Bwawa la nyerere haliwez kukamilika Leo Wala kesho labda 2025 huko.
Nilijaribu kumuuliza mtu ambaye Ni rafik yangu yupo huko Kama engineer aliniambia kila kitu na Mambo mengi Sana .
Ukweli wanasiasa Ni watu waongo balaa sijui why wanadanganya kwenye vitu sensitive Kama hivi.
Unawezaje kuongea uongo wa mchana kweupe wakat unajua fika hili jambo haliwezekan kwa wakati fulani?
Pia rafik angu alinidokeza kuwa Kuna mitambo inatakiwa ipelekwe huko site lakin hiyo mitambo haiwez kufika salama lazima ijengwe barabara ya lami kutoka mkata km sikosei Hadi huko Rufiji na hiyo barabara Bado haijajengwa.
Pia nikamuuliza vipi speed ipoje ,akanihakikishia kuwa katika mradi unapelekwa kwa speed kali basi Ni huo mradi ,Ila changamoto tu Ni uongo wa wana siasa kuwahadaa wananchi wao.
Hivyo mradi unaendelea kwa speed kali lakin itachukua muda mrefu kukamilika maana mradi Ni mkubwa balaa ,miaka minne au mitano mbele ndipo mradi utakamilika ,so acheni kusikiliza hao Wana siasa uchwara .