Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini lukuvi kaongea ukweli makanisa wamechoma moto mapadri wameuwawa.na mengine mengi
Lakini lukuvi kaongea ukweli makanisa wamechoma moto mapadri wameuwawa.na mengine mengi
mkuki kwa nguruwe! lukuvi kaongea nje ya kofia ya uongozi, ni haki yake. kutokuwa na imani na waislam ni kosa zaidi kuliko la sheikh ponda kuhamasisha wapagani, wakristo na wasioamini wauwawe?..RIDICULOUS!
Nnachompendea @FaizaFox ni kuwa anaipenda dini yake kuliko chama chake...waIslamu wote wangekuwa kama yeye, tungekuwa UKAWA tunashangilia ushindi saa hizi!
Mheshimiwa Rais Kikwete,
Kwa heshima na taadhima na mapenzi ya hali ya juu niliyonayo katika uongozi wako, siyo siri, ni dhahiri shahiri na kila mwana JF anaweza kuwa shahidi yangu kwa hilo.
Kikwete, nnaamini wewe ni mchapa kazi, nnaamini wewe una muono mpana na mrefu, nnaamini wewe unatimiza wajibu wako kwa kadri ya uwezo wako aliokujaalia Mwenyeezi Mungu.
Nakuomba yasikilize maneno ya William Lukuvi kwa umakini na ujifikirie, huyu William Lukuvi anaitakia mema Tanzania hii?
William Lukuvi amma kwa ujinga wake amma kwa werevu wake, ameutia dosari kubwa utawala wako. Ameenda Kanisani kuwaeleza Wakristo wenzake, tena kwa kujigamba na kejeli na kuonesha kibri ya hali ya juu, kuwa hana imani na Waislaam. Kumbuka iwe Muislaam wa Zanzibar au wa Tanganyika au kokote duniani, Waislaam ni kama kiwiliwili kimoja, unapokiumiza kidole kimoja basi mwili wote unasikia uchungu na unapatwa na maumivu.
William Lukuvi, yuko kwenye Serikali ambayo haina dini! lakini yeye mwenyewe ana dini na alienda kuongea kwenye nyumba ya dini na huko ndipo alipowaudhi Waislaam.
Hiyo ni dosari kubwa sana katika utawala wako. Tunakuomba muachishe kazi haraka sana William Lukuvi kabla hajazua balaa lingine, maana hata alipowahi kwenda kujitetea bungeni alionesha kibri zaidi ya kile alichoonesha Kanisani na akatamba na kuwachiwa muda na Mwenyekiti (mkristo pia) zaidi ya mbunge mwingi yeyote aliyechangia mijadala kwenye bunge maalum, ili ajitetee. Nilifikiri kuwa William Lukuvi ataomba radhi lakini cha kustaajabisha hajaomba radhi na karudia tena na tena na tena kuwa ana hofu na alichokieleza kanisani ni hofu yake na hakuna anaeweza kuhoji hilo.
Sisi tumemuelewa na hatumuhoji yeye, tunakuhoji wewe Rais wetu, jee, kiongozi wako ametugawa au ametuunganisha Watanzania kwa kauli zake hizo?
Jibu lako, mimi silijuwi, lakini jibu letu, ni wazi kabisa kuwa William Lukuvi katugawa Watanzania badala ya kutuunganisha, na si kuwa katugawa Watanganyika na Wazanzibari, la hasha, katugawa Waislaam na Wakristo. Na hilo ni hatari kubwa sana kwa Taifa letu.
Tunakuomba chukuwa hatua za haraka sana, umstaafishe huyu Waziri wako kabla hii athari na mpasuko alotuwekea kuzidi zaidi ya hapa alipotufikisha.
Msikilize:
[video=youtube_share;5gvZyIJkTFY]http://youtu.be/5gvZyIJkTFY[/video]
Nnamalizia kwa kutoa shukrani zangu ikiwa utapata wasaa wa kuyaona haya niliyokueleza.
Hao wanaoongea bungeni sina tatizo nao, wakiwa huko wana kinga na wanaweza kujibiwa na wengine, tatizo langu huyu aliyeenda kuongea Kanisani kwa uchochezi kabisa kuhusu Waislaam wa Zanzibar kuwa wakiachiwa watakuwa nchi ya Kiislaam na wataruhusu Bara ishambuliwe, hivi huku bara hakuna Waislaam?.
Hibi hstsri hii ya kugawanywa kwa waislamu na wakristo mmeanza kuiona wakati huu baada ya hotuba ya Lukuvi. Tuache unafiki, wakati ule mihadhara ya Uamusho wakihamsisha Makafir toka bara warudi kwao Zanzibar ni ya Waislam mlikuwa vipofu na viziwi? Hamkuona kabisa bar zikichomwa moto, maduka yakishambuliwa, makinisa yakichomwa. Kama mliona mbona nguvu hizi zi kulaani sikuzisikia. Waliohusisha Uamusho (Taasisi ya Kiislam) na CUF sio Lukuvi ni Wazanzibari wenyewe ktk mivutano yao ya kisiasa baada ya kibsini ukweli na kuchoka siasa za vurugu ZNZ.
Mara tumesahau vurugu za Mwembechai na maduka ya Kitimoto. Yawezekana huko ni mbali sana, mauaji ya karibuni ya kushindania nani achinje nani asichinje tumesahau. Sikuona watu kuja humu JF wakitoa tahadhari na wakiwakemea viongozi wa dini kwa kiwagawa watu ila Lukuvi sababu ni mwanasiasa wa Chama msichokipenda. Tunapopata nafasi tahadhariya nia mbaya za baafhi yetu lazima itolewe haijarishi ni popote pale. Ukizingatia ile ilikuwa ni hadhara sio mkutsno wa siri
laki tano yako kanunue baruti.
hivi kisasi alichokuwa anakiongelea hapa chini ni kisasi gani vile?
"Makafiri wanatakiwa kuyaheshimu mambo matakatifu ya Kiislamu na kuyajua, kama hawataheshimu Mwenyezi Mungu alisema lazima mlipize kisasi katika mambo matakatifu. Mungu alisema ni lazima mlipize kisasi mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Mambo matakatifu yamewekewa kisasi"
Lv u my cster
lipumba alisema haya mbona hajakanusha mpka Leo kuwa mkulu alikua anapita miskitini nakuaidi mambo mengi kwa waislam faiza hayo yote uyaoni unaona ya lukuvi tu ilifikia muislam akapelekwa ubalozi vatican angalie hali ya wakristo lkn ndo hivoKama ni uchochezi mbona hata mkulu naye nimchochezi unafikiri atawezaje kumwajibisha mchochezi mwenzie