Kinadharia:
Je, unataka kujijua wewe ni mtu wa aina gani? Haya nionyeshe rafiki zako nami ntakwambia tabia zako.
Kimahesabu:
Ikiwa "X" ni sawa na "Y",
Kisha "Y" ikawa sawa na "Z",
Kwa hiyo "X"nayo itakua sawa kabisa na "Z"
Kiuhalisia:
Mwenyekiti wa ccm, ambaye hatujui uwezo wake kiutendaji, aliteua watendaji wake wa serikali kwa kadri alivyoona wanafaa. Muda mfupi baadaye sisi wananchi tukaanza kushuhudia uovu ukifanywa na wateule hao. Kama mteule ametenda uovu na muovu hajakemewa wala kuonywa na mteule wake inabidi tujiongeze na kujitathmini upya (kama itawezekana).