Lulu: Sipendi "masharobaro"

Lulu: Sipendi "masharobaro"

Ndio hivyoo wanakua wametulia angalau japo sio wotee, ,
Maana kuna mwingine ana 50 years lakini akili zake ni miaka 18

Masharo uharo weng wana akil za usiku tu hakuna la maana wanalowaza.tehtehhh
 
Mtu mzima kashajenga ana watoto wanne wote wanafanya kazi mshahara wake ukiingia unakua hauna kazi zaidi ya starehe, useme nn usipewe.sasa sisi masharo kazi yenyewe kunyoa tumepenga kwa mama amina kodi 30 per month

Hahahaaaaa umenchekesha sana asee
 
Kuna categories za masharo, wanaojitambua na wasiojitambua.
Wanaojitambua hawaongi.
Wasiojitambua full kuhonga.
Sasa dada lulu hapa cjui alikua anawalenga wapi haswa.
Sijajiandaa kwa maswali twafadhali..
 
Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee , Elizabeth Michael ‘ Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii , Lulu alisema akiwa na mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.

“Masharobaro hawana nafasi kwangu , kwa sababu hawafikirii maisha kabisa , hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro ,” alisema Lulu .


Ninashida ya kupata namba yake plz mwenye namba yake aniPM.
 
Back
Top Bottom