Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Katika Mkutano wa wake na Waandishi wa Habari leo 14/6/2024, wakati akitoa uthibitisho alioambiwa aupeleke na Spika wa Bunge ndani ya siku 10, Luhaga Mpina amesema;
"Hapakuwa na usimamizi wa bei nchini kwani hata pale sukari ilipopatikana kwa bei ndogo nje ya nchi bado iliuzwa kwa kubwa hapa nchini ambapo mfuko wa Kilo 50 uliuzwa Tsh. 145,000. Rejea risiti Na. ya TRA ya EFD Na. 32 ya tarehe 22 Februari 2024 na risiti yenye verification code Na.28630946606 ya tarehe 23 Februari 2024 zilizotolewa na Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Limited katika ofisi za Dar es Salaam.
"Mawaziri hawa walitengeneza uhaba wa sukari, kutoa vibali vya kuagiza sukari zaidi ya mahitaji, kuruhusu sukari inayoingizwa kwa msamaha wa kodi kuuzwa kwa bei kubwa kinyume cha sheria.
"Pia msamaha huo wa kodi unapelekea Serikali kupoteza mapato ya Tsh. Bilioni 580 na kuwawezesha wafanyabiashara kupata faida ya ziada zaidi ya Tsh. Bilioni 465. Kwa maoni yangu hizi ni njama zilizosukwa na baadhi ya Viongozi na watendaji wa Serikali kuiba mapato ya nchi."
Pia soma: Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
