyadhifa ambayo umeipata kwa “hisani” ya CCM

Umejiuliza ni wangapi wamewahi kufanya kama Mpina ndani ya CCM na mwisho wao ulikuaje kisiasa na kiuchumi?
 
Luhaga Mpina umekuwa machachari sana kuiwajibisha serikali ya chama chako tofauti na wabunge wenzako wengine wote wa chama chako. Kama utaendelea na mwendo huo unaweza kuleta mabadiliko makubwa mno ukiwa ndani ya CCM kuliko nje yake.

Wewe sasa hivi unachukuliwa kama nembo ya ujasiri ndani ya chama chako kama vile alivyokuwa Benard Membe. Tofauti na wakati wa Membe sasa mazingira ya kufanya siasa yameboreka kiasi na ndio maana mpaka sasa hujaitwa na kamati ya maadili na hakuna dalili za kukufukuza kutoka ndani ya chama au kuundiwa zengwe lolote.

Usizifuate njia za Lowassa, Slaa, Nyalandu na Membe za kuhama chama, wananchi wengi wamezichoka siasa za aina hiyo, utawapoteza kujitoa katika chama chako.
Mpina yupo wrong party anapaswa kuja CHADEMA ili awaweze kutimiza wito wake vizuri, karibu sana ndugu Luhaga kwenye wapiganaji wa kweli.
 
Nawe unaamini kikatiba, chama kikikufukuza Kwa kutumia Katiba Yao, mahakama unaweza kuzuia kufukuzwa kwako?

Jifunze hata kwenye mpira, Wambura Mwanasheria alipotimuliwa TFF, hakutoboa mahakamani.
Mbona wakina Mdee, Bulaya, Nusrat n.k wametoboa?
 
Luhaga Mpina umekuwa machachari sana kuiwajibisha serikali ya chama chako tofauti na wabunge wenzako wengine wote wa chama chako. Kama utaendelea na mwendo huo unaweza kuleta mabadiliko makubwa mno ukiwa ndani ya CCM kuliko nje yake.

Wewe sasa hivi unachukuliwa kama nembo ya ujasiri ndani ya chama chako kama vile alivyokuwa Benard Membe. Tofauti na wakati wa Membe sasa mazingira ya kufanya siasa yameboreka kiasi na ndio maana mpaka sasa hujaitwa na kamati ya maadili na hakuna dalili za kukufukuza kutoka ndani ya chama au kuundiwa zengwe lolote.

Usizifuate njia za Lowassa, Slaa, Nyalandu na Membe za kuhama chama, wananchi wengi wamezichoka siasa za aina hiyo, utawapoteza kujitoa katika chama chako.
huyu ni mtu anaandaliwa kama Membe ,akachafue upinzani kisha arudi nyumbani
wapinzani chondechonde, msimpokee
 
Back
Top Bottom