Luteni Ian Kagame

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
Pichani ni Ian Kagame (jina lake kamili ni lan Kagame Deogratius Rutagambwa) ambaye alijiunga na jeshi la nchi hiyo wiki iliyopita.

Ian alikuwa ni miongoni mwa Maofisa cadets 568 waliopewa kamisheni katika Chuo cha Kijeshi cha Rwanda ambao waliweza kufaulu mafunzo ya kijeshi nchini Rwanda, kemisheni hizo zilitolewa na Rais Paul Kagame mwenyewe.

Ian Kagame Deogratius Rutagambwa ambae ni moja ya askali wapya katika jeshi la Rwanda alijiunga na Chuo cha kijeshi cha Royal Military Academy huko Sandhurst nchini Uingereza mnamo Agosti 8, 2021 na kuhitimu mafunzo yake Agosti 12, mwaka huu ambapo alitunukiwa cheo cha Luteni wa Pili (Second Lieutenant).

Chuo hiki cha Royal Military Academy cha huko Sandhurst ni miongoni mwa vyuo bora vya Kijeshi nchini Uingereza, vinavyo wafunza watoto wa viongozi wakubwa duniani, hasa kutoka Afrika, Mtoto wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba pia alipata mafunzo yake chuo hiki na kuhitimu mwaka 2000.

Hiyo Tisa, Kumi ni Kwamba...

Ian alikuwa ni miongoni mwa askali 24 maalumu waliopelekwa nje ya nchi kupata mafunzo muhimu, Ian Kagame Deogratius Rutagambwa ni mtoto wa 3 kuzaliwa kati ya watoto wa Kagame na mtoto wa pili wa kiume.

Huyu ndio mtoto pekee wa Kagame aliweza kufaulu mafunzo ya juu ya kijeshi na kujiunga na jeshi la nchi hiyo, mtoto mkubwa wa Kagame aitwae Ivan aliachilia masomo katikati katika Chuo cha Kijeshi cha West Point huko Marekani mwaka 2010 miezi miwili tu baada ya kujiunga, Alisema hakupendezwa na Jeshi.

Huyu Ivan alimkatisha tamaa baba yake sana, Paul Kagame alikili hilo hadharani.

Kuna tetesi kwamba Rais Kagame anapanga Ian (Ian Kagame Deogratius Rutagambwa) achukue nafasi yake mwaka 2034, awe ndio mrithi wake wa kiti cha uraisi.

MUHIMU: Itambulike ni tetesi..[emoji1]

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu CMCAView attachment 2414354View attachment 2414358View attachment 2414355View attachment 2414356View attachment 2414357
 
Wapi Wema Sepetuh?
 
PAK ana elimu Kiwango gani?

Kwa mtiririko wa kawaida. Elimu ya kagame ni form six ama high school.

Maana aliacha chuo kikuu Makerere akiwa mwaka wa kwanza na kujiunga na jeshi.

Mseveni alimpeleka kusoma chuo cha kijeshi marekani.. kinaitwa general staff college.

Wanaojua elimu za kijeshi zilivyo mtiririko wake ndio wanajua zaidi
 
Asante Mkuu. Una kitabu Chochote kimezungumzia historia yake? Komredi Zuma haikufika hata std 7, ndo maana tulishuhudia vibweka ikiwemo kubaka na kudai kunawa immediately baada ya tendo
 
Kuna nchi wakati mwingine kutawaliwa na madikteta au krithishana ni afadhali kuliko kuacha demokrasia ichukue mkondo wake. Rwanda, Uganda ni nchi ambazo demokrasia yao ni mtutu wa bunduki.
Kagame yuko hapo ili kuweka mtengamano wa kisiasa nchini rwanda. Vinginevyo angeshtakiwa kwa kutungua ile ndege mwaka 1994.
Acha watawale, na watoto wao na wajukuu wao. Kinyume chake ni mtutu wa bunduki kutawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…