Napendekeza watoe specifications ya mita ya LUKU iwe kama simu vile, zitengenezwe commercially. Wewe unanunua line (account) yako TANESCO buku tu mita unanunua kwa wauzaji mbali mbali mitaani.Kwa mara nyingine tena Tanesco inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali...
Toka kwa shemeji uone ilivyo kero kununua na kuweka
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Tunaheshim mawazo yako:Kwa mara nyingine tena Tanesco inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali.Kama ilivyokuwa kwa kubadilisha nguzo za miti na kuweka nguzo za zege...
Inawezekana wewe hujafahamu ninachokieleza...ukitengeneza mpango wa mabilioni kubadilisha mita za umeme wakati zilizopo hazina tatizo la kiufundi wakati unalalamika huna fedha za kukamilisha usambazaji wa umeme vijijini na pia unaongeza gharama za kuweka umeme inashangaza sana.Tunaheshim mawazo yako:
Lakini inaonekana huna ufaham wa faida zitokanazo na luku za digital! jipe muda ku study lengo lao! Utawashukuru sana!
Kongole kwa TANESCO, hakika unapokuwa popote ni unajaza tu bila kugusana na luku yenyewe! kama vocha tu!
Unajua kuna mita ngapi za umeme chini ya TANESCO?na zinagharimu kiasi gani?hivi kweli Tanesco inaweza kujigamba kununua na kubadilisha mita zote za luku?kama mteja anahitaji kubadilisha basi gharama iwe ya mteja mwenyewe na siyo ya Tanesco...Tanesco ina vipaumbele vingi kuliko hiki.Huyu jamaa hajui kero zake, kuna muda umeme unakata afu ile mita ya kuwekea luku sehem ya betri mbovu unaanza gongea majirani. Hio ya digital ndo mpango mzima.
Hizi sio lawama ni ushauri na siku zote ushauri haulazimishwi kama wanaona ni sawa waendelee na mpango...in short binafsi sioni sababu ya kubadilisha hizi Luku kwa gharama ya fedha za umma wakati hazina tatizo lolote.mteja binafsi na wateja wapya wanaweza kugharamia na kuweka mfumo mpya...Wabongo ni lawama kila kitu, hawana jema wala moja. Serikali iruhusu ndoa za jinsia moja watu kama watoa mada tuwaoe tu labda akili zao zitakuwa sawa.
Huyu jamaa hajui kero zake, kuna muda umeme unakata afu ile mita ya kuwekea luku sehem ya betri mbovu unaanza gongea majirani. Hio ya digital ndo mpango mzima.
Tunazidi sana kulalamika.Kwa mara nyingine tena Tanesco inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali.
Kama ilivyokuwa kwa kubadilisha nguzo za miti na kuweka nguzo za zege.
Tanesco itaondoa luku ambazo hazina matatizo yoyote kwa mteja au Tanesco na kuweka hizo mpya za kigitali wakati Tanesco ina madeni mengi na pia inashindwa kutekeleza miradi yake ikiwemo urekebishaji wa mifumo ya umeme na kuondoa ukatikaji wa umeme.
Nashauri uondoaji wa luku za zamani utegemee mahitaji binafsi ya mteja na ajigharamie mwenyewe kubadilisha luku na pia luku za kidigitali zitolewe kwa wateja wapya. Kubadilisha luku zote ambazo hazina tatizo lolote ni ubadhirifu na uchafuzi wa mazingira na sio kipaumbele cha tanesco wala matatizo yanayowakabili watumiaji.
We ni kichwa ngumu..Kila kitu Tz ni kupinga tuu