Lumumba, Dar: Mzee Kinana na Mzee Makamba waitikia wito Kamati ya Maadili ya CCM

Lumumba, Dar: Mzee Kinana na Mzee Makamba waitikia wito Kamati ya Maadili ya CCM

Ila huu utamaduni sio mzuri,huu wa kukomoana,maana una create circle ya kukomoana huko mbele,
Hata Kama sio wewe,watoto wajukuu,vitukuu wanaweza kuja kupata tabu,
Tuishi kwa upendo,ooh
 
siku nyingine usikiongelee chama cha ukombozi kama SACCOS ya ufipa, CCM ni chama cha wanachama wote sio chama chao

Hivi bado hawajakuona tu? Mimi CCM damudamu ila siwezi kuwa shabiki nisiyeng'amua mambo.

"NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU NI MWIKO"

Zidumu sera za TANU na CCM ya late 1970s na 1980s!!

Leo hii CCM chama changu kinapoteza ladha na hakuna uhondo wala msisimko wa kiuzalendo uliotizama maslahi mapana ya nchi, SIO CCM ya leo wengi wanaangalia nitapata nini binafsi. Nimtukuze mtu nionekane, niwatukane na kuwatisha maisha wapinzani nipate fadhila za walio juu!!!

Upinzani sio UADUI, bali chachu ya maendeleo
 
Sidhani kama kuna ukweli hapo, na ikiwa hivyo ni baada ya vikao vilvyofanyika, na hao wazee kutatua mambo na Mwenye kiti , sasa mambo ya kusawazisha na kwenda kwenye kikao, kunywa chai na wanachama wenzao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KINANA, MAKAMBA WAITIKIA WITO…

Makatibu wakuu wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Yusuf Makamba na Abdulrahaman Kinana wamefika mbele ya kamati ndogo ya Usalama na Maadili katika ofisi ndogo za CCM Lumumba Jijini, Dar
IMG-20200210-WA0159.jpg
IMG-20200210-WA0158.jpg

Kinana, Makamba na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe waliitwa mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM baada ya sauti zao kuenea katika mitandao ya kijamii zikieleza jinsi CCM inavyopoteza mvuto, uendeshaji nchi na jinsi chama kilivyoshindwa kuwalinda makatibu huo dhidi ya mtu anayewachafua.

Wengine ambao sauti zao zilisikika katika mkanda huo ni Nape Nnauye, ambaye ni mbunge wa Mtama, William Ngeleja (Sengerema) na January Makamba (Bumbuli) walimuomba radhi Rais John Magufuli.
 
Makatibu Wakuu Wastaafu, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula.

Baadhi ya Picha zinaonyesha jinsi walivyokuwa wakiingia ofisini Lumumba na pia kujiandaa na mahojiano.

IMG_1464.JPG
 
Finally agreed
Makatibu Wakuu Wastaafu, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula.

Baadhi ya Picha zinaonyesha jinsi walivyokuwa wakiingia ofisini Lumumba na pia kujiandaa na mahojiano.

View attachment 1353508

Jr[emoji769]
 
Mtu mwenye akili timamu alijua vizuri kuwa yaliyokuwa yanasemwa kuhusu hawa wazee ni uongo ambao ungejibiwa na muda.

Wazee wasingekataa kuitikia wito bali wanaweza kukataa yaliyojiri kwenye wito.

Tatizo la mitandao kwa sasa nchini ni uongo umekuwa ukitangulia kabla ya ukweli!
 
Back
Top Bottom