Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

Bottom line is, kavunja sheria gani? Maana loophole ya kisheria ni kosa la bunge sio waziri.

Kingine waziri kasema walipewa vibali hao Kagera sugar etc lakini hawakuingiza sukari mlitaka afanyeje?
Amevunja sheria inayosema Waziri alipaswa kufuata matakwa ya kibali cha bodi ya sukari, ambacho kilichosema waagize tani laki moja na ishirini tu, na sio laki nne na kumi. Hilo moja.

Mbili, unaposema Kagera Sugar hawakuagiza sukari, tulitaka Bashe afanyeje. Tunataka Bashe atueleze mfanyabiashara kaomba kibali cha kuagiza sukari, hakuagiza sukari, kwa nini hawakuagiza sukari ? Kwa nini mnatupa maelezo shallow na ya kivivu kama hayo?

Kwa nini Kagera Sugar waombe kibali halafu wasiagize sukari ????????????????????????????????????????
 
Hata iweje, Luhaga Mpina amekwisha jipambanua kuwa yeye ni tofauti na wabunge wengine ndani ya CCM.

Lililobaki ni kwa wananchi kutambuautofauti kati yake na wabunge wengine wa CCM, na kumpa shukrani anazozistahili.
Na ajiandae kabisaaa kwamba hatokirudia tena hiko kiti chake cha ubunge 🤣🤣🤣
 
Amevunja sheria inayosema Waziri alipaswa kufuata matakwa ya kibali cha bodi ya sukari, ambacho kilichosema waagize tani laki moja na ishirini tu, na sio laki nne na kumi. Hilo moja.

Mbili, unaposema Kagera Sugar hawakuagiza sukari, tulitaka Bashe afanyeje. Tunataka Bashe atueleze mfanyabiashara kaomba kibali cha kuagiza sukari, hakuagiza sukari, kwa nini hawakuagiza sukari ? Kwa nini mnatupa maelezo shallow na ya kivivu kama hayo?

Kwa nini Kagera Sugar waombe kibali halafu wasiagize sukari ????????????????????????????????????????
Mbona kaeleza kuwa walifanya hivyo ili kukiwa na shortage wauze kwa bei kubwa. Kaeleza kilo moja iliuzwa elfu 3 bei ya jumla!

Sasa tunataka sukari iwe shortage au cheap? Maana ikipungua tunalalamika, ikizidi tunalalamika. Ina maana hamtaki bei ishuke?
 
Sukari ni sarakasi tu ya Wafanyabiashara wakubwa na Serikali naona Spika yupo upande wa Serikali ila ukweli anaujua wacha aendelee kuwabeba watu wachache sikutegemea Spika kufanya hiki anachokifanya...
 
Aliombwa ushahidi lini juu ya hili na hakupeleka?
Kama ushahidi wa waziri mkuu kupulizwa ulipelekwa ni hatua gani zikichukuliwa?
Unaelewa nachohoji? Kuna mdau Nanye Go kadai Mpina hajawahi kudanganya bungeni?

Ndio nikasema alidanganya kuhusu miamala shuku ya thamani ya Trillion 120 kuwa ni pesa za wizi ilihali ilikua ni enquiries tu sio kwamba zilikutwa na hatia.

Same to suala la Trillion 30 alizosema zimepigwa akaulizwa mbona bajeti ni 50 Trillion pekee!! Akakosa majibu alipoulizwa na Mwigulu.

Ndio sasa nasema SIO KWELI kwamba ANATOAGA USHAHIDI kwa upotoshaji anaofanya Bungeni.
 
Bashe anatosha sana kwenye bongo movie jamaa ni muigizaji mzuri sana bungeni anavyoongea kwa machungu utadhani anajali kweli.

Nilidhani atakataa hawajatoa vibali vya kuagiza tani łąki nne, nikasikia hadithi za viwanda kutozalisha kwa miezi nane toka mwezi wa kumi mwaka jana.

Sasa kama walikuwa awazalishi na pamoja kupewa vibali hawakufanya hivyo kwenye magodown yao walikuwa wanaenda kupekuwa nini sukari ilipoadimika.

Doesn’t add up, Bashe ndio muongo story yake aipo consistent.
We naye huelewi kitu, Bashe kasema walipewa vibali hawakuleta sukari between December to late February.

Na walipoleta wakazificha ili scarcity iendelee kuwepo so ikabidi ndio atoe vibali vingine.

Mpina anachodai ni kwamba alitoa vibali kinyume cha sheria ilihali waziri anasema sheria haimlazimu kutoa tender.

So Mpina amejikita kwenye madhaifu ya sheria na sio kwamba waziri ndio kakikuka sheria.

Anyway mmeambiwa kuleta ushahidi, so kuliko kutukana humu nendeni mkamsaidie kuleta huo ushahidi kuwa technical teams ziltaka Tani laki moja ishirini na sio tani laki nne na kumi!!
 
Sukari ni sarakasi tu ya Wafanyabiashara wakubwa na Serikali naona Spika yupo upande wa Serikali ila ukweli anaujua wacha aendelee kuwabeba watu wachache sikutegemea Spika kufanya hiki anachokifanya...
Sijaelewa bado shida ni nini? Sukari imeagizwa nyingi na kweli bei imeshuka sasa mlitaka nini? Vibali visitolewe ili sukari iwe chache kama January?
 
Vitu unavyohoji ni vikubwa sana kwako mkuu..
Jibu swali, kama deficit ya Tani laki 4 na 10 alafu iliyoletwa ni Tani laki 2 na 20 so far sasa kivipi sukari imezidi mahitaji?

Unajua waTanzania ujuaji ni mwingi kuliko uhalisia. Maana bei imeshuka na sukari inapatikana sasa mlitaka iweje?
 
Na ajiandae kabisaaa kwamba hatokirudia tena hiko kiti chake cha ubunge 🤣🤣🤣
Kwa hiyo kiti cha ubunge ni muhimu zaidi ya anachokiamini yeye kuwa kiko sawa; na kwa sababu hiyo anyamaze!

Sijui kama ulihitaji kuambiwa hilo ili ufahamu tofauti ya Luhaga na hao wabunge wengine, kwa sababu ni jambo lililowazi kabisa.

Sasa wewe hapo 'mjenzi wa kale', kinachokutoa akili hapa ni kipi hasa, unatarajia kupata hicho kiti cha ubunge atakachokiacha Luhaga Mpina?
 
Jibu swali, deficit ya Tani laki 4 na 10 alafu iliyoletwa ni Tani laki 2 na 20 so far sasa kivipi sukari imezidi mahitaji?

Unajua waTanzania ujuaji ni mwingi kuliko uhalisia. Maana bei imeshuka na sukari inapatikana sasa mlitaka iweje?
Hakuna uhaba wa Sukari kinachofanyika ni sarakasi tu ili watu wachache wafanye biashara kwa kupata vibali kwa kutoa rushwa kubwa...Sukari tunayotumia Tanzania ni ya kiwango cha chini sana tofauti na Nchi zingine ambazo Ilovo wapo kuanzia Eswatin,SA,Zimbabwe,Zambia na hapa kwetu baadhi ya hizo Nchi uzalishaji unazidi mahitaji mpaka inafikia wanachoma moto zilizopita muda maana Eswatin pana muda wanakua na Sukari tani 800,000 kwa mwaka wakati Tanzania miaka yote wao wana upungufu tu ili watengeneze dili kama wanavyofanya ukitaka ujue viwango bora vya Sukari agiza hapo Zambia uone ubora wa sukari sio haya Mavumbi tunayoambiwa muda wote hayapo...
 
Kwa hiyo kiti cha ubunge ni muhimu zaidi ya anachokiamini yeye kuwa kiko sawa; na kwa sababu hiyo anyamaze!
Sijui kama ulihitaji kuambiwa hilo ili ufahamu tofauti ya Luhaga na hao wabunge wengine, kwa sababu ni jambo lililowazi kabisa.
Sasa wewe hapo 'mjenzi wa kale', kinachokutoa akili hapa ni kipi hasa, unatarajia kupata hicho kiti cha ubunge atakachokiacha Luhaga Mpina?
Ahahahah mkuu KALAMU hujanielewa, mimi hapo nimeongea kifasihi zaidi.....no kwamba kwa akili za watu wa ccm zilivo kwamba hawapendi watu wa kuhoji na kutumia akili hvo huyu Luhaga haji kuwa tena sehemu ya timu yao.....
 
Back
Top Bottom