John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Nukuu za aliyoyazungumza Mbunge wa Jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde, leo Jumatatu Februari 7, 2022:
"Sikiri kuwa, kuna makundi yanayoutaka urais kwa maana wanasubiri ratiba kugombea, bali kuna makundi haramu yanayotaka kugombea urais 2025 ambao wanaanza mapema kabla ya wakati, mimi kundi langu ni kundi linaloongoza nchi kwa sasa.
"Vyama vinavyotunyooshea vidole havina uhalali hata kidogo, vyama vingine vina miaka 30 lakini hata ofisi hazina, hivi ingetokea aliyeanzisha benki angejenga kwa matope na kuezeka kwa majani hivi kuna mtu angeamini na kuweka fedha zake kweli.
"Baada ya kutoka katika uongozi wa chama (CCM), Dkt. Bashiru Ally ameendelea kuonyesha ukomavu na ukubwa wake tangu mwanzo, anazungumza pale inapobidi na ananyamaza inapobidi. Mwenendo wake uko vizuri. Kuhusu, Polepole yeye yuko tofauti na Dkt. Bashiru.
"Ukiwa ni mbunge wa kuteuliwa na Rais, maana yake wewe jimbo lako ni Ikulu, hivyo hata mwenendo wako unapaswa kuwa sawa na mwenendo wa Ikulu.
"Kuna baadhi ya watu ambao wamechelewa kumuelewa Rais Samia anataka nini, yawezekana mmoja wao ni Polepole.
"Kuhusu kauli ya Rais Suluhu Samia kuwaonya mawaziri kuwa ni vyema wakawa wanaheshimiana wao kwa wao na wakati mwingine ni vizuri wakafuata methali za Kiswahili kwamba mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, kufuatia kauli hiyo, hakuna sehemu Rais aliwaambia waibe.
"Nimefuatilia ukosoaji wa Polepole kuhusu kauli ya Rais ya mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, niseme tu hakumwelewa Rais, kula urefu wa kamba ni kula vitu ambavyo umepangiwa kisheria, ukiwa waziri unapata stahiki nyingi ikiwemo posho zaidi, usafiri.
"Zipo njia za kukosoa anazotumia Polepole si sahihi, zipo njia sahihi na rasmi za kuwasilisha maoni yake yanayokosoa. Polepole siyo mlafi wa madaraka, lakini nahisi kuna tatizo fulani sehemu fulani.
"Rais Samia alisema atalinda mila na desturi, dhambi iko wapi? Machifu wa zamani walikuwa wanatoza kodi, walikuwa wanahukumu, wakipita walikuwa wanabebwa, je machifu wa sasa wako hivyo? Ni wapi chifu alizuia shughuli zisifanyike.
"Kwa namna tunavyokwenda na kwa kasi anayokwenda nayo Rais Samia na namna anavyofanya kazi bila kufokea mtu huku matokeo yakionekana, napata mashaka ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2025 utakuwa ni mkubwa sana kuliko ilivyokuwa 2020.”