Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.

Lukuvi alikuwa anatekeleza na kutenda kulingana na matakwa ya mwajiri ambaye ni mteule wake pia.
 
Kila cku hapa unatetea dhulma na uonevu wa serikali ya ccm ila leo kwa vile kagusa dini yako ndo unang'aka hapa. Itendee dini yako haki kwa kupinga udhalimu wa CCM kwa wananchi na wapinzani pia.
 
Je ingekuwa anaongea msikitini angekuwa na ujasiri huo?
Lipumba naye aliwahi kuongea maneno ya uchochezi wa kidini msikitini. Wasiopenda udini walihamaki japo wapo waislaam waliona poa tu. Nyerere alisema wanasiasa muflisi wanakimbilia udini, ...Ndio hawa sasa tunawaona.
 
william Lukuvi ameendelezea tu pale alipoishia JK. Kama ni kumlaumu peke yake mtakuwa mmemuonea tu.
 
Ndiyo maana nnamuomba Kikwete amstaafishe huyu kabla madhara hayajawa makubwa, Waislaam watajibu na Wakristo watajibu, itakuwa mtafuruku mkubwa kama hatua za haraka hazijachukuliwa za kumuondoa huyu William Lukuvi kwenye duru za siasa.

Kila siku unalalama humu kwamba serikali ya mfumo kristo .................... sasa unataka Kikwete afanye nini?? Mwacheni Lukuvi apiganie mfumo wa CCM unless mnataka kuubadilisha!!??
 

Hao wanaoongea bungeni sina tatizo nao, wakiwa huko wana kinga na wanaweza kujibiwa na wengine, tatizo langu huyu aliyeenda kuongea Kanisani kwa uchochezi kabisa kuhusu Waislaam wa Zanzibar kuwa wakiachiwa watakuwa nchi ya Kiislaam na wataruhusu Bara ishambuliwe, hivi huku bara hakuna Waislaam?.
 
Kila siku unalalama humu kwamba serikali ya mfumo kristo .................... sasa unataka Kikwete afanye nini?? Mwacheni Lukuvi apiganie mfumo wa CCM unless mnataka kuubadilisha!!??

Hayo ni mawazo yako na una uhuru ka hayo, mawazo yangu ni kama ilivyo post #1 .
 
william Lukuvi ameendelezea tu pale alipoishia JK. Kama ni kumlaumu peke yake mtakuwa mmemuonea tu.

Sikumuona wala kumsikia Jakaya Mrisho Kikwete akiwagawa Waislaam na Wakristo, jee, wewe umemsikia? Kama jibu ni 'ndio" tunaomba ushahidi. Mimi sikumshutumu William Lukuvi mpaka nilipopata ushahidi na nimeuweka hapo kwenye post #1 .
 
FaizaFoxy Jk akifuata huu ushauri nahamia,ccm siku hiohio
 
Last edited by a moderator:
Kila la kheri, iwapo unaamini kuwa atawajibishwa na yeyote yule. Ukweli ni kuwa huyu jamaa hatawajibishwa wala nini. Anachokifanya ni kama ametumwa vile. Sana sana ataambiwa "huu ni upepo tu, utapita". Yangu macho na masikio.
 
FF hoja yako ni ya msingi kabisa na kama huyo uliyemwandikia angekuwa makini basi alipaswa kumng'oa siku ile alipokuja Bungeni eti anatetea hoja aliyotoa kanisani.
Tatizo ni moja tuu, CCM imeoza na mbaya zaidi kila kiongozi anamjua mwenzie kaoza sehemu gani hivyo ukimwajibisha mtu basi kinatokea kile kiitwacho "umemwaga mboga mie namwaga ugali"
Mwisho wa yoteni kuogopana na ndio maana hata ufanye nini ndani ya CCM neno kuwajibika halipo.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Usijifanye una busara kuandika hapa wewe!! si wewe uliyemtukana hapahapa JF Mzee Warioba kwamba aende zake akavute tumbaku? Sio wewe FOX au unataka tuilete thread yako hapa. Kumtukana mzee Warioba kunaondoa mantiki yote ya thread yako hapa, na kinachobaki ni ulevi tu wa Dini za kigeni. Sasa unajifanya hutaki uchochezi wa kidini, mjinga wewe utamdanganya nani? Ni kweli alichosema LUKUVI sio sahihi lakini na wewe ondoa kwanza Boriti jichoni mwako ndipo uone Kibanzi kwa mwenzio. Wapo wadau wametamka wazi Bungeni kuwa serikali tatu zitawaleta Alqaeda Zanzibar unasemaje kuhusu hilo? Kumbuka Lukuvi alikuwa anamwakilisha J.K!!!!
 
Lukuvi alikuwa anatekeleza na kutenda kulingana na matakwa ya mwajiri ambaye ni mteule wake pia.

Waajiri wake ni wananchi, huyo ni Mbunge wa Isimani. Aliyemteua uwaziri ni Kikwete na ndiyo maana nimemuandikia Kikwete, unayoyaona kwenye post #1 nimeyatuma na kwenye email ya Ikulu.
 

Ikiwa Sheikh huyo ni waziri kwenye Serikali basi ningekuwa wa kwanza kumwambia huo ni uchochezi na ningeomuomba Rais amwachishwe kazi kama nnavyofanya hapa kwa William Lukuvi. Mfano hai ni pale nilipomuona Sheikh Jongo bmk akijidai kulia kiuongo-uongo bungeni, nikaaandika humu humu JF kuwa huyo ni mnafik tu hana lolote.

Kumbuka hapa tunaongelea waziri ambae ni kiongozi wa serikali isiyo na dini na si sheikh au padri.
 
Lipumba naye aliwahi kuongea maneno ya uchochezi wa kidini msikitini. Wasiopenda udini walihamaki japo wapo waislaam waliona poa tu. Nyerere alisema wanasiasa muflisi wanakimbilia udini, ...Ndio hawa sasa tunawaona.

Huyu FaizaFoxy alikuwa anamtetea Lipumba alipompigia Kikwete kampeni za Udini Misikitini halafu leo anamkana Lukuvi kwa kuhubiri Udini huohuo.
Siungi Mkono hoja ya kumfukuza Lukuvi kwa Sababu imetolewa na Mdini na anataka Lukuvi afukuzwe kwa sababu sio Mwislamu mwenzake na sio kwa sababu hapendi udini.
 

Tafadhali weka ushahidi wa hayo usameyo. mimi nimeweka ushahidi kwa aliyoyasema William Lukuvi.

Jee, huko msikitini Lipumba aliwataja Wakristo? au alisema ana hofu na Wakristo? fikiri!

Kikwete Cabinet yake Waislaam ni wachache kuliko Wakristo, kwanini sijata mwingine yeyote awachishwe kazi na nimem-single out William Lukuvi? sababu ni hiyo nimeiweka kwenye post #1 , msikilize mwenyewe, wacha porojo.

Alilolifa ya William Lukuvi kama wewe unaliona ni jema kuna wengi wanaliona si jema, pitia posts za hii nyuzi na nyuzi zinginezo humu humu JF ujionee.
 

Kumwambia Mzee Warioba aende akapige tumbaku, hilo si tusi huo ni ukweli, yeye ni mpiga fegi kama alivyokuwa Nyerere. Tusi liko wapi hapo.

Yes, nilimwambia hivyo na nilisema kishamaliza kazi yake aliyotumwa, kisha iwasilisha bungeni sasa aende akatafute ulaji mwingine akapige na tumbaku zake. Hiyo ni fact. Ulitaka aendelee na kazi ambayo si yake?

Hapa naongelea William Lukuvi na fitna aliyokwenda kuipandikiza Kanisa kwa Wakristo dhidi ya Waislaam na nnasema hilo si jambo jema, Jee, wewe unaliona ni jema?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…