Lukuvi ajibu tuhuma za baadhi ya wanasiasa kujimilikisha ardhi. Asema umilikishwaji hufanyika kwa kuguata sheria na hakuna kiongozi aliyejimilikisha a

Lukuvi ajibu tuhuma za baadhi ya wanasiasa kujimilikisha ardhi. Asema umilikishwaji hufanyika kwa kuguata sheria na hakuna kiongozi aliyejimilikisha a

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekanusha vikali kauli iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwa kuna baadhi ya viongozi wamepora ardhi ikiwemo ardhi ya eneo la Mbarari mkoa wa Mbeya na kusisitiza kuwa kati ya viongozi waliotuhumiwa hakuna hata kiongozi mmoja aliyepora ardhi.

Hata hivyo, Waziri Lukuvi alisema umilikishaji ardhi nchini unafuata sheria na serikali haina ubaguzi katika kumilikisha mtu yeyoye ardhi huku akiweka wazi kuwa umilikishaji ardhi kwa mtu yeyote hauna kikomo.

Lukuvi amekanusha uvumi huo jana alipokutana na waandishi wa habari mkoani Iringa akitolea ufafanuzi wa baadhi ya kauli zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa vyama vya siasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.

“Serikali ya awamu ya tano haina ubaguzi wa kumilikisha ardhi na mwananchi yeyote bila kujali itikadi ya chama cha siasa anaweza kumilikishwa” alifafanua Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, Seriali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kushughulikia masuala ya ardhi ikiwemo lile la kuvibakisha vijiji 920 kati ya 975 vilivyokuwa kwenye hifadhi na kubainisha kuwa, serikali inaangalia namna ya kuvibakisha vijiji vingine 55 vilivyosalia.

Akitolea ufafanuzi suala la Mbarari, Lukuvi alisema wananchi wanaoishi katika vijiji 29 eneo la Mbarari wameamuriwa kubaki eneo hilo ingawa kwa mujibu wa GN Namba 28 ya mwaka 2008 walitakiwa kuondoka lakini kwa huruma ya Rais John Pombe Magufuli alibatilisha uamuzi huo na kuagiza vijiji visiondolewe.

“Wananchi wa Mbarari waendelee kuishi kama wanavyoendelea, Mgogoro wa Mbarari ni wa muda mrefu tangu mwaka 2008 na serikali ya awamu ya tano haipaswi kulaumiwa na Rais Magufuli siyo mtu wa kubeza kwa kuwa vijiji vilitakiwa kuondolewa lakini aliamuru vibaki” alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, baada ya uamuzi wa kutoviondoa vijiji 920 kati ya 975 hatua inayofuata ni kupima upya mipaka sambamba na kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kubainisha matumizi ya maeneo ya maeneo husika.

Vile vile, Lukuvi alisema serikali katika kuwajali wananchi imeamua pia kufuta mapori tengefu 12 yenye zaidi ya hekta 707,659.4 sambamba na kumega hifadhi 14 za misitu kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji.

Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, serikali ya awamu ya tano imeendelea kuchukua hatua za kupunguza na kufuta mashamba makubwa kwa wamiliki waliokiuka masharti ya umiliki na kubainisha kuwa, kwa sasa serikali imeshafuta mashamba yasiyopungua 49 na kugawiwa kwa wananchi.

Akigeukia tatizo la ardhi katika mkoa wa Morogoro, Waziri Lukuvi amesema kazi ya uhakiki mashamba 11 katika eneo la Kilosa imekamilika na muda ukiruhusu watatangaziwa mashamba yaliyofutwa kutokana na wamiliki wake kukiuka masharti ya umiliki.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alihitimisha mkutano wake na waandishi wa habari kwa kutoa onyo kwa wananchi wote waliomilikishwa ardhi kuhakikisha wanafuata sheria na kusisitiza kuwa, sheria za ardhi zimewekwa ili kutekelezwa na wasiozifuta watafutiwa umiliki na kupatiwa watu wengine.
 
Ni vyema Lukuvi kuweka wazi sasa orodha ya viongozi wakuu wote wastaafu (Rais, Makamu wa rais na Waziri mkuu) maeneo ya ardhi wanazozimiliki kisheria hapa Tanzania, Ukubwa wa hayo maeneo, ni lini walimilikishwa na utaratibu uliotumika kuwamilikisha ili kuondoa maneno ya pembeni na mtaani. Na kwa kuanzia, aseme sasa yanayomhusu Magu, maana ni mtumishi wa umma.

Na kama waziri atashindwa sasa, basi sisi tutaendelea kuamini kile kinachosemwa na watu huku pembeni na pia tutahisi kuna udhalimu katika hilo.
 
Lukuvi badala ya kumtetea boss wake kazidi kumchonganisha. Lukuvi ni kama anathibitisha magufuri kweli anamiliki hilo eneo kwa kufuata sheria..
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekanusha vikali kauli iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwa kuna baadhi ya viongozi wamepora ardhi ikiwemo ardhi ya eneo la Mbarari mkoa wa Mbeya na kusisitiza kuwa kati ya viongozi waliotuhumiwa hakuna hata kiongozi mmoja aliyepora ardhi....
CCM MWAKA HUU KIDAGAA KIMEWAOZEA
 
Kwa hiyo Lukuvi anataka kusema kuwa ni kweli Magufuli anamiliki zaidi ya Ekari 25000 za ardhi ambazo amezichukua kipindi hiki cha miaka mitano wakati akiwa Rais?

Maana Tundu Lissu ndio alitufungua macho kuyajua hayo ya sirini.
We ulikuwa ujui? Sisi wa karagwe tunajua mchezo mzma kihanga yote kajimilikisha
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekanusha vikali kauli iliyotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwa kuna baadhi ya viongozi wamepora ardhi ikiwemo ardhi ya eneo la Mbarari mkoa wa Mbeya na kusisitiza kuwa kati ya viongozi waliotuhumiwa hakuna hata kiongozi mmoja aliyepora ardhi...
Lukuvi ni empty set.

Aeleze kwanza msimamo wake juu ya Zanzibar
 
Hapo Tunasema Ni Kama Kuchambia Mgomba
Yaani Unateleza Badala Ya Kuondoa Mnyaa Ndiyo Mnyaa Imepakazwa Mtu Ananuka
 
Kuna tuhuma moja hajaijibu
Hekali elfu 25 ,kihanga Karagwe
Wamechanganyikiwa hadi hawajui waseme lipi na lipi walisahau,na bado LISSU toa nyoka zote zilizo jificha pangoni
 
Kwa hiyo Lukuvi anataka kusema kuwa ni kweli Magufuli anamiliki zaidi ya Ekari 25000 za ardhi ambazo amezichukua kipindi hiki cha miaka mitano wakati akiwa Rais?

Maana Tundu Lissu ndio alitufungua macho kuyajua hayo ya sirini.
Screenshot_20200926-213641.png
 
Mahitaji halisi na ya uhakika ya mwanadamu
Si zaidi ya 2×6 ft ya ardhi
Yalobaki yote ni mapambo ya dunia tu
 
Back
Top Bottom