Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Status
Not open for further replies.
Ndio marafiki viongozi wa Kikwete hao, nchi inaongozwa kwa hisia. Rasimu ipo, imejieleza, imejifafanua, jamaa haisomi ana ongea mamno ya kufikirika. Halafu Sitta nae kakwama kwenye matope anampa nafasi Lukuvi kujieleza bungeni bila walio mtuhumu kuwepe, ati mwanasheria. Ukiyashangaa ya Makinda utayaona ya Sitta na ccm.
 
Kwenye Ukristo hakuna dhambi mbaya kama hofu na wogo, ndiyo maama bible insema tumeumbwa kwa Roho ya ujasiri. Hiyo ratiba inakuhusu wewe maana Lipumba atazindua album ya Lipumba.

Teh teh teh!

Eti tumeumbwa kwa ujasiri....ujasiri gani huo unashindwa kulisimamia unalosema. Umebaki sasa kugeuza maneno mara ratiba inakuhusu wewe teh teh teh!

Mnasema mnaenda kuzindua album ya lukuvi Makanisani mara tena sio Lukuvi imekua Lipumba teh teh teh!

We mpakwa mafuta umepatwa na nini?

Na bado mtaendelea kuumbuka kila kanisa mtakalo kwenda kuhubiri hofu yenu dhidi ya Uislam!
 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amekiri kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ya uchochezi kanisani kwa madai ya kuingiwa hofu na harakati za asasi ya kidini ya Uamsho, kufanana na za Chama cha Wananchi (CUF) za kudai Serikali ya mkataba. Waziri Lukuvi alitoa kauli hiyo jana bungeni, akitoa ufafanuzi wa kauli aliyopata kuitoa katika Kanisa la Methodist wakati wa kumsimika Askofu Mteule, Joseph Bundara. Katika misa hiyo, Lukuvi aliwaambia waumini wa kanisa hilo kwamba muundo wa serikali tatu utavunja Muungano na ikipitishwa, jeshi litaingilia kati kuongoza nchi, kauli ambayo juzi ilisababisha UKAWA wasusie Bunge. Katika ufafanuzi wake jana bungeni Lukuvi alikiri kutoa kauli hiyo kanisani kwa madai ya kuingiwa hofu ya kutokea ubaguzi wa kidini. Alisisitiza kuwa hofu yake inatokana na harakati zinazofanywa na kikundi cha Uamsho visiwani Zanzibar, kufanana na za CUF ambazo ni kudai Serikali ya Mkataba. Alisema uamsho imekuwa ikihusishwa na vurugu zinazotokea mara kwa mara visiwani humo, zinazohusishwa na vuguvugu la kudai mamlaka kamili ya Zanzibar. Akitolea mfano, Lukuvi alisema Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, alipotumwa Zanzibar kupeleka Rasimu ya Katiba, rasimu hiyo ilichukuliwa na wanauamsho na kuichanachana, kisha kuisigina mbele yake. “Sasa niwaulize humu ndani…Uamusho ni nani…?” Wajumbe kwa wingi wao na vigelegele wakajibu “Ni CUF”. Akauliza mara ya pili: “Uamusho ni nani…?” akajibiwa: “ CUFUUUUU”. “Lakini kuna swali liliulizwa hapa bungeni, CUF wakaja juu wakasema ni Taasisi ya Kidini…sasa unaniambiaje mimi nisiwe na hofu ya kidini wakati kuna chama cha siasa kinahusiana na Uamsho lakini ina ladha ya kidini. “Na kwa kuwadhihirishia hivyo, kila mara CUF na Uamsho utakapomtaja Mwalimu Nyerere na kumtaja Karume wanakwambia alaaniwe.. lakini hizi ndiyo sera za hao mnaowasema, sasa tunakuwaje na chama cha siasa ambacho tayari kinajipanga kutawala Zanzibar, lakini kinaendeshwa na Sera za Uamsho…uamsho wenyewe wanasema ni Taasisi ya Kidini, kwa nini usiwe na wasiwasi na mihemko yote ile ya Uamsho mpaka na Bara tukatikishika, kwa nini tusiwe na wasiwasi kwamba CUF ikichukua nchi basi Uamsho ndiyo utatawala, kwa nini tusiwe na hofu, yametokea na sisi tumeyaona, kwa nini wanajificha kwenye kivuli cha dini ili kufanya siasa…na kwa nini dini imetumika vizuri sana kueneza sera za CUF za serikali tatu, na kila wachosema CUF ndicho wanachosema uamsho?,” alihoji Lukuvi. “Na ukishaona chama kinajitayarisha kuchukua madaraka kama ilivyo kwa CUF, kinatumia taasisi hii yenye msimamo mkalii kueneza sera zake ni hatari kwa mustakabali wetu, ni hatari kubwa,” alisema. Alisema kama kweli Uamsho ni taasisi ya kidini na inatekeleza sera ambazo zinatekelezwa na vyama vya siasa, lazima Watanzania wajiulize kuna nini. Alisema kuna tishio la baadhi ya watu ambao wameanza kufikiria kwamba Wazanzibar wanafaidi sana wakiwa Tanzania Bara na kufikiria kuwafukuza na kunyang’anya mali zao na iwapo watafanikiwa kuwanyang’anya watawafukuza. “Sasa baada ya Wazanzibari kuondoka, tutaanza kuangalia hawa Wachina, hawa Wahindi na vinginevyo tutakuja hata kwenye dini, Wakristo wana mali zaidi kuliko Waislamu. “Lakini kwa Zanzibar ambayo ina dini kubwa moja na tunajua hizi dini, kwa mfano katika dini ya Ukristo kuna dini ndogo ndogo nyingi na ndani ya ukristo kuna watu wenye siasa kali lakini na ndani ya Uislamu kuna watu wenye siasa kali kwa hiyo mimi nina hofu nyingine ya ubaguzi . “Nasema kunaweza kukatokea ubaguzi wa kidini, inaweza ikatokea ubaguzi wa kieneo kwani inaweza kutokea hata Unguja akaenda mtu akasema Waunguja wote ondokeni hapa pamejaa, sasa hizi ni hofu zangu, mfumo huu wa serikali mbili umetuondolea hofu hizi hatuna hofu kabisa ya maisha haya, leo hatumfikirii Mpemba atoke au Muunguja atoke, Msukuma atoke, hatufikirii,” alisema. Awali kabla ya Lukuvi kutoa ufafanuzi huo, Sitta aliwaambia wabunge kuwa amemlazimisha Lukuvi kukatiza safari yake nchini India ili atoe ufafanuzi wa kauli alizozitoa katika Kanisa la Methodist. Alisema amelazimika kumwita Lukuvi ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka nchini jana kwenda India kwa matibabu ili atoe ufafanuzi wa kauli yake ambayo juzi ilisababisha UKAWA, wanaounga mkono serikali tatu, kususia Bunge hilo. Moto wa wajumbe wa UKAWA, kutoka bungeni juzi uliwashwa na Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alisema serikali na mawaziri wake wameanza kampeni ya kupinga muundo wa serikali tatu unaopendekezwa na rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Alisema hoja ya Lukuvi inafanana na ile ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge, Machi 21, mwaka huu. Tanzania Kwanza wamruka Lukuvi Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaojiita Tanzania Kwanza, wamemruka Mjumbe wa Bunge hilo, William Lukuvi, kuwa kauli aliyoitoa kanisani na kusababisha mtafaruku ndani ya bunge ni maoni yake binafsi na si maoni ya serikali ya CCM. Akitoa ufafanuzi jana, Kiongozi wa kundi hilo, Adam Malima, alisema Lukuvi kama mjumbe ana uhuru wa kutoa maoni yake na kwamba aliyoyasema ni yake na wala si ya chama wala serikali. Kuhusu kauli za matusi, Malima alisema haoni kama kuna matusi na kuongeza kuwa tusi kubwa ni lile alilolitoa Profesa Lipumba kwamba wote wanaodai serikali mbili ni Interahamwe. CHANZO: TANZANIA DAIMA 18.04.2014

Duuh, mawazo mazuri but uandishi wako ni hatari sana, jaribu kuweka paragraphs coz nimeshindwa kuelewa pia inachosha kusoma
 
Bora kukata viuno umesimama kuliko kukata viuno umekalia Jamvi kama wafanyavyo watukufu.

Sisi hatukati viuno kijana....Mimi nitakuwekea ushahidi hapa wa jinsi mnavyoimba na kukata viuno mkiwa kanisani ili uone kula nachokisema hapa na ushahidi nacho.

Nyie wapakwa mafuta ni mabingwa wa kuzua!
 
Haka katabia ka kuimba na kukata viuno kanisani, kamewaathiri sana ubongo wenu mpaka kwenye maisha ya kawaida!

Au umeshapata mvinyo hapo kanisani sasa unachanganya mada?!

Haya narejea tena suali halafu unijibu. Je na wewe una hofu kama mpakwa mafuta mwenzio Lukuvi?

Matusi ya nini? Mbona sisi hatuwasemi mnayoyatenda misikitini? Maneno haya kayasema muislamu mwenzako. Muulize yeye ndie atakupa jibu. Au unamuogopa?

Amandla......
 
Sasa ni dhahiri kwamba kumbe hata CCM inaendeshwa kwa sera za Kikatoliki, maana msimamo wa Kardinali Pengo ndio msimamo wa CCM, Sasa utaniaminishaje kwamba CCM sio mshirika wa Wakatoliki,

Hata majuzi tumemwona Mwenyekiti wa Bunge akiwatemebelea Kardinaru Pengo na akageresha Kumwona Mufti Simba lakini hiyo ilikuwa danganya toto. CCM Udini mliouasisi ugtawamaliza ninyi wenyewe, kwa sasa tunao uelewa mkubwa kuliko mlivyodhani.
 
Teh teh teh!

Eti tumeumbwa kwa ujasiri....ujasiri gani huo unashindwa kulisimamia unalosema. Umebaki sasa kugeuza maneno mara ratiba inakuhusu wewe teh teh teh!

Mnasema mnaenda kuzindua album ya lukuvi Makanisani mara tena sio Lukuvi imekua Lipumba teh teh teh!

We mpakwa mafuta umepatwa na nini?

Na bado mtaendelea kuumbuka kila kanisa mtakalo kwenda kuhubiri hofu yenu dhidi ya Uislam!

Inaonekana unasoma kama umepakatwa, nimekwambia tukutane Mchambawima Zanzibar Lipumba anazindua album ya Lukuvi. Again siwezi kuwaogopa Wafilisti maana ni viumbe wadogo sana kwangu, na hilo wanalijua.
 
Sisi hatukati viuno kijana....Mimi nitakuwekea ushahidi hapa wa jinsi mnavyoimba na kukata viuno mkiwa kanisani ili uone kula nachokisema hapa na ushahidi nacho.

Nyie wapakwa mafuta ni mabingwa wa kuzua!

Mnafanya nini mkiswali? Msipende kutusi wanavyoabudu wenzio.

Amandla.......
 
Matusi ya nini? Mbona sisi hatuwasemi mnayoyatenda misikitini? Maneno haya kayasema muislamu mwenzako. Muulize yeye ndie atakupa jibu. Au unamuogopa?

Amandla......

Mimi sijamtukana mtu labda kama ukweli umekua matusi siku hizi?!
 
Sisi hatukati viuno kijana....Mimi nitakuwekea ushahidi hapa wa jinsi mnavyoimba na kukata viuno mkiwa kanisani ili uone kula nachokisema hapa na ushahidi nacho.

Nyie wapakwa mafuta ni mabingwa wa kuzua!

Niliwahi kumuuliza Mfilisti mmoja kuhusu ukataji viuno kwenye jamvi, akaniambia ukataji viuno kwenye jamvi kuna raha yake hasa kwa women.
 
Serikali ya CCM haina maslahi kwa Watanzania, wewe pia unalijua hilo ingawa kila kukicha unaipigania hapa lakini zikija issues ndiyo unanza kuja na haya ya serikali Kristo blah blah blah. With CCM Tanzania haitafika popote ........... ni siasa tu hakuna maendeleo zaidi ya propaganda. Juzi juzi tu watu walikuwa wanauponda walaka wa Lema wakati una ukweli ndani yake. Udini unanuka Bongo noma na chanzo ni CCM!!

Ukweli ni huu,Serekali ya CCM tumeiweka sisi wananchi wapenzi wa CCM tulio wengi nchini.ukiona viongozi wa ccm ni wengi bungeni ujue wanatuwakilisha sisi tulio wengi.wakitoka humo mjengoni watakuja kwetu.tupo pamoja nao. Wananchi hawatachotwa mawazo yao kwa ngonjera hii na ile.
 
....lukuvi anauliza bungeni "uamsho ni naniii?".....watu wanajibu kwa ujumla wao (wakiwemo mawaziri wa utawala huu)..eti "uamsho ni CUFUUUU"......hivi kweli hapa ndipo nchi hii ilipofikia!!!....kwamba leo chama cha kisiasa TZ kinaitwa taasisi ya dini!!!kweli??......huu udini unaoenezwa na watawala wa taifa hili ni sawa kweli???watu wanaona hili ni sawa??....hii nchi hii imefikia hapa na watu wanaona sawa bungeni??..alafu wakiambiwa wanalalamikaje??
 
Inaonekana unasoma kama umepakatwa, nimekwambia tukutane Mchambawima Zanzibar Lipumba anazindua album ya Lukuvi. Again siwezi kuwaogopa Wafilisti maana ni viumbe wadogo sana kwangu, na hilo wanalijua.

Wewe teyari ushakua muongo...na hilo linadhihiri kwenye mabandiko yako....Ukiwa muongo husiwe mwenye kusahau!

Rejea kile ulichoandika utajua wewe ni Mnafiki na nimwenye kuzua uongo!
 
Hiyo phobia ya nini? Uislaam wa Zanzibar unamuhusu nini Lukuvi? hata awe na hofu? Nchi yenye Waislaam 99% wakiamua kuwa nchi ya Kiislaam ni kosa? mlitaka waseme wao hawana dini?

Hizo takwimu umzibuni kwa ujanja gani.tupatie mganyo wa dini nyingine na wasio na dini hapo zanzibar.hata ingekuwa hivyo unataka kusema wasio wa dini yako watalazimishwa kufuata sheria za imani yako.au una maana watanganyika wote wakija huko watatumikia sheria za dini moja?wewe unaona hii ni sawa kwa imani yako ya haki!
 
Wewe teyari ushakua muongo...na hilo linadhihiri kwenye mabandiko yako....Ukiwa muongo husiwe mwenye kusahau!

Rejea kile ulichoandika utajua wewe ni Mnafiki na nimwenye kuzua uongo!

Ufafanue uongo wangu, wewe ndiyo mzito wa kuelewa.
 
Nadhani haumfahamu Ritz vizuri mimi sishikiwi akili na viongozi wa siasa kama nyie mnavyoshukiwa akili na Mbowe na Dr.Slaa, mimi naangalia dini yangu kwanza, wewe mbona hautaki kufuata tamko la Pengo anataka serikali mbili. mimi ni Mtanganyika nataka huu muungano uvunjike tuwakabidhi Zanzabar nchi yao halafu tupambane sisi kwa sisi huku Tanganyika, nyie wakirsto si mnafundishwa makinisani kwenu kuwa mchague serikali mbili, tusubiri tuone.
Ritz hakuna mwanamageuzi anayeshikiliwa akili na viongozi wa siasa isipokuwa wa-ccm, hivi hujiulizi kwenye bunge hili wale G55 wamepotelea wapi! Hujiulizi wajumbe wa baraza la wawakilishili wameshikwa na nini ndani ya bunge la katiba hata dhamira waliyoingia nayo pale imetoweka! Kwakifupi ni mfumo ccm sio mfumo kristo wala nini, zimwi hapa ni ccm, likona kete ni uislamu linaicheza, likiona sasa ni ukristo linaicheza kiasi kwamba wewe na mimi tunajikuta tukilumbana japo nia ya ukombozi ni moja.
 
Matusi ya nini? Mbona sisi hatuwasemi mnayoyatenda misikitini? Maneno haya kayasema muislamu mwenzako. Muulize yeye ndie atakupa jibu. Au unamuogopa?

Amandla......
Unaonekana una hofu sana na Uislam aka "Islamophobia"
 
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa
wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

[video=youtube_share;PIAPAAd3Dck]http://youtu.be/PIAPAAd3Dck[/video]

cc Ritz, gombesugu, kahtaan, THE BIG SHOW, CHAMVIGA
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.


Japokuwa tunaishi katika siasa na wanasiasa lakini siasa siku zote ni mchezo mchafu. Ndiyo maana binafsi naungamkono hoja ya kurudishwa kwa serikali ya TANGANYIKA kwani hata wanaosema gharama itakuwa kubwa sioni logic yao kwani hata ndani ya serikali 2 zilizopo matumizi, ubadhirifu, ufisadi na wizi vimekithiri kiasi kwamba hata faida siioni, hivyo nibora TANGANYIKA yetu irudi ili matumizi yazidi ili na wao wakose za kukwapua.

Mambo ya udini sijui Ukristo, Uislamu hayo tuwaachie wenye fikra fupi kwani binafsi kila mtu regardless of his/her religion ni ndugu yangu kwani nimeishi hivyo kwa miaka mingi ambayo MUNGU ameniwezesha kuishi hadi sasa, jambo la msingi ni kuwa makini na wanasiasa....mimi kwa taaluma yangu huwa kuna msemo tunapenda kuutumia ktk shughuli zetu unaosema hivi. "......NEVER TRUST A BULL, ESPECIALLY A JERSEY BULL......"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom