Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.

Well said...
 

Mnapotosha
Kauli ya lipumba inahusu kumtambua kikwete siku ya kutangazwa matokeo.
Cuf ndio walikuwepo na wakayatamnua matokeo na kikwete alimkumbatia kumpongeza.
Sio kumsaidia kupata kura.cuf wenyewe hawakua na mtaji wa maana uchaguzi ulopita sasa alimsaidia vipii.
Hata kama alimpa tough ya kutambua udhindi na hapo msikitini alizungumza umuhimi wa kujipanga kwa waislam kwenye mambo yasiasa.
Hakutaja kanisa kuwa linataka kuanzisha uktisto tanzania
Hapa tunaxungumzia waziri akisema waislam wa unguja wataleta dola ya waislam na makanisa yatavunjwa..huu nii ujuni na interharamwa style ...ni fitina kubwa sana..
 
Mkuu mimi ni Mkristo Mkatoliki. Tumtofautishe Prof. Lipumba,Mwenyekiti wa CUF Taifa na Waziri ktk Serikali yetu ya JMT. Lukuvi amefanya makosa makubwa,kama ingekua nchi nyingine ameisha jiuzulu!

Kweli. Lukuvi ni Waziri katika serikali lakini si kiongozi mkuu wa hiyo serikali. Aidha, sijawahi kumsikia akitaka urais. Huyu mwingine ni kiongozi Mkuu wa chama kikubwa cha siasa nchini mwetu na ameshagombea urais mara kadhaa. Kwa maana hii, Lukuvi hawezi kushika nchi lakini uwezekano wa Lipumba kushika nchi upo. Sasa nani anatakiwa kuwa responsible zaidi katika matamshi yake?

Amandla.......
 
Baada ya Lukuvi kuzidi kutetea kuiwa serikali ya Zanzibar kwa kuhoji kuwa Zanzibar itakuwa nchi ya kiislamu yenye msimamo mkali ambao utahatarisha maisha ya Wakiristu na majumba yao ya ibada ,wale WaZanzibari maCCM ambao walipokuwepo Zanzibar walikuwa kitu kimoja na walipofika Dodoma na kupigwa brush kwenye vikao lukuki vilivyoitishwa na Chama Cha CCM kwa wanachama wao na kuwapa muwasho uliowaweka maCCM Zanzibar kama wanakasoro.

Lukuvi akijiamini kuwa MaCCM waZanzibar walioachwa bungeni baada ya wenzao kuondoka na Ukawa hawazimi hawawashi na wamekuwa kama kuku walionyonyolewa ,wapowapo tu wengine wakibaki kurembua na wengine wamejitia mirangi ya uso na midomo ,sasa hivi wazenji hao maCCM kusema kweli wamepwaya viba sana na hawajui watetee kitu gani kwani waliokuwa wakiwashambulia kwa matusi ,hawapo tena na hawatorudi.
Na habari iliyopo mitaani ni kuwaomba Ukawa warudi na kama ikishindikana kinachofuatia ni kuvunja bunge hilo.
 
ndugu zangu wanajf ninawaomba kwa heshima na taadhima wakati huu si wakuangalia dini hebu tujitahidi kwa pamoja tudai tanganyika yetu atakae kuwa mkristo au muislam ni imani yake kwa manufaa yake na anachotaka kufanya lukuvi na hao wasakatonge wenzake ni kuvuruga mada ili tugeukie dini tusitetee wala kupigania nchi yetu
 
kumbe bi mkubwa linapokuja suala la dini chama unakitupa pembeni????????
 

Mkuu,

Umejitahidi kunena/kuelekeza mangi...lakini ndo bado waregea kule kule!? Yaani umeidhoofisha bayana yako kwa kuelekeza personal grievances zako dhidi ya CCM, badala ya kujikita kwenye mada dhidi ya Lukuvi kupewa fursa na Viongozi wa Kanisa kueneza Islamophobia kwa waumini!? Daah! Au weye Mkuu hilo huoni kama ni tatizo!?

Pia unaposema yakua ati Wakristo hawana matatizo/khofu dhidi ya Watanzania wenzao wenye imani ya Kiislam!?...hivi Mkuu kweli weye unajiaminisha kuwa ndo mouth piece ya Wakristo woote hapo nchini!? Hata yule Cardinal Pengo pia pana Wakristo kadhaa ambao hawakubaliani na baadhi ya misimamo/fikra zake...sembuse weye Mkuu!? Daah!

Kwa kifupi,umeidhoofisha bayana/post yako kwa kuweka kimbelembele cha chuki zako kwa wale CCM!

Mada sensitive kama hizi, inalazim tujitahidi kujadili kitaaluma zaidi na kwa pamoja...bila ya kujali mno misimamo/itikadi zetu za kisiasa!?

Ahsanta sana.
 
Naona leo siku nzima unani-quote tu mie basi chukua hii bayana kiduchu.

Nitarudi punde hapa ukumbini.

Cc; gombesugu THE BIG SHOW wabara Sword
 
Last edited by a moderator:
Patriot
===>Walikuwa hawajajua undani wa Magamba,hawana lolote ndio michezo yao hyo kila wakati kucheza na imani za watu halafu wavimbishe matumbo yao,sasa bora ukweli umedhihirika.
 
Last edited by a moderator:
Ritz
===>Kumbe ulikuwa hujui kuwa mnaowatetea wana AGENDA zao za siri?Poleni sana.
 
Last edited by a moderator:

Unaepotosha ni wewe. Lipumba alizungumzia kutetea haki ya wale aliosema ni raia wa daraja la pili dhidi ya makafir. Amesema wazi kuwa dua yake ni kuwa Mwenyezi Mungu amnusuru na makafir. Lukuvi amesema anaogopa uislamu na hususan aina ya uislamu unaoijochomoza Zanzibar. Mifano aliyoitoa ni ya kweli. Au unataka kutuambia kuwa wakristu hawajapigwa risasi, makanisa yao kuchomwa, hawaja mwagiwa tindikali, biashara zao kuvunjwa n.k. huko Unguja? Alipokosea Lukuvi ni kutumia vitendo vya waislamu wachache kujenga hofu katika wakristu dhidi ya uislamu. Lipumba nae alikosea alipotaka kujenga imani kuwa hali duni ya waislamu unatokana na wakristu.

Amandla.....
 
Mkuu gombesugu.

Haya pitia hii bayana kiduchu.
Duu!!!
 
Last edited by a moderator:
Ritz
===>Kumbe ulikuwa hujui kuwa mnaowatetea wana AGENDA zao za siri?Poleni sana.
Mimi sipo humu kutetea mtu mimi napambana na mfumo kristo, nisome nimeandika mengi sana kuhusu haya majambo, mkuu kwa hiyo wewe upo Chadema kukutetea ukristo wako.
 

Stahamala kitu gani....I am straight, I dont like double standard hapa.

Setikali hii ni serikali ya kikristo, so she claim.
Serikali ya CCM anayoipenda sana. Sasa analalamika nini na mambo ya udini usio na kichwa wala miguu.

Upuuzi tu umewajaa hawa wachumia tumbo wa ccm.
 
Soma hii bayana, hata siku moja mwizi huwa hakubali kama ameiba.
Amandla....
 
Hata sijaelewa unachojaribu kueleza hapo juu Mdau..
 
Mkuu mimi ni Mkristo Mkatoliki. Tumtofautishe Prof. Lipumba,Mwenyekiti wa CUF Taifa na Waziri ktk Serikali yetu ya JMT. Lukuvi amefanya makosa makubwa,kama ingekua nchi nyingine ameisha jiuzulu!

Mkuu,

Nimekusoma vizuri mno!

Naliwahi kunena hayo ulozungumzia hapo kiduchu mara kadhaa humuhumu-JF!

Yaani tatizo jangine lililopo hapo nchini na hata baadhi ya hizi the so called developing world countries/third world countries...hakuna strong democratic institutions and/or more responsible civil service structure/mechanism, ili kusimamia hizi kanuni na maadili ya viongozi/wanasiasa,khasa wa ngazi za juu!? Daah!

Hapa sikusudii asilan ati yakua zile Western world capitals viongozi/wanasiasa wake ni perfect na hawafanzi makosa,hasha!...lakini ukitazama kwa makini utaona ile degree za huo uchafu/unyama ni tafauti kubwa mno na kwenye hizi nchi zetu takriban zoote!?

Labda nasi tuwape hawa viongozi/wanasiasa wetu myaka mingine japo mia mbili-200...ndipo gradually wafikie hivi viwango vya uadilifu na kufuata kwa umakini hizi kanuni za madaraka/uongozi!? Daah! Teeh! Teeh! Teeh!

Ahsanta.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…