Luqman Maloto (Mwanahabari): (Hotuba ya Rais Samia) haikuwa hotuba yenye hadhi ya Mkuu wa Nchi

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
RAIS SAMIA HAHITAJI TENA MKALIMANI WA HASIRA!

Anaandika Ndimi Luqman MALOTO

HONGERA jeshi la polisi kwa kutimiza miaka 60. Yupo mtu aliniandikia ujumbe WhatsApp, unaosema: “Polisi inaposherehekea miaka 60, Dodoma inanuka damu.” Aliambatanisha na taarifa ya watu watatu waliouawa na kuchomwa moto!

Nikasikiliza hotuba ya Rais Samia kwa Jeshi la Polisi katika maadhimisho yao ya miaka 60. Kabla ya hotuba, na baada ya kifo cha Ali Kibao, nimekuwa mwenye hofu kubwa. Nilipomsikiliza Rais Samia, hofu ikaongezeka zaidi ya mara dufu.

Ali Kibao ameuawa. Mazingira ya kifo chake yanaogopesha, yanatia simanzi, yanafikirisha na ukomo wa fikra ni giza totoro. Taifa linahitaji faraja. Rais Samia ndiye mfariji wa taifa. Hotuba yake haijafariji, imekuza hofu.

Kosa kubwa la kiufundi ambalo Rais Samia alilifanya ni kutaka kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Mosi; kuungana na waombolezaji wa kifo cha Ali. Pili; kuwarudi kwa kishindo waombolezaji wa Ali, ambao wanataka majibu ya kifo chake.

“Mauaji haya hayakubaliki,” alisema Rais Samia. Ilikuwa kauli mwafaka. Alichokosea Rais Samia ni kujaribu kufanya ulinganisho baina ya kifo cha Ali dhidi ya majaribio mawili ya kuuawa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump. Alikosea pia kulinganisha kifo cha Ali na mauaji ya Albino.

Jaribio la kwanza, Trump alishambuliwa kwa risasi na kijana Thomas Crooks, 20. Alimjeruhi Trump sikio, halafu walinzi wa Trump kutoka Secret Service, walimuua Crooks. Shambulizi la pili, mshukiwa ni Ryan Routh, 58. Ameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mashitaka 100.

Ali Kibao, alishushwa kwenye basi na watu waliojitambulisha ni maofisa usalama, wakiwa na mitutu ya bunduki nzito. Wakamfunga pingu, wakaondoka naye. Kisha, wakamuua na kumtupa Ununio. Uchunguzi ulionesha mwili wake uliumizwa vibaya kwenye fuvu, pia alimwagiwa tindikali.

Unawezaje kufananisha majaribio ya Trump, ambayo wahusika wanafahamika, dhidi ya tukio la Ali? Uchunguzi unaoombwa kuhusu Trump ni kwamba upelelezi usiishie kwa Crooks na Routh peke yake, uende ndani zaidi. Uchunguzi wa Ali ni giza. Hakuna hata mshukiwa wa kwanza.

Rais Samia alichagua kuwa mtetezi wa vyombo vya usalama, hasa polisi. Bila shaka sababu kubwa ni hadhira aliyoihutubia, wengi ni maofisa wa ngazi za juu wa polisi. Kutetea polisi kipindi ambacho wanatuhumiwa kuendesha utekaji hadi mauaji ni hatari. Dola za kipolisi (Police States), kama Chile ya Augusto Pinochet, zilianza hivi.

Wapinzani walitekwa hadi kuuawa kwa siri. Pinochet alipotokeza, aliwapongeza maofisa wa polisi kwa kazi nzuri. Unalisifu vipi jeshi la polisi, wakati Sativa, amemtaja hadi jina ofisa wa polisi aliyeongoza utekaji dhidi yake, akapitishwa Oysterbay Police, akateswa, akapelekwa Arusha, kabla ya kutupwa msituni Katavi?

Rais Samia anafahamu kuwa jeshi la polisi na idara nyingine za usalama, haziundwi na malaika, bali binadamu ambao wameshathibitika kufanya makosa mengi. Kuua watu hata kubambikia kesi wasio na hatia. Rais Samia si mara moja, ameshanyoosha kidole kwa polisi. Haiwezekani leo atetee polisi, kisa wanaotuhumu ni wapinzani wake wa kisiasa.

Rais Samia alisema, Septemba 11, kuna chama kilifanya mkutano na kupanga njama za kihalifu. Alisema sauti zote za mipango yao wanazo. Kama ndivyo, kwa nini wahusika hawajakamatwa? Rais hapaswi kulalamika. Hakuna mwenye ruhusa ya kutenda uhalifu, awe mwanasiasa au kiongozi wa dini.

Kuna mahali, Rais Samia aliamua kufanya marejeo ya wanasiasa wanaoituhumu Chadema kuhusika na vitendo vya utekaji, akiwemo Dk Slaa. Swali ni lilelile; kama Chadema ni wahusika, kwa nini hawapelekwi mahakamani ili ukweli ujulikane? Rais Samia anapaswa kuiondoa nchi kwenye hizi tenzi za nadharia.

Mabalozi mbalimbali walizungumzia kuuawa kwa Ali Kibao na kutaka uchunguzi ufanyike. Inaonekana Rais Samia amekerwa na matamko ya mabalozi. Alisema, yeye hajawahi kuwaagiza mabalozi wa Tanzania, waziambie nchi nyingine cha kufanya pale matatizo yanapotokea. Swali; kama wewe hulii na misiba ya wenzako, ndiyo hutaki watu walie msiba ukiwa kwako? Lengo linakuwa nini?

Rais Samia alianza vizuri sana kidiplomasia. Hata kisiasa alifanya vema. Hotuba yake kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi, imetoa picha kuwa amepiga u-turn kubwa, kisiasa na kidiplomasia.

Ni kama analaumu falsafa ya “R4”, aliyojinasibu kuitumia kuimarisha demokrasia kwa “maridhiano, uhimilivu, mageuzi na ujenzi mpya wa nchi”. Sasa, Rais Samia anasema “R4” zisiwe uchochoro wa kuvunja sheria. Anakumbusha nchi ilipotoka kabla ya yeye kuwa Rais. Je, anawaza kuirudisha nchi ilipotoka?

Namkumbusha, Rais Ali Mwinyi, katika kitabu chake “Mzee Rukhsa”, ameandika “Demokrasia ni kama jini, ukilitoa kwenye chupa, huwezi kulirudisha.” Maana yake, kuruhusu demokrasia, halafu kujaribu kuiminya, lazima kuwepo na madhara.

Zamani, Rais Samia alipohutubia, alimudu kuficha hisia na hasira zake. Dhahiri, alihitaji mkalimani wa hasira (anger management translator), wa kufikisha ujumbe mahsusi ili wengine watambue hisia zake. Kwa hotuba ya Rais Samia, miaka 60 ya Jeshi la Polisi, hahitaji tena anger translator.

Rais Samia sasa anazungumza na kuruhusu hasira na hisia zake, vionekane waziwazi. Haikuwa hotuba yenye hadhi ya Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu wala Mfariji Mkuu wa Taifa. Ni hotuba ya mlezi na mtetezi wa vyombo vya usalama.

Ni hotuba iliyowaacha wananchi kwenye wasiwasi na mashaka juu ya usalama wao. Wanaodai kutishiwa maisha na walio hatarini kutekwa, waende wapi? Je, waliotekwa pasipo kujulikana walipo? Vipi waliopoteza ndugu zao? Wakimbilie wapi baada ya kuambiwa “kifo ni kifo?”

Taifa lilipiga mayowe kila kona mtoto Asimwe (mwenye ualbino), alipouawa na kunyofolewa viungo. Angalau watuhumiwa walifikiwa na kufikishwa mahakamani. Hata baba yake mzazi yumo. Ndivyo, wanataka wahusika wa kifo cha Ali Kibao, nao wapatikane. Si kweli kuwa watu hawajali vifo vya watu wenye ualbino.

Kusema vifo vingine huwa havipigiwi kelele ni kugawa watu. Watu waseme “wanasiasa wakiuawa wao ndiyo sauti zinapazwa”. Huu ni mchezo wa kikoloni, “divide and rule” – “wagawe uwatawale”. Chonde Rais Samia.

Source: Ndimi Luqman MALOTO
 
Wengi hawajailelewa hotuba ya mh raisi ila ni hotuba bora kupata kutolewa!
Ni hotuba bora kabisa hususan kwa wale mliowaona pale ukumbini wakimshangilia sana.

Na wewe haiyumkiniki wewe ulikuwepo ukumbini na kabla ya hapo mlishuhudia shughuli ya graduation ya polisi na walionesha namna mnavyoweza kuwashambulia wananchi wenye vibendera na sauti za tunataka haki zetu.

Ni hotuba nzuri kwenu
Ni hotuba hatari kwa usalama wa Taifa
 
Nimesikitika sana kwa hotuba ile

The Hate Speech.
 
Ni hotuba bora kabisa hususan kwa wale mliowaona pale ukumbini wakimshangilia sana.

Na wewe haiyumkiniki wewe ulikuwepo ukumbini na kabla ya hapo mlishuhudia shughuli ya graduation ya polisi na walionesha namna mnavyoweza kuwashambulia wananchi wenye vibendera na sauti za tunataka haki zetu.

Ni hotuba nzuri kwenu
Ni hotuba hatari kwa usalama wa Taifa
Tukutane mwembe togwa trh 23!
 
Good analysis.Tuongozwe Kwa Sheria Siyo Kwa ukarimu wa Mtu.
 
Unapompatia mwanamke majukumu makubwa yanayohitaji uamuzi yakinifu tegemea uharibifu.

Hawajaumbwa hivyo niwadhaifu kiasili hata huku majumbani tunaishi nao.

Ile speach alionesha udhaifu mkubwa ni bara angeendelea kuishi kmya kuliko alivyopuyanga.

Kwa dunia ya leo hakuna kiongozi anaweza kuzuia watu kumpinga na kumkosoa maana ina watu waelewa na wasomi ukichangia na teknolojia jukumu lake sio kujibu kila anachoambiwa na wapinzani bali atimize majukumu yake kulingana na katiba inavyomtaka. Nasio kutetea kundi fulani.

Ngoja siku polisi wakimgeuka anajitoa ufahamu wakati polisi hana rafiki, wale ni mashetani wakimaliza upinzani wataitafuta damu hukohuko kwenu.

Wale wa karibu na huyo mama mwambieni tu kwamba "Nchi haindeshwi kwa mihemuko".
 
Ni hotuba bora kabisa hususan kwa wale mliowaona pale ukumbini wakimshangilia sana.

Na wewe haiyumkiniki wewe ulikuwepo ukumbini na kabla ya hapo mlishuhudia shughuli ya graduation ya polisi na walionesha namna mnavyoweza kuwashambulia wananchi wenye vibendera na sauti za tunataka haki zetu.

Ni hotuba nzuri kwenu
Ni hotuba hatari kwa usalama wa Taifa
Wengi kwenye hotuba za viongozi wakuu huwa hawapigi makofi kwa sababu ya "contents" zilizomo kwenye hotuba hizo bali posho watakazopokea au walizopokea!
Ndo maana hata kiongozi akiwatukana wataishia kucheka tu kama mazuzu na kupiga makofi ya kinafiki.
Akili za tumboni ni mbaya na zinadhalilisha utu!
 
Waliomwandalia rais hotuba hawana lengo nzuri kabisa, wamenganisha rais na wananchi, na wafadhili IMF na WORLD BANKS. mwakani kuna uchanguzi mkuu pesa anategemea huko huko na amehalibu.
 
Wamemchonganisha rais na wananchi, mataifa makubwa,wadhili, pamoja WORLD BANKS NA IMF na mwakani kuna uchanguzi mkuu ? Waachia nafasi. au rais ameamua mbwai na iwe mbwai ? Hata gombea mwakani?
 
Back
Top Bottom