Lulu arudi chuo, anachukua telecommunication engineering

Lulu arudi chuo, anachukua telecommunication engineering

Telecommunication hii ninayoijua mimi au.. Nahama course mie. Maana saaa hii course itakuwa supu ya mbwa tena ya baridi
 
Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Telecommunication engineering.

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.

Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Telecommunication engineering,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.

Source ;Bongo 5
Duhh, hilo neno "NACHUKUA" ina maana keshafaulu na hakuna haja ya kutahiniwa
 
Labda ni jina la filamu yake mpya ulimi ukamteleza akasema anaenda kusomea badala ya kuandaa ni binadamu jamani tumuelewe tu.
 
amadeusha post: 16592455 said:
usije sababisha watu tukacheka kw nguvu sana serikali iingilie kati ikajua mnamkebehi apa [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Hahahahh..mkuu hawa Bongo movie wana masihara sana na taaluma za watu..
 
Kabisa! Hivi umeshapata kujiuliza alitumia Law ipi ya Issac Newton hadi kulipeleka chini jibaba kama Marehemu Kanumba?!
3rd Law mkuu 'to every action there is an equal and opposite reaction'. [emoji123] [emoji123] [emoji123]
 
Dakika hii tu umebadilisha kasema anasomea human resource sasa wewe unabadilisha kwa makusudi kabisa....!!
 
Msanii mahiri wa filamu Elizabeth Micheal ‘Lulu’ amerudi chuoni na kuamua kuchukua kozi ya Telecommunication engineering.

Muigizaji huyo ameweka wazi anachosomea baada ya mashabiki katika mtandao wa Periscope, kutaka kujua anasomea nini baada ya kupost video mbalimbali katika mtandao huyo huku akizungumzia maswala ya chuo.

“Jamani nimechoka kuulizwa nasomea nini, nasomea nini, nachukua Telecommunication engineering,” alisema Lulu.

Muigizaji huyo hakupenda kuweka wazi ni chuo gani anasoma, lakini aliweka wazi wiki hii naingia katika mitihani.

Lulu ni miongoni mwa wasanii wachache wa filamu walioamua kurudi darasani na kuongeza maarifa.

Source ;Bongo 5
Nimesoma hii habar sikuielewa hata kidogo lakin nilipojaribu kuangalia jina la mleta mada ndio nikaielewa uzue
 
Le mtindizzz kafiwa na mama yake mzazi(rip)... Ila huyu mzee kapinda hana uchungu kabisa as if there's nothing happened...
 
Hahaha... Sio kwa comments hizo. Mwacheni achukue hyo telecommunications yake.. Hahaha.. Ila hajasema kama ni foundation au masters
 
Lulu naye! Anadhani hatujui anasoma hapo Magogoni hicho chuo kinaandaa masekretari.. Na wako kwenye mitihani kuanzia wiki jana.

Siku hizi ukisoma MS Word na XL Unasoma Engineering???[emoji23] [emoji23]

Muhimu anasoma tatizo Ni nini?
 
Miongoni mwa wanafunzi maboya wa perfect vision huyu nae kwenye list alikuwemo,kutwa alikuwa anashinda kwenye vigenge vya chips na wadau nao walikuwa hawayumbi kumshesha humo no skul labda ushonaji kwa masista wa kijezuiti pale mbinga

Wacha dharau
 
Binti anapenda kujipaisha sana ilhal sio..Ukweli huyu alianza form one perfect vision pale nyuma ya ubungo plza,akashindikana alivofika form two.Darasan anaingia akijiskia,kila usiku ye yupo klabu na vichupi na analewa,mara mahakamani ana kesi za kutukana na kupigana kugombania visharobaro..hiyo shule wakamshindwa wakamfukuza..Akaenda kwenye hiyo shule na mzaz wake ndo wakamkubali,hiyo shule ya midway ni kama special centre tu,inapokea hao waloshindikana huko ndo mana matokeo mabaya hivo ni div 4 na zero tu.
Hata magogoni anachukua record management sio human resource management kama anavyojipaisha!..
 
Back
Top Bottom