Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

luku imeisha kwenye akili ya lukuvi maana ni pumbu.....------- maana hata mtoto mdogo anajua effects za 2 na 3 ndo mpango mzma.
 
Masikini Lukuvi na siasa zao za divide and rule. Wakienda misikitini wanaongea hiv wakirudi makanisani wanageuza maneno. Pa1 na yote hayo siungi mkono uamuzi wa kususa majadiliano kama ni matusi wote walikuwa wanayatoa.
 
Kinadharia:
Je, unataka kujijua wewe ni mtu wa aina gani? Haya nionyeshe rafiki zako nami ntakwambia tabia zako.

Kimahesabu:
Ikiwa "X" ni sawa na "Y",
Kisha "Y" ikawa sawa na "Z",
Kwa hiyo "X"nayo itakua sawa kabisa na "Z"

Kiuhalisia:
Mwenyekiti wa ccm, ambaye hatujui uwezo wake kiutendaji, aliteua watendaji wake wa serikali kwa kadri alivyoona wanafaa. Muda mfupi baadaye sisi wananchi tukaanza kushuhudia uovu ukifanywa na wateule hao. Kama mteule ametenda uovu na muovu hajakemewa wala kuonywa na mteule wake inabidi tujiongeze na kujitathmini upya (kama itawezekana).
 
Bora mjinga kuliko moumbavu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
..................very shameful Lukuvi, kamalizia na kupigania maslahi ya Lytonga Mrema kisa kabakia mjengoni.

Mrema analipa fadhila za kulipiwa matibabu ya kisukari na ukurutu unaomteketeza ..
 
UKIRISTO ULINGIA ZANZIBAR KABLA TA TANGANYKA. tangu wakati huo wakristo wapo zanzibar.
na kanisa la kwanza zanzibar ardhi walipewa na waislamu wa zanzibar.. huu ubaguzi unapandikizwa kusudi ili kupata uhalali wa kukandamiza kwa maslahi ya matumbo ya mafisadi.
 
Nyie machoko wa uchochezi hamkumwelewa Mh Lukuvi ila waliowengi wamemwelewa ipasavyo,haya nendeni mkawachochee watz waingie kwenye machafuko ya udini,ukabila na ubaguzi roho ziwatue
 
Ninamshangaa sana Mh Lukuvi kwa kauli zake za uchochezi ambazo amekuwa akizitoa mara kwa mara na kusababisha hofu na taharuki isiyokuwa na msingi wowote. Kauli yake ya ovyo na isiyokuwa na mashiko ni ile aliyoitoa kanisanai wakati alipoalikwa katika hafla ya kumsimika askofu wa kanisa la Methodist. Lukuvi amesikika laivu bila chenga akiwatisha wananchi kwamba ikiwa watazikubali serikali 3 kwenye kura ya maoni, basi wategemee jeshi kuchukua nchi! Kama ndivyo basi, sisi raia tunaoteseka chini ya utawala wa CCM tunalikaribisha jeshi lije litawale badala ya kuendelea kuishi ndani ya utumwa wa serikali ya CCM.

Na maneno haya Lukuvi ameyarudia tena alipohojiwa na waandishi wa habari kutaka atoe ufafanuzi zaidi (wakidhani labda mwanzo alinukuliwa vibaya) na ameendelea kutetea hoja yake hiyo. Alijitetea kwamba yeye sio mtu wa kwanza kutamka maneno hayo kwani yameishawahi kutamkwa na mkuu wa nchi wakati anazindua bunge la katiba. Huu ni utetezi wa kitoto na kijuha. Rais alitamka maneno hayo akiwa bungeni na ameyatamka akiwa kama amiri jeshi mkuu (Commander-in-chief of the armed forces). Haya sio maneno ya kutamkwa ndani ya kanisa wala mahali popote pale. Maneno haya yana ukakasi mkubwa mbele ya jamii na yanaweza kuisambaratisha nchi na hata kusababisha vita ya kimbari. Tukumbuke kwamba Intarahamwe walikuwa wakifanya uchochezi kama huu kupitia makanisani na matokeo yake kila mtu anayajua.

Lukuvi hakuishia hapo tu lakini pia aliwadanganya wananchi kwamba wazanzibar wanataka uhuru kamili ili waifanye nchi yao kuwa ya kiislamu. Huu ni uwongo, uzandiki na unafiki wa kupindukia! Wazanzibar wanashindwa nini kujibadilisha kuwa nchi ya kiislamu wakati nchi yao ina mamlaka kamili tangu 2010? Ama kweli Lukuvi ana akili ndogo kuliko mbegu ya haradali! Hivi anadhani kwamba watanzania wa leo ni mbumbumbu kama wale wa 1947?

Watanzania tuwe makini na viongozi wenye akili ndogo kama Lukuvi kwani watu kama hawa ndio walioitumbukiza nchi ya Rwanda kwenye mauaji ya kimbari kwa kauli za kichochezi na zinazowagawanya wananchi. Kauli hii ya Lukuvi imezidi kulipasua taifa hadi kupelekea bunge la katiba kukaribia kuvunjika. Kauli za namna hii sio za kufumbia macho hata kidogo kwani madhara yake ni makubwa sana katika mshikamano na mustakabali wa nchi yetu. Akili za kuambiwa, changanya na za kwako!

Mungu ibariki ZANZIBAR, Mungu ibariki TANGANYIKA. Amina.

‘Lukuvi anajenga hofu kwa wananchi’ - Kitaifa - mwananchi.co.tz
:yield:
 
Acheni kuweweseka, Ukweli ndio huo!

amesahau kusema chadema na cuf wameshirikiana na mzee warioba kutengeneza hii rasimu ili kutudhoofisha sisi magamba.dah chadema noma sana yaani wanatunyima sana usingizi,sijui kwanini hili lichama lilisajiliwa.mbaya zaidi ule mchongo wetu wa kumtumia nzito kabwela wameustukia sijui rangi gani tutaacha ona miaka hii.
 
Muda wa kutoa maoni ulishakwisha namshangaa sana Lukuvi. Tatizo CCM wana hofu wanajua watanzania tushachoka na usanii wao
 
Nimeanza kuunga mkono serikali mbili sasa...

Huwezi mpa kichaa akulindie watoto. Anaweza kuwachoma moto...

Though siipendi CCM but kwa hili nipo nao nitahakikisha napollute angalau watu 500 -1000 waniunge mkono. Na uhakika kati ya hao watavuta wengine wa kutosha..

Ugaidi sipendi kabisa.
 
nilikuwa nafikiri lukuvi ana kichwa juu ya shingo yake kumbe ni kifuu cha nazi. masikitiko makubwa kabisa.
 
Masikini Lukuvi na siasa zao za divide and rule. Wakienda misikitini wanaongea hiv wakirudi makanisani wanageuza maneno. Pa1 na yote hayo siungi mkono uamuzi wa kususa majadiliano kama ni matusi wote walikuwa wanayatoa.

Ulitaka waendelee na matusi
 
Back
Top Bottom