Lukuvi hivi unawatafuta nini wananchi kwenye ardhi? Hebu tuliza spidi unaenda kasi isiyo na faida

Lukuvi hivi unawatafuta nini wananchi kwenye ardhi? Hebu tuliza spidi unaenda kasi isiyo na faida

Majuzi umetoa kauli tata kuhusu umiliki wa ardhi katika ndoa, tumekueleza kuwa uwe makini na kaulikauli hizi

Kisha naona unatoa kauli nyingine kutishiatishia wananchi kutwaa ardhi zao.

Ni hivi ndugu Lukuvi, sisi wananchi hatupendi stress, kutishwatishwa, kusukumwasukumwa, kupelekwapelekwa.

Kama ardhi tunazimiliki kihalali, wewe tulia ofisini uje na mawazo yenye tija juu ya namna ya kuboresha umiliki wa ardhi, kuboresha masuala ya mipango miji. Lakini siyo kila ukiamka unaanza kutupigapiga mikwara, mara hili mara lile.

Lukuvi kwani ukikaa ofisini ukapanga mipango mizuri ya wizara unaona hiyo ni kazi ngumu isipokuwa kutishatisha wananchi kunyang'anya ardhi zao?

Najua serikali inataka kodi ya ardhi kama chanzo cha kodi, lakini katika kipindi hiki cha December ambapo wananchi tuna mambo mengi yanayohitaji pesa unakuja kupushpushwananchi utadhani askari Magereza anavyopush wafungwa hayo mambo sisi wananchi hatuyataki!

Lukuvi Kama umedhamiria kufuta hati za wananchi, Au kunyang'anya mali za wananchi hebu fuata sheria, haya mambo ya kupelekeshanapelekeshana hatutaki.

Hivi nyie viongozi, mtaanza lini kuheshimu wananchi badala ya kujiimpose juu yetu utadhani nyie ni manyapara wetu?

Lukuvi awamu hii umeanza na mguu mbaya, hebu tuliza ball kwanza, Mambo ya msingi hayataki manguvunguvu. Tuliza mshono, achana na mawazo ya unyang'anyinyang'anyi, fanya kazi zenye tija!

View attachment 1657580
🤣🤣🤣
 
Ameyasema hayo lini?

Yani December hii na siku kuu zote hizi halafu useme watu wajenge?

Bora asubiri mwezi March huko kisha aseme hadi December watu wajenge walau itakuwa afadhali Yani atoe walau mwaka mzima hivi mtu anaweza kudunduliza kujenga ukuta
 
Tatizo lingine ni usumbufu na urasimu mkubwa katika utolewaji wa Vibari vya ujenzi.

Atoe tamko watu wajenge bila vibari aone kama watu baadhi hawatajenga.
 
wengine hununua viwanja au mashamba kwa mikopo ya muda mrefu.

Hivyo mara nyingi mtu husubiri amalize kukatwa mkopo wa Ununuzi wa kiwanja au shamba kisha akope tena mkopo mwingine kwaajili ya ujenzi.

Kwa hiyo msisitizo uwe ktk kulipia kodi na kusafisha mara kwa mara!
 
Walivunja nyumba za wananchi wa Kimara-Mbezi kwa ukatili mkubwa, sasa wanataka kupora wananchi ardhi.
Hawa jamaa ni makatili haijawahi kutokea
 
Back
Top Bottom