GE2025 Luhende: Tutaweka kompyuta kila shule ili watoto wetu wajifunze

GE2025 Luhende: Tutaweka kompyuta kila shule ili watoto wetu wajifunze

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukene mkoani Tabora kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Luhende, ameahidi kuhakikisha anaboresha sekta muhimu za maendeleo ikiwemo barabara, afya, elimu, kilimo na upatikanaji wa umeme endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge, pembezoni mwa Ofisi ya CCM Kata ya Bukene, Luhende amesema dhamira yake ni kufungamanisha sekta hizo ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Bukene.

 
Back
Top Bottom