Lyatonga Mrema adaiwa kupora mke wa mtu

Acheni kumletea zengwe mzee wa watu

Wamuache atulie na mke wake

Ova
 
je angekua mtu kama Kimei au mtu mwenye pesa zake nyingi si wangeuana[emoji23]
 
Safi sana. Walichofanya hapa ni vizuri mno kumuacha afanye ambacho bado anaweza kukifanya hata kama inachukua muda kiduchu.

Katika Gerontology tunajifunza kitu inaitwa "Kumaintain na kustimulate autonomy"Yani Kumaintain zile capacity ambazo bado wazee wanaweza kufanya physically,mentally na socially.

Mtu anaweza kuinuka mwenyewe muache ainuke mwenyewe hata kama itachukuz dakika 5 kuituka.

Bahati nzuri uzee ni lazima kwa binadamu yeyote ambae atajaaliwa umri mrefu lazima huwa kuwa kuna diminuations katika autonomy hivyo inatakiwa Kumaintain capacity zinazobaki.
 
Miongoni mwa mafala ni huyo ndugu wa mke wa Mrema.

Ina maana katumwa na aliyekuwa mme wa huyo mama kulalamika kwa niaba yake?
 
Baadhi ya vitu vinavyoshusha hadhi magazeti ni Kama hivi.

Kwanini mmtafute ndugu wa karibu wakati wahusika wapo.


Huyo mme hawezi kuongea ?
 
Babu wa Kiraracha we faidi tu usisikilize maneno ya wanajamii.
 
Wabongo wanafiki na uchawi mwingi sana!walikua wapi?afu RAIA mwema nao waache habari za kishabiki

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Ndoa ya Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema imeibua utata na kusemekana kuwa ni batili kufuatia uwepo wa madai kuwa mwanamke aliyefunga nae ndoa, Doreen Kimbi, ni mke wa mtu.

Inasemekana kwamba katika hafla fupi iliyofanyika baada ya ndoa hiyo iliyofungwa katika Kijiji cha Kiraracha, Marangu, haikuhudhuriwa na ndugu wa damu wa Doreen, isipokuwa marafiki zake wachache.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema lililoripoti taarifa hiyo ni kwamba, ndugu wa karibu wa mwanamke huyo wamesema hawakupewa taarifa juu ya ndoa hiyo na wameshangazwa kuona picha za ndugu yao akila kiapo cha pili cha ndoa.

Taarifa zinadai kuwa Doreen alifunga ndoa na Fredrick Mushi katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme, Tabata mkoani Dar es Salaam na kujaaliwa mtoto mmoja, na baadaye kushindwa kuendelea na maisha ya ndoa baada ya kudaiwa kuwa mumewe aliondolewa kazini na kushindwa kuihudumia vyema familia yake.

“Mwaka 2019 mwanamke baada ya kuona kuwa ndiye anayemlea mume, akamkimbia na kwenda kuishi Moshi ambako alifungua biashara ya maua na upishi, hizo biashara zingine alizosema kwa kweli hatuzifahamu,” alisema ndugu huyo.

Kwa mujibu wa ndugu wa Doreen, wanasema wameshangazwa juu ya kauli ya Mrema kuwa alifika nyumbani na kukubaliana kuhusu mahari bila wazazi, kaka na dada zake kujua chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…