Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Pichani ni Luhaga Mpina
Dk Tulia ametoa maelekezo hayo wakati akiahirisha Bunge leo Jumanne ya Juni 4, 2024 baada ya mbunge huyo kudai, “Waziri Bashe amesema uongo na amevunja sheria.”
Wakati wa mabishano ya hoja kati ya Bashe na Mpina kuhusu uingizaji wa sukari ya nje, Dk Ackson amemuliza Mpina kwa kutumia kanuni ya 70 kwamba ana hakika waziri anasema uongo. Mpina amejibu “anasema uongo na kuvunja sheria.”
Kufuatia hali hiyo amesema kwa mujibu wa kanuni ya Bunge ya 70 anayesema mbunge au waziri amesema uongo ndiye anatakiwa kuleta uthibitisho.
“Naomba ieleweke siyo kwamba namuweka Mpina kwenye kona,” amesema Spika. Mpina anatakiwa kuwasilisha ushahidi wake Juni 14, 2024.
Hoja iliyosababisha Mpina kutakiwa kuwasilisha uthibitisho inahusu kiwango cha uagizaji wa sukari ya ziada nje ya nchi katika kipindi ambacho viwanda vinakuwa vimesimamisha uzalishaji.
Mpina amedai kwa mujibu wa sheria uagizaji wa sukari nje ya nchi kwa ajili ya kuziba pengo unatakiwa uwe takriban tani 150, 000 na zabuni itangazwe.
UPDATES