Lyatonga Mrema adaiwa kupora mke wa mtu

Lyatonga Mrema adaiwa kupora mke wa mtu

Uzi tayari
Umefukua kaburi chief[emoji44]
IMG_20220414_104308.jpg
 
Ina maaana Mrema na ushushu wake hakufanya due dilligence?

Sasa mbona anadaiwa kupora mke wa mtu?

👇

Ndoa ya Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema imeibua utata na kusemekana kuwa ni batili kufuatia uwepo wa madai kuwa mwanamke aliyefunga nae ndoa, Doreen Kimbi, ni mke wa mtu.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, ndugu wa karibu wa mwanamke huyo amesema hawakupewa taarifa juu ya ndoa hiyo na wameshangazwa kuona picha za ndugu yao akila kiapo cha pili cha ndoa.

Taarifa zinaeleza kuwa Doreen alifunga ndoa na Fredrick Mushi katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme, Tabata mkoani Dar es Salaam na kujaaliwa mtoto mmoja, na baadaye kushindwa kuendelea na maisha ya ndoa baada ya kudaiwa kuwa mumewe aliondolewa kazini na kushindwa kuihudumia vema familia yake.

“Mwaka 2019 mwanamke baada ya kuona kuwa ndiye anayemlea mume, akamkimbia na kwenda kuishi Moshi ambako alifungua biashara ya maua na upishi, hizo biashara zingine alizosema kwa kweli hatuzifahamu,” alisema ndugu huyo.

Hata hivyo ameendelea kueleza kuwa wanashindwa kuelewa lengo la ndugu yao kuolewa na Mrema, hasa ikizingatiwa kuwa bado hajaachana rasmi na mumewe wa awali kwa mujibu wa taratibu za kanisa.

Kwa mujibu wa ndugu wa Doreen, wanasema wameshangazwa juu ya kauli ya Mrema kuwa alifika nyumbani na kukubaliana kuhusu mahari bila wazazi, kaka na dada zake kujua chochote.

“Hilo la mahari hatujui nani kapokea, kwa sababu huyu ni ndugu yetu lazima tujitokeze kushiriki na kufahamu taratibu gani zimefuatwa kuvunja ndoa yake ya kwanza.

Hatujawahi kusikia wala kuhisi kuwa ndugu yetu ataolewa mara ya pili maana alikuwa na uhusiano wa karibu na mumewe wa kwanza,” ameeleza mwanafamilia.

Hata hivyo inaelezwa kuwa katika hafla fupi iliyofanyika baada ya ndoa hiyo iliyofungwa katika Kijiji cha Kiraracha, Marangu, haikuhudhuriwa na ndugu wa damu wa Doreen, isipokuwa marafiki zake wachache.
Watoto wa Mrema waende mahakamani kunullfy hii ndoa. Doreen alifunga ndoa mpya wakati ana ndoa tayari na Mr Mushi.
 
Watoto wa Mrema waende mahakamani kunullfy hii ndoa. Doreen alifunga ndoa mpya wakati ana ndoa tayari na Mr Mushi.

Tatizo watu wa nje tunapenda kuongea kwa kuhisi. Mambo ya ndoa ni siri ya wanandoa. Si ajabu divorce ipo.

Hata kwa Jack watu walisemaga hivi hivi kwamba Mengi ana ndoa halali na mke wa kwanza. Ndoa ya Jack ni ndoa batili.

Juzi ndio Ukweli ukajulikana kwamba Mengi alikuwa na divorce na mke mkubwa na ndoa ya Jack ni ndoa halali.
 
Tatizo watu wa nje tunapenda kuongea kwa kuhisi. Mambo ya ndoa ni siri ya wanandoa. Si ajabu divorce ipo.

Hata kwa jack watu walisemaga hivi hivi kwamba mengi ana ndoa halali na mke wa kwanza. Ndoa ya jack ni ndoa batili

Juzi ndio Ukweli ukajulikana kwamba mengi alikuwa na divorce na mke mkubwa na ndoa ya jack ni ndoa halali
Ya Mengi divorce ya nje ya mahakama inamaanisha nini? Hata Mengi alikuwa hajamtaliki mkewe though aliomba divorce. Kuna kitu hapa wewe subiri utaona.
 
Ya Mengi divorce ya nje ya mahakama inamaanisha nini ?Hata Mengi alikuwa hajamtaliki mkewe though aliomba divorce. Kuna kitu hapa wewe subiri utaona.
Ya Mengi divorce ya nje ya mahakama inamaanisha nini ?Hata Mengi alikuwa hajamtaliki mkewe though aliomba divorce. Kuna kitu hapa wewe subiri utaona.

Mahakama ya wilaya ya Kinondoni ilivunja ndoa ya kwanza ya Mengi mwaka 2015. Mahakama ilitoa hati ya talaka.
 
Mahakama ya wilaya ya kinondoni ilivunja ndoa ya kwanza ya Mengi mwaka 2015. Mahakama ilitoa hati ya talaka
20220829_121745.jpg

Ukisoma kwa undani hapo kuna kitu. Any way tusubiri. Pia kwani Jack na Mengi walifunga ndoa lini ?
 
View attachment 2338340
Ukisoma kwa undani hapo kuna kitu. Any way tusubiri. Pia kwani Jack na Mengi walifunga ndoa lini ?

Haijalishi walifunga ndoa lini. Lakini serikali na kanisa la KKKT ambalo mengi alikuwa muumini linaitambua ndoa ya Jack na Mengi..

Sasa kama kanisa linatambua. Na serikali inatambua.. mwingine ni nani aseme sio ndoa halali. Wakati Taasisi zote zinaitambua.

Ni sheria gani ya ndoa inayosema ndoa ya jack na mengi sio halali.. maana ndoa ni mkataba wa kisheria.. sheria ya ndoa inapinga wapi ?
 
We hakuna narudia Tena hakuna kanisa lolote la kkkt linalotambua ndoa ya mengi na jack!

Km walikuwa wanatambua ungeona wamefunga hapa nyumbani baada ya kutoka kufunga huko nje ya nchi!

Roman, Lutheran (kkkt), Anglican....
Hawavunji ndoa,watakushauri,watakuzungusha wee mpk utachoka....
Ndoa zinavunjwa mahamani na kanisa halihusiki kabisa!
Ndo maana hata km una divorce ya mahakamani Romani, kkkt hufungi ndoa unless otherwise "PESA" itumike Kwa baadhi ya wachungaji wajinga wajinga...
 
Back
Top Bottom