Naona hii HADITHI, inafanana na zile hadithi tamu za Said Bawji enzi zileeee za gazeti la SANI. Likitoka leo likiwa na hadithi ambayo haijaisha, na kuambiwa ITAENDELEA TOLEO LIJALO, basi unakaa na hamu ya kulisubiri TOLEO LIJALO kwa zaidi ya miezi miwili. Tofauti na hadithi za John Rutayisingwa tulizokuwa tukizisoma kwenye gazeti la Mzalendo,kila Jumapili, kabla hajahamia kwenye gazeti la Dimba na Rai.
Dunia imebadilika. Jiandae, malizia simulizi yako yote pembeni, kisha uilete hapa, yabaki maoni ya wasomaji. Na huko magazetini, kukatiza katiza simulizi, ni kwa ajili ya biashara, ili ununue tena gazeti lijalo. Sasa sijajua mleta simulizi hii, hii katiza katiza, zina lengo gani!