Lutheran Primary School Moshi ilivyokuwa 1958 na sasa

Lutheran Primary School Moshi ilivyokuwa 1958 na sasa

Gold ...
Umenitukana.
Sifanyi mjadala na mtu mwenye kutukana.
Maswali magumu unatafuta sababu za kuyakwepa, si ndiyo? Tuwekee hiyo nukuu yote husika kwenye Kitabu cha Listowel siyo kutuambia tusome kurasa fulani. Huyo Listowel alikuwapo kwenye mkutano? Hii siyo natural science mzee, kama Physics, Mathematics, Chemistry na Biology where hard facts rule by way of incontrovertible evidence or poof, if you will. Ukidanganya hapa kama unavyofanya, mambo yako ya siku zote ya "He said, She said", bila ushahidi wowote, watu wanachukulia kama ndiyo ukweli. Sasa naomba utuwekee nukuu za kurasa kutoa kwenye hicho Kitabu cha Listowel na chanzo cha taarifa zake.
 
Na Mwalim Cecil Matola, V.Kyaruzi , C. Mtamila na wengine
Kwahiyo Historia haikamiliki bila kuwataja Abdul Sykes na Baba yake!

Historia ya Mwl Nyerere umeieleza kwa ''cherry-pick'' unapoeleza jambola ''Wazee wako'' .

Nyerere anaonekana zaidi anapopewa sh 200 na Mshume Kiyate akanunue mboga !

Pale anapokaaingiwa mayai nyumbani kwa Abdul Sykes n.k

Hutamsoma Nyerere kama katibu wa Tawi la Tabora, wala kumsikia kama mtu aliyeleta mapinduzi ndania ya siasa za Dar es Salaam kwa kukiwekea chama misingi wa Katiba na kukisambaza majimboni kwa nguvu kuliko ilivyowahi kutokea.

Role ya Nyerere ilikuwa transformation ya chama kutoka katika 'jamii au Familia'' kuwa chama cha siasa. Huo ndio msingi wa kuandika katiba ya chama.

Nyerere alibaini kukiacha chama kilivyo kutatokea matatizo kitakapopanuka zaidi.

Matatizo ni yale aliyoeleza Mohamed Said katika kitabu chake yakimhusisha Abdul Sykes na wahuni walipovamia Ofisi na kubagaza baba zao.

Ile ilikuwa ''red flag'' ya chama kukosa muongozo.

Uchaguzi wa Arnatouglo unadhahirisha kwamba chama kilikuwa katika ''transition'' iliyosaidia sana transformation kwenda TANU na ku define siasa za nchi hii hadi leo.

Kwako Nyerere ni daraja la kumpamba Abdul Sykes, lakini historia inasahihisha hilo ndio maana Nyerere hayupo miaka 20 lakini ''anajibu'' hoja zako kutoka alipo! hahitaji kuandikiwa kitabu kuna uhitaji wa vitabu vinavyomhusu.
Nguruvi3,
Huu ukurasa unatoka katika kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Kitabu hiki ndicho kitabu cha kwanza kuchapwa kuhusu historia ya TANU.

Listowel alikuja Tanganyika mwaka wa 1963.

Nimesoma barua za Listowel alizokuwa akiandikiana na Ally Sykes katika Nyaraka za Sykes na baadhi nimezifanyia rejea katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Bahati mbaya Mwalimu hakupendezewa na jinsi Listowel alivyomwandika na alimwandikia barua ya malalamiko.

Mwenyeji wa Listowel Dar es Salaam alikuwa Ally Sykes na mtu aliyewaunganisha alikuwa Peter Colmore kutoka Nairobi mshirika wa Ally Sykes katika biashara.

Ukurasa huu unaeleza uchaguzi wa TAA wa April 1953 Arnautoglo Hall kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere.

Listowel ameeleza kuwa Nyerere alipata ushindi mdogo.

20220404_065351.jpg

1649046800001.png
 
Umesomea shule za kanisa..leo unaliponda kanisa kusema lina wahukumu..absurd kabisa.

Liombe msamaha kanisa...au ndio shukrani ya punda.

#MaendeleoHayanaChama
 
Umesomea shule za kanisa..leo unaliponda kanisa kusema lina wahukumu..absurd kabisa.

Liombe msamaha kanisa...au ndio shukrani ya punda.

#MaendeleoHayanaChama
Jiwe...
Wapi nimeliponda kanisa?
Weka hapa ushahidi.
 
Mzee Shkamoo. Asante kwa kumbukizi nzuri.

Ila watu wa zamani walijua namna ya kujenga nyumba Imara.
 
LUTHERAN PRIMARY SCHOOL MOSHI KAMA ILIVYOKUWA 1950s NA SASA

Nilianza darasa la kwanza mwaka wa 1958 kwenye jengo hilo hapo chini lililokuwa ni Kanisa la Kilutheri.

Baada ya miaka mingi nilifika Moshi kuangalia pale nilipoanza shule.

Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 20 December, 1986 na nikapiga picha hiyo ya kwanza nimesimama kwenye mlango wa kuingilia kanisani ambako ndiko nilipoanza kusoma.

Ile piano ambayo Mwalimu Paul alikuwa akipiga na sisi wanafunzi tukiimba ''hyms,'' ilikuwa pale pale ilipokuwa mwaka wa 1958.

Piano ile ilirejesha kwangu kumbukumbu nyingi pamoja na nyimbo nilizojifunza pale na zote nikizikumbuka kama vile niliziimba jana ---''Damu ya Kondoo,''Ni Nani Aliyetuumba ni Mungu Mwenyewe,'' ''Ewe Mwezi ni Rafiki Yangu,'' ''Tunamsifu Baba Marehemu Kingi George.''

Kuzunguka kanisa kulikuwa na bustani nzuri ya maua ya rangi tofauti na kulikuwa na ukoka uliopandwa kiasi huoni ardhi.

Mwalimu Paul alikuwa mtu mzima na ndiye aliyeniandikisha shule nikiwa na miaka sita.

Alikuwa siku zote akivaa pama hata darasani.

Alikuwa akitufundisha kuwa watu wakifa wanakwenda mbinguni.

Miaka miwili tu mama yangu alikuwa amefariki na ndiyo sababu ya mimi kuchukuliwa na mama yangu mdogo na kujanae Moshi alipokuwa akifanya kazi katika Nursing Home ya Mgiriki Dr. Georgedis nianze shule.

Hospitali hii ilikuwa makhsusi kwa Wazungu tu.

Kwa kuwa Mwalimu Paul alikuwa akitufunza kuwa watu wakifa wanakwenda mbinguni nilikuwa na kawaida ya kukaa kwenye ukoka kwenye bustani peke yangu na wakati mwingine nikilala chali kuangalia juu mawinguni nikitegemea kumuona mama yangu.

Namkumbuka mwanafunzi mwenzangu umri sawa na mimi akiitwa Njuguna wakati mwingine akija kukaa na mimi pale bustanini.

Njuguna alikuwa mzuri na nikipenda sana awe karibu yangu.

Miaka ilisogea na pamoja tukawa wakubwa kiasi miaka miaka 12 hivi.

Siku moja kwenye fete alipewa microphone akaambiwa aimbe nyimbo yoyote aitakayo.

Junguna akaimba, "Oh Carol," ya Neil Sedaka kwa ustadi mkubwa sana.

Kila niisikiapo nyimbo hii humkumbuka Njuguna.

Njuguna ametangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita.

Namkumbuka Hidaya yeye tukifuatana pamoja kwenda shule.

Siku moja nikauliza kama Hidaya yuko mjini.

Nikafahamishwa kuwa amefariki miezi michache iliyopita.

Alikuwa nurse Hospitali ya Mawenzi.

Majonzi yalinijia ingawa tulipoachana sote tulikuwa watoto wadogo labda wa miaka 10.

Miaka imekwenda wapi?

Picha hiyo ya pili nimeipiga tarehe kama hii ya leo mwaka jana nikapiga sehemu ile niliyosimama mwaka wa 1986 miaka 36 iliyopita.

Kanisa ambalo ndani yake ndiko lilipokuwa darasa langu la kwanza pamebadilika sana kama inavyoonekana kwenye picha.

View attachment 2163433
Nakupa salute mkuu.Hakika wewe ni mmbobezi mwenye weledi kwenye historia ya Tz kabla na baada ya uhuru.Mwenyezi Mungu sub hannah akupe maisha mema na marefu yenye amani uendelee kutuhabarisha.Wewe ni hazina.Nikutakie Ramadhan Kareem.
 
Mount...
Amin kwa sote.
 
Nguruvi3,
Huu ukurasa unatoka katika kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Kitabu hiki ndicho kitabu cha kwanza kuchapwa kuhusu historia ya TANU.

Listowel alikuja Tanganyika mwaka wa 1963.

Nimesoma barua za Listowel alizokuwa akiandikiana na Ally Sykes katika Nyaraka za Sykes na baadhi nimezifanyia rejea katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Bahati mbaya Mwalimu hakupendezewa na jinsi Listowel alivyomwandika na alimwandikia barua ya malalamiko.

Mwenyeji wa Listowel Dar es Salaam alikuwa Ally Sykes na mtu aliyewaunganisha alikuwa Peter Colmore kutoka Nairobi mshirika wa Ally Sykes katika biashara.

Ukurasa huu unaeleza uchaguzi wa TAA wa April 1953 Arnautoglo Hall kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere.

Listowel ameeleza kuwa Nyerere alipata ushindi mdogo.

View attachment 2174930

View attachment 2174943
Wee mzee mjinga sana. Unasema mzungu Listowel mwenyeji wake alikuwa Sykes, na hapohapo unamchukulia huyohuyo Listowel kama chanzo chako kikuu kuhusu uchaguzi wa TAA Arnatouglou? How dumb do you possibly think we might be? Kwanza huyo mzungu hajaweka takwimu za matokeo ya uchaguzi husika, na nikisoma maandishi yake, ni wazi anaandika kijuujuu tu na kimasihara sawaswa na umbeya. Hakuna facts hapo wee mzee. Ni wazi umeamua tu kumwamini mtu mmoja, Listowel, sababu ni Mzungu Mwingereza rafiki wa Sykes ili ku support hoja yako nzima kuhusu matokeo ya uchaguzi wa TAA Arantoglou. Huna vyanzo mbadala zaidi ya huyo Listowel rafiki wa Wajomba zako?
 
Huyo Mzungu Listowel hajataja hiyo «small margin» ni kura ngapi za ushindi kati ya kura ngapi zilizopigwa jumla. Tuambie wewe sasa.
 
Hiyo source yako ya Mzungu Listowel inaleta mashaka sana. Hamna details kama tarehe, na hard evidence/facts. It all looks very superficial and suspicious, and possibly intentionally so.
 
Nguruvi3,
Huu ukurasa unatoka katika kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Kitabu hiki ndicho kitabu cha kwanza kuchapwa kuhusu historia ya TANU.

Listowel alikuja Tanganyika mwaka wa 1963.

Nimesoma barua za Listowel alizokuwa akiandikiana na Ally Sykes katika Nyaraka za Sykes na baadhi nimezifanyia rejea katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Bahati mbaya Mwalimu hakupendezewa na jinsi Listowel alivyomwandika na alimwandikia barua ya malalamiko.

Mwenyeji wa Listowel Dar es Salaam alikuwa Ally Sykes na mtu aliyewaunganisha alikuwa Peter Colmore kutoka Nairobi mshirika wa Ally Sykes katika biashara.

Ukurasa huu unaeleza uchaguzi wa TAA wa April 1953 Arnautoglo Hall kati ya Abdul Sykes na Julius Nyerere.

Listowel ameeleza kuwa Nyerere alipata ushindi mdogo.

View attachment 2174930

View attachment 2174943

Mohamed
Ukisoma hiyo barua utaona mambo yanayo ''negate'' kitabu chako

Soma kuanzia hapo visitors walipokuwa ''indignant , sad, and frustrated''
Ni wazi walikuwa na matumaini na Nyerere kiasi alikubali ''pressure'' ya kuingia katika uchaguzi

Mohamed Said anasema Nyerere alipendekezwa na Abdul Sykes kule Nansio Ukerewe

Pili Nyerere aliingia katika uchaguzi akipingwa na Abdul Sykes, ikiwa Abdul alitaka Nyerere achukue uongozi ilikuwaje akaweka jina lake?

Na hapa inashadidiwa na barua inaposema ' To save both Abdul Sykes and Nyerere embarrassment... '' kwa maana kulikuwa na mtifuano si kwamba Abdul Sykes alipenda.

Barua inasema Denis Phombeah alimpigia Nyerere chapuo na alishinda kwa kura chache
Bila kujali kura ngapi kilichotokea ni Abdul Sykes Kubwagwa na hapo ndipo point ilipo

Lakini pia barua inathibitisha kile tunachosema kila siku.
Soma aya ya mwisho '' ...marafiki zake wakamta abadilishe T.A.A kuwa Taasisi ya kisiasa.

Kwa maana kwamba haikuwa Taasisi kama ilivyotarajiwa
Nyerere alibadili vipi ! kwanza kuwa na KATIBA

Huko nyuma niliandika kuwa Nyerere alifanya ''transition na transformation'' na ndicho ''marafiki zake walichotaka'' kwa mujibu wa Listowel
 
Nguruvi,
Mimi sina tatizo na vipi unavyoiona historia hii.

Hii kwako ni historia mpya mara ya kwanza umeisoma kwangu kama alivyoisoma mwalimu wangu Prof. Haroub Othman na ikamtaabisha sana.

Kama Abdul Sykes angetoa jina lake katika uchaguzi ule bila shaka wengi wangechukulia kuwa kaghadhibika.

Tambua kitu kimoja kuwa hicho chama kaasisi baba yake 1929 na akina Sykes walikuwa na ushawishi mkubwa sana katika TAA na katika siasa za Dar es Salaam.

Tambua kuwa Abdul Sykes alikuwa Secretary na Act. President kutokea 1951 - 1953.
Halafu Abdul na Nyerere walikuwa marafiki wakubwa sana.

Inasikitisha kuwa Nyerere hakupata kueleza haya.

Kuna kitu kimoja hukijui kuwa TAA ilikufa Nyerere alipochukua uongozi na ikabidi Abdul na Dossa waingie kati kurejesha imani za wanachama.

Hii ndiyo sababu mikutano mingi ya viongozi wa TAA ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na ikawa hivyo hadi TANU ilipoundwa na baada ya hapo.

Nacheka peke yangu kama mwehu.
Wewe Listowel unamkubali sana.

Kwangu mimi Listowel kajitahidi sana katika kitabu chake hiki.
Sasa kama nisingendika kitabu cha Abdul Sykes haya mnayojadili hapa mngeyajuaje?

Kwa nini hushangai imekuwaje historia hii yote ikafutwa?
Kilikuwa kinatafutwa kitu gani?

Tarehe 27 April, 1985 Nyerere alipokuwa anastaafu katika viwanja vya Ikulu alitoa jumla ya medali 3,979.

Abdul wala mdogo wake Ally na wengi aliokuwanao katika kupigania uhuru wa Tanganyika hawakuwa kwenye orodha.

Abdul na wenzake wote niliowataja katika kitabu cha Abdul Sykes hawakuambulia kitu.
Haikushangazi?

Iko siku nitakuwekeeni hapa vituko vya Lady Judith Listowel.
Alikuwa akimchekesha sana Ally Sykes wakati wa utafiti wa kitabu chake.

Huyu mama alikuwa na fedha nyingi sana.
Mumewe ni kutoka House of Windsor na alipata kuwa Gavana Ghana.

Huwa jamaa wananiambia kwa nini siandiki kitabu cha maisha yangu kwani ninajua mengi sana.

Siku nilipopokea nakala ya Kiswahili niliandika tarehe yake.

View attachment 2175878
 
Mzee MS kumbe hao unaowaponda leo ndio walikusaidia kupata elimu dunia sijui walikufanya nini mpaka umewachukia na kuwazushia uwongo mwingi
 
Mzee MS kumbe hao unaowaponda leo ndio walikusaidia kupata elimu dunia sijui walikufanya nini mpaka umewachukia na kuwazushia uwongo mwingi
Belo,
Kuna siri kubwa katika uandishi wa hadharani kama huu na hasa kwa namna niandikavyo.

Ingekuwa mimi naandika chuki nisingekuwa hapa nilipo kuwa navutia wasomaji wengi kunisoma na kufanya mjadala na mimi.

Ikiwa umesoma chuki, matusi au uongo kutoka kwenye kalamu yangu uanike hapa barzani watu wausome.

Kuhusu elimu nimesoma shule za misheni, za serikali na halikadhalika madrasa.

Nimesoma vilevile vyuo vya serikali ya Tanzania na vyuo vingine nje ya Tanzania.
 
Sema usemavyo,ni ujuha na utumwa kuona dahari kutumia lugha ngeni hasa ya mkoloni na bwana wa biashara ya utumwa
Ms mwenyewe aliandika kitabu chake toleo la kwanza kwa lugha ya malkia.
Na anafurahia kuwa spotted na Cambridge and other.
Tulia tu Mkuu
 
Historia kama historiaaaaaaaaaaa
Mzee mtoa mada uutibu moyo wako kwanza khe
Kwani Tanganyika Tz sijui TANU blablabla nyiiingi what 4?
Hama kama hupendezwi na historia iliyopo
Kila siku tunakuambia udini unakuumiza Mzee relax hakuna aliyerudi toka mbinguni kuzimu ahera akatuhakikishia Mungu wa kweli
Wasimulie wajukuu na vitukuu vyako hizi historia za abunuwasi
Waliokupa Elimu ambao ni Christian schools kuuuuutwa kuwananga
 
Pakawa,
Huu ni ukumbi huru mtu ana haki ya kuandika apendacho mradi hatukani.

Ikiwa wewe hupendezewi na kalamu yangu njia nyepesi ni kuacha kunisoma.

Ukiiona post yangu unapita wima.

Kunisoma kisha ukaja hapa kunibughudhi huu si uungwana.

Kuhusu elimu yangu nimesoma kwingi duniani si kuwa elimu yangu ilikuwa mahali pamoja.

Mathalan hii elimu ya mnakasha yaani mijadala kanisomesha Sheikh Haruna kwenye madrasa yake.

Wajukuu wangu ni umri wa chekechea wanaoweza kusomeshwa na mimi ni vijana wa umri wako ambao ni marika ya wanangu.

Wala hapa hapana dini nisomeshayo ila naeleza mchango wa Waislam katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ikiwa huipendi historia hii jiepushe nayo.
 
Nguruvi,
Tambua kitu kimoja kuwa hicho chama kaasisi baba yake 1929 na akina Sykes walikuwa na ushawishi mkubwa sana katika TAA na katika siasa za Dar es Salaam.
Mohamed Said, huchoki kusema uongo? Aliyeasisi na aliyekuwa Rais wa kwanza wa AA mwaka 1929 alikuwa ni Mwalimu Cecil Matola au unataka tukumbushane?
Tambua kuwa Abdul Sykes alikuwa Secretary na Act. President kutokea 1951 - 1953.
Mohamed Said, uongo mwingine huu. Hebu elezea...Abdul Sykes aliupataje U-President wa TAA 1951? Alichaguliwa na nani katika kikao gani? Yawezekana alikaimu hiyo nafasi baada ya bosi wake, Dr Vedasto Kyaruzi kupewa uhamisho na Wakoloni.
Kuna kitu kimoja hukijui kuwa TAA ilikufa Nyerere alipochukua uongozi na ikabidi Abdul na Dossa waingie kati kurejesha imani za wanachama.
Mohamed Said, duh! Hata aibu hakuna. Eti TAA ilikufa baada ya Nyerere kuchaguliwa kuwa kiongozi wake mkuu (President). Huu uzushi unautoa wapi? Believe this and you will believe anything (James Hadley Chase!)
Hii ndiyo sababu mikutano mingi ya viongozi wa TAA ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na ikawa hivyo hadi TANU ilipoundwa na baada ya hapo.
Naomba usiturudishe katika historia ya nyumba walikokuwa wakikutana waasisi wa AA mwaka 1929!

Yaani mimi nacheka tu...wakati mwingine natamani hata kukaa kimya. Niliwahi kuuliza Abdulwahid Sykes alikuwa nani ndani ya TAA ilipoanzishwa mwaka 1948 baada ya Zanzibar kujitoa AA? Abdulwahid Sykes alikuwa nani ndani ya AA/TAA wakati Mwalimu tayari ni kiongozi wa AA Tabora mwaka 1945? Nikauliza Abdulwahid Sykes alikuwa nani ndani ya TAA mwaka 1953 alipogombea uongozi wa juu wa TAA kwa kupambana na Mwalimu Nyerere?

Kwa hili swali la mwisho, waongo watadai Abdulwahid ndiye alikuwa Raisi! Hapana, Abdulwahid Sykes hakuwahi kuchaguliwa kuwa Raisi wa TAA toka iundwe mwaka 1948 hadi TANU inaasisiwa mwaka 1954...yeye alikuwa ni katibu tu, period. Ndiyo maana mimi nasema TAA ilizorota sana kwa kukosa uongozi baada ya uhamisho wa Raisi wake Dr. Vedasto Kyaruzi hadi inampata kiongozi mpya, Mwalimu Nyerere mwaka 1953.

CC: Nguruvi3
 
Back
Top Bottom