GE2025 Lukuvi ashinda kwa kwa tofauti ya kura 4,587 Ismani

GE2025 Lukuvi ashinda kwa kwa tofauti ya kura 4,587 Ismani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mbunge aliyemaliza muda wake wa Jimbo la Ismani, William Vangimembe Lukuvi, ameibuka mshindi wa kishindo katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo, akiwashinda wagombea wenzake kwa tofauti kubwa ya kura.

Huku wananchi wa Kihorogota na Kising'a wakieleza kuwa ushindi wa Lukuvi ni ishara tosha kuwa Oktoba wanatiki kwa uzido huo kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

"Tunataka kuonesha watu wanaosema wamekuja kumstafisha Lukuvi ubunge kuwa sisi wananchi bado tunamuitaji Lukuvi wetu kazi kubwa ameishanya jimboni hata kama wao wanadai ni mzee basi sisi ni mzazi wetu tunae na tunatamba nae "

Katika matokeo yaliyotangazwa rasmi kutoka kata zote 13 za Jimbo la Ismani, Lukuvi amepata jumla ya kura 5,746 huku mpinzani wake wa karibu, Festo Kiswaga, akipata kura 1,159 tu.

Tofauti ya kura baina yao ni kura 4,587, hali inayoonesha jinsi wanachama wa CCM katika jimbo hilo walivyomuamini Lukuvi kuendelea kuwa mwakilishi wao.

Katika kata ya Mahuninga, Lukuvi alipata kura 421 dhidi ya Kiswaga aliyepata kura 28. Hali kama hiyo ilijirudia katika kata ya Malenga Makali ambako Lukuvi alipata kura 464 huku Kiswaga akipata 139. Kata ya Migoli ilimpa Lukuvi kura nyingi zaidi—kura 644, huku Kiswaga akijikusanyia kura 84.

Kwenye kata ya Kihorogota, Lukuvi alipata kura 431 dhidi ya 63 za Kiswaga. Kata ya Kising’a Lukuvi alipata 448, huku Kiswaga akipata 40.

Kata nyingine kama Izazi, Mboliboli, Itunundu na Ilolo Mpya pia zilimpa ushindi wa kushangaza, akizidiwa tu kwa ukaribu katika kata ya Mlowa ambapo alipata kura 350 huku Kiswaga akiwa naye karibu kwa kura 340.

Kata ya Idodi ilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyompa Lukuvi kura nyingi zaidi, akipata kura 676 dhidi ya 26 za Kiswaga, wakati kata ya Mlenge ilimpa Lukuvi kura 610 huku Kiswaga akipata 200. Kata ya Nyang’oro Lukuvi alipata kura 461 dhidi ya 90 za Kiswaga.

Ushindi huu wa Lukuvi unadhihirisha namna ambavyo bado ana ushawishi mkubwa ndani ya chama na kwa wananchi wa Jimbo la Ismani.

Wananchi wengi wamekuwa wakimuelezea Lukuvi kama kiongozi mwenye maono, anayejua changamoto za eneo hilo na mwenye uzoefu wa kutosha katika siasa za kitaifa na maendeleo ya jamii.

Kwa ushindi huu mkubwa, Lukuvi anatarajiwa kupeperusha tena bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao iwapo chama kitampitisha , huku matarajio ya wananchi wake yakiwa ni kuona kasi ya maendeleo inaendelezwa pale ilipoishia.


:::::::::::::::::::::::::

🗳️ MATOKEO YA KURA ZA MAONI CCM – NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI
🟢 Matokeo ya kata 13 zote za Jimbo la Isimani

1. Kata ya Mahuninga – William Lukuvi: 421 | Festo Kiswaga: 28
2. Kata ya Malenga Makali – William Lukuvi: 464 | Festo Kiswaga: 139
3. Kata ya Migoli – William Lukuvi: 644 | Festo Kiswaga: 84
4. Kata ya Kihorogota – William Lukuvi: 431 | Festo Kiswaga: 63
5. Kata ya Kising’a – William Lukuvi: 448 | Festo Kiswaga: 40
6. Kata ya Izazi – William Lukuvi: 340 | Festo Kiswaga: 22
7. Kata ya Mboliboli – William Lukuvi: 250 | Festo Kiswaga: 20
8. Kata ya Itunundu – William Lukuvi: 299| Festo Kiswaga: 48
9. Kata ya Ilolo Mpya – William Lukuvi: 403 | Festo Kiswaga: 59
10. Kata ya Nyang’oro – William Lukuvi: 461 | Festo Kiswaga: 90
11. Kata ya Idodi – William Lukuvi: 676 | Festo Kiswaga: 26
12. Kata ya Mlowa – William Lukuvi: 350 | Festo Kiswaga: 340
13. Kata ya Mlenge – William Lukuvi: 610 | Festo Kiswaga: 200

📊 Jumla ya Kura Kata 13:
  • William Lukuvi: 5,746
  • Festo Kiswaga: 1,159
➡️ Tofauti ya kura kati ya mshindi namba moja na namba mbili: 4,587
 
Aseee HIVI HUYU mzee huwa hachoki au hanaga KAZI zingine?


Kwishaaaa
 
Huyo Mzee kajimilikisha jimbo kwa miongo 3..... wabongo bhana
 
Lukuvi hajawahi kula Mshahara wa Mbunge kwa miaka yote, Mshahara wa bunge wa miaka mitano anautuza kwa ajili ya kuwanunua wajumbe kwenye kura za maoni. Anayo timu ya ndugu zake kwa ajili ya kuratibu rushwa kila kata

Sijui kama mnanielewa
 
Back
Top Bottom