Otorong'ong'o
JF-Expert Member
- Aug 17, 2011
- 37,957
- 26,414
hakuna suala la ukristo hapa mnajichanganya
mimi nakubaliana na mawazo ya wewe mleta mada dhidi ya Lukuvi ila si ukristo dhidi ya uislam
wala wakristo hawana hila na waislam na hakuna trick hapa
wewe Faizafox unakwepa kuihusisha CCm moja kwa moja unakimbilia ukristo maana wewe na hili Dubwana CCm ni A+
hapa tatizo ni CCM na nia yao, pale Lukuvi hana nia mbaya na Uislam ila anautumia uislam na kanisa Kuendelea kuifanikisha mbinu ya CCM kuendelea kutawala kwa hila.
hapa kunaletwa fitina kati ya Dini ili CCm iendelee kuwapo, mleta mada unaificha CCM unaibua adui katika mzozo eti ni ukiristo na serikali ya mfumo flan, lukuvi unamfanya minor kwenye hii ishu huku CCM ukiiondoa kabisa. Tafakari upya!
kama serikali ingekuwa mfumo kristo basi mwinyi, kikwete wasingelikuwa watawala. hapa tatizo ni CCM kucheza na akili za Dini kuendelea kuwapo madarakani na matakwa yake kufanyika, tena wanajua kabisa waislam mkiguswa tu balaa lkn bado wanaujasri wakuwatumia pande zote kufanikisha mambo yao na kuharibu wasichotaka...lol
kweli aliezoea kuishi kwa hila....
pesa nayo ni sabuni ya roho kwani Bungeni waliokuwa wakimpigia makofi na hata bila kuomba miongozo juu ya lukuvi pale hawakuwapo waislamu? au wazanzibari ambao pia ni waislam? lakini pesa imewazima, kimyaaa wameweka dini na utaifa wao pembeni, CCM mtoa kitu anaatumikiwa kwa uaminifu, hapa ndipo ninapopenda propoganga za masisiemu yanawachanganya kisha mnakuja kulia huku. ila kwakuwa anakitu aaaah, hamtoki hata Dini zenu zibamizwe.
sisiem wagawe uwatawale.....na imewabamba leo sasa FaizaFox hutaki kuitaja CCM unawaleta wakristo kama ndio adui, hata Lukuvi si Adui anasmamia kazi ya Dubwana linaitwa CCM, akitemwa tu hata leo yupo tayari kukubali serikali 3
na kuamini na kutangaza uislam na ukristo ni imani tu za watu wala si mbaya alimradi wote ni wafuasi wa mungu wa amani
Well said...