Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mheshimiwa Rais Kikwete,
Kwa heshima na taadhima na mapenzi ya hali ya juu niliyonayo katika uongozi wako, siyo siri, ni dhahiri shahiri na kila mwana JF anaweza kuwa shahidi yangu kwa hilo.
Kikwete, nnaamini wewe ni mchapa kazi, nnaamini wewe una muono mpana na mrefu, nnaamini wewe unatimiza wajibu wako kwa kadri ya uwezo wako aliokujaalia Mwenyeezi Mungu.
Nakuomba yasikilize maneno ya William Lukuvi kwa umakini na ujifikirie, huyu William Lukuvi anaitakia mema Tanzania hii?
William Lukuvi amma kwa ujinga wake amma kwa werevu wake, ameutia dosari kubwa utawala wako. Ameenda Kanisani kuwaeleza Wakristo wenzake, tena kwa kujigamba na kejeli na kuonesha kibri ya hali ya juu, kuwa hana imani na Waislaam. Kumbuka iwe Muislaam wa Zanzibar au wa Tanganyika au kokote duniani, Waislaam ni kama kiwiliwili kimoja, unapokiumiza kidole kimoja basi mwili wote unasikia uchungu na unapatwa na maumivu.
William Lukuvi, yuko kwenye Serikali ambayo haina dini! lakini yeye mwenyewe ana dini na alienda kuongea kwenye nyumba ya dini na huko ndipo alipowaudhi Waislaam.
Hiyo ni dosari kubwa sana katika utawala wako. Tunakuomba muachishe kazi haraka sana William Lukuvi kabla hajazua balaa lingine, maana hata alipowahi kwenda kujitetea bungeni alionesha kibri zaidi ya kile alichoonesha Kanisani na akatamba na kuwachiwa muda na Mwenyekiti (mkristo pia) zaidi ya mbunge mwingi yeyote aliyechangia mijadala kwenye bunge maalum, ili ajitetee. Nilifikiri kuwa William Lukuvi ataomba radhi lakini cha kustaajabisha hajaomba radhi na karudia tena na tena na tena kuwa ana hofu na alichokieleza kanisani ni hofu yake na hakuna anaeweza kuhoji hilo.
Sisi tumemuelewa na hatumuhoji yeye, tunakuhoji wewe Rais wetu, jee, kiongozi wako ametugawa au ametuunganisha Watanzania kwa kauli zake hizo?
Jibu lako, mimi silijuwi, lakini jibu letu, ni wazi kabisa kuwa William Lukuvi katugawa Watanzania badala ya kutuunganisha, na si kuwa katugawa Watanganyika na Wazanzibari, la hasha, katugawa Waislaam na Wakristo. Na hilo ni hatari kubwa sana kwa Taifa letu.
Tunakuomba chukuwa hatua za haraka sana, umstaafishe huyu Waziri wako kabla hii athari na mpasuko alotuwekea kuzidi zaidi ya hapa alipotufikisha.
Msikilize:
[video=youtube_share;5gvZyIJkTFY]http://youtu.be/5gvZyIJkTFY[/video]
Nnamalizia kwa kutoa shukrani zangu ikiwa utapata wasaa wa kuyaona haya niliyokueleza.
Hujazisoma vizuri, umekurupuka.
Faizafoxy: Self qualification is no qualifiction. Wacha watu wakusifu. Ukiona baba mwenye nyumba anajitapa mbele ya wanawe kuwa yeye ndiye baba wa nyumba ujue pana walakini. Baba mwenye nyumba hujulikana hata bila ya kujipigia upatu, tena kwa watoto wake.
Sheikh wa Bakwata, Jongo alijidai kulia kiunafik BMK, na hapa anapewa za uso: https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/650463-sheikh-jongo-bado-ana-mengi-ya-kujifunza.html
Faizafoxy: Self qualification is no qualifiction. Wacha watu wakusifu. Ukiona baba mwenye nyumba anajitapa mbele ya wanawe kuwa yeye ndiye baba wa nyumba ujue pana walakini. Baba mwenye nyumba hujulikana hata bila ya kujipigia upatu, tena kwa watoto wake.
Mbona hapa hakuna hoja kwa kweli; watawala hawajaona kosa lolote la Lukuvi.
Hoja utaiona wapi? maco unayo lakini hayaoi, masikio unayo lakini hayasikii.
Sitegemei mtu kama wewe kuiona hoja katika hili.
Lakini kumbuka, nyuzi hii imesambazwa kwenye mablogu mtandaoni kwa walioiona hoja.
Mbona hapa hakuna hoja kwa kweli; watawala hawajaona kosa lolote la Lukuvi.
Upo sensitive na topic za udini utadhani crawler za NSA zimeona keywords za magaidi wenzio:heh::heh:. I can't waste my time analyzing kitu kimeandikwa na Faiza Foxy. Na mtu yeyote anayetaka kuanza sober discussion na Faiza Foxy anapoteza tu muda. Faiza Foxy hayuko sober amelewa udini

Una dhihaka mbaya sana wewe na Mh. rais!Mheshimiwa Rais Kikwete,