LUKU inakula umeme sio poa

LUKU inakula umeme sio poa

Hizi mita wanazofunga sasa nahisi zina changamoto fulani

Ova
 
Toka tarehe 22/12 umeme unaenda kwenye luku sio poa. Wastan wa units 28 Kwa siku Kwa nyumba ya kutumia balbu 5 na friji, TV
Kuna loose connection kwenye waya ya neutral au kuna shoti mahali. Ita fundi aje arekebishe laasivyo muda si mrefu kitaumana.
 
Hapa tu ndipo ninapowaoneaga wivu baadhi ya Wafanyakazi wa TANESCO aisee
 
Mimi niliweka umeme wa 20000 na nikapata unit 56 tangu mwezi wa 10 tarehe 2 mpaka leo nimebakiwa na Unit 2.04. lengo nikae na zilizobaki Hadi tarehe 7.

NB:Sina familia naishi alone nasishindi gheto
 
Mchawi AC, huyo jamaa kama anatumika usiku kucha lazima uipate fresh!!(kuna ac inatumia hadi 2units/hr)
Kabla ya ac nlikua natumia unit 6 kwa siku bado naona ni mwingi kwa vitu hivyo
 
Ukisoma comments za watu kwenye huu uzi unaweza hisi Tanesco inatoa huduma kwa raia wa nchi tofauti kumbe wote wapo Tanzania.
 
Toka tarehe 22/12 umeme unaenda kwenye luku sio poa. Wastani wa units 28 Kwa siku Kwa nyumba ya kutumia balbu 5 na friji, TV
Duuuuuuh hata kama ungekua na AC umeme usingeenda hivi hapo kuna tatizo
 
31.12.2023 niliweka wa 20,000 (56 units) Jana tarehe 02.01 umeisha
Mkuu cheki na fundi lazima kutakuwa na shida mahali au hata leakage, pia kingine unaweza fanya jaribio rahisi kama itawezekana angalia salio la unit zako kisha zima main switch yako baada ya muda kiasi cheki tena salio la unit zako ukikuta imepungua hata kidogo kiasi gani ujue kuna tatizo

Vinginevyo cheki na fundi, yeye ataangalia vitu unavyotumia na kukadiria matumizi yako kama yatazidi basi kuna tatizo kwa hakika


Kuna jamaa mmoja alikuwa analalamika umeme unaenda sana, kumbe kuna TV la mtumba alichukua ndio kimeo, ukicheki screen kubwa picha ang'avu ila linakula unit hata pasi ikasome, ndio hivyo ikabidi iwe inawashwa kwa machale
 
1. Kuna shoti mahali,
2. Angalia Earth yako Kama iko vzur
 
Binafs kwangu natumia unit 28(umeme wa elfu 10) Siku nne, na nna makorokoro mengi kuliko yako mtoa mada. Huenda Kuna shida mahali
 
Kaka jirani umeme wako umeunganisha na mabanda ya kuku masaa 24 taa za joto zinawaka unadhani umeme utakosa kwenda sana?
 
Back
Top Bottom