Hapana.
Unaudhika vipi kwa kupewa elimu usiyoifahamu?
Mhandisi...
Hili ndilo linalonishangaza mimi.
Mathalan.
Mwalimu kachukua uongozi TAA 1953 lakini haielezwi kauchukua uongozi huo kutoka kwa nani.
Mimi nimeeleza kuwa Mwalimu kachukua uongozi kutoka kwa Abdul Sykes katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo.
Uchaguzi ulikuwa wa kuonyesha mikono na Returning Officer alikuwa Dennis Phombeah Mnyasa kutoka Nyasaland na ndiye alikuwa Meneja wa Arnautoglo Hall.
Huyu Phombeah ilipokuja kuundwa TANU 1954 kadi yake ya TANU ikawa no. 5.
Uchaguzi ule ulikuwa mgumu sana kwa kuwa Nyerere hakuna aliyekuwa anamjua anashindana na Abdul Sykes aliyekuwa Act. President na Secretary wa TAA.
Abdul kijana maarufu wa mjini na mtoto wa Kleist Sykes muasisi wa African Association.
Lakini nikaeleza kuwa kulikuwa na mpango kuwa Nyerere lazima ashinde uchaguzi ule kwani hayo ndiyo yalikuwa maamuzi yaliyopitishwa Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu na walioshiriki katika kikao hicho ni Mwapachu, Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.
Kisa hiki naamini unakifahamu nimekieleza mara nyingi hapa barzani.
Mwalimu katika hotuba yake ya kuaga Diamond Jubilee kasema tu kuwa, "wakanichagua kuwa Rais wao."
Nani waliomchagua hakueleza.
Mimi nimesherehesha kwa kiasi changu hadi kusema kuwa Dennis Phombeah alimfanyia kampeni Nyerere ashinde yeye alikuwa hajui kuwa uchaguzi ule ulikuwa ushapangwa na kamati ya ndani ya TAA kuwa huu ndiyo uchaguzi wa mwisho na 1954 TANU inaundwa na Nyerere ataongoza harakati za kudai uhuru.
Ndugu zangu wanasoma historia hii hasira zinapanda.
Wanasema mimi "mdini" na "mchochezi."
Hawataki kusoma historia ya Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hawataki kusoma historia ya Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika aliyekuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya kwanza UNO 1955.
Prof. Haroub Othman aliposoma kitabu changu historia hii ilimuathiri sana akataka uhakika zaidi na alizungumza na Mwalimu na akazungumza na Ahmed Rashaad Ali rafiki wa Abdul Sykes katika uhai wake.
Prof. Haroub hakughadhibika alihangaika kutafuta ukweli wa yale niliyoandika.