Lyatonga Mrema adaiwa kupora mke wa mtu

Lyatonga Mrema adaiwa kupora mke wa mtu

Ndoa ya Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema imeibua utata na kusemekana kuwa ni batili kufuatia uwepo wa madai kuwa mwanamke aliyefunga nae ndoa, Doreen Kimbi, ni mke wa mtu.
Inasemekana kwamba katika hafla fupi iliyofanyika baada ya ndoa hiyo iliyofungwa katika Kijiji cha Kiraracha, Marangu, haikuhudhuriwa na ndugu wa
kuishi Moshi ambako alifungua biashara ya maua na upishi, hizo biashara zingine alizosema kwa kweli hatuzifahamu,” alisema ndugu huyo.
Acheni Wivu
 
1648457425633.png
 
Ina maaana Mrema na ushushu wake hakufanya due dilligence?

Sasa mbona anadaiwa kupora mke wa mtu?

[emoji116]

Ndoa ya Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema imeibua utata na kusemekana kuwa ni batili kufuatia uwepo wa madai kuwa mwanamke aliyefunga nae ndoa, Doreen Kimbi, ni mke wa mtu.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, ndugu wa karibu wa mwanamke huyo amesema hawakupewa taarifa juu ya ndoa hiyo na wameshangazwa kuona picha za ndugu yao akila kiapo cha pili cha ndoa.

Taarifa zinaeleza kuwa Doreen alifunga ndoa na Fredrick Mushi katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme, Tabata mkoani Dar es Salaam na kujaaliwa mtoto mmoja, na baadaye kushindwa kuendelea na maisha ya ndoa baada ya kudaiwa kuwa mumewe aliondolewa kazini na kushindwa kuihudumia vema familia yake.

“Mwaka 2019 mwanamke baada ya kuona kuwa ndiye anayemlea mume, akamkimbia na kwenda kuishi Moshi ambako alifungua biashara ya maua na upishi, hizo biashara zingine alizosema kwa kweli hatuzifahamu,” alisema ndugu huyo.

Hata hivyo ameendelea kueleza kuwa wanashindwa kuelewa lengo la ndugu yao kuolewa na Mrema, hasa ikizingatiwa kuwa bado hajaachana rasmi na mumewe wa awali kwa mujibu wa taratibu za kanisa.

Kwa mujibu wa ndugu wa Doreen, wanasema wameshangazwa juu ya kauli ya Mrema kuwa alifika nyumbani na kukubaliana kuhusu mahari bila wazazi, kaka na dada zake kujua chochote.

“Hilo la mahari hatujui nani kapokea, kwa sababu huyu ni ndugu yetu lazima tujitokeze kushiriki na kufahamu taratibu gani zimefuatwa kuvunja ndoa yake ya kwanza.

Hatujawahi kusikia wala kuhisi kuwa ndugu yetu ataolewa mara ya pili maana alikuwa na uhusiano wa karibu na mumewe wa kwanza,” ameeleza mwanafamilia.

Hata hivyo inaelezwa kuwa katika hafla fupi iliyofanyika baada ya ndoa hiyo iliyofungwa katika Kijiji cha Kiraracha, Marangu, haikuhudhuriwa na ndugu wa damu wa Doreen, isipokuwa marafiki zake wachache.
Huyo anaesema ndoa ni batili kauli yake ndo batili.

Mrema hakufunga ndoa kwa siri, ilitangazwa mara kadhaa na hakuna pingamizi lililowekwa kabla na hata wakati wa kufungwa ndoa kanisani.

Huyo ndg yake Doreen ni marioo atakuwa alikuwa analishwa na dada yake sasa imefika mwisho atafute za kwake
 
Hapa ndio unaona ndugu katika familia zetu za kimaskini walivyo wapumbavu. Yani kwenye familia kuna watu wamekaa baki wanaangalia nani kafanya nini ili waibuke huko mafichoni walipo na kuongea blah blah, na kusema wao ndio ndugu wa flani,
Nina uhakika kama angefunga ndoa na choka mbaya hakuna ndugu ambaye angejitokeza , sasa huyo ni Mrema tu, je angekua mtu kama Kimei au mtu mwenye pesa zake nyingi si wangeuana
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee mrema figisu haachagi usikute yeye ndo alimtoa kwenye ndoa fanya mume wamtu afukuzwe kazi
Hivi aliyekuwa polisi ni huyu mama au mumewe?... maana kama alifumaniwa huko polisi ina maana huyu mama ni balaa.

Na wakati huo Mrema alikuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Ile miwani nyeusi badala ya shela ilikuwa inaficha jambo lililopo nyuma ya pazia.

Ila huyo mme wa zamani sii kwamba hakuwa anajua kinachoendelea hapana!

Atakua alijua kila kitu ila kelele za sasa ni uthibitisho kwa dunia kutia muhuri wa kuachana kwao.
 
Ina maaana Mrema na ushushu wake hakufanya due dilligence?

Sasa mbona anadaiwa kupora mke wa mtu?

👇

Ndoa ya Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema imeibua utata na kusemekana kuwa ni batili kufuatia uwepo wa madai kuwa mwanamke aliyefunga nae ndoa, Doreen Kimbi, ni mke wa mtu.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, ndugu wa karibu wa mwanamke huyo amesema hawakupewa taarifa juu ya ndoa hiyo na wameshangazwa kuona picha za ndugu yao akila kiapo cha pili cha ndoa.

Taarifa zinaeleza kuwa Doreen alifunga ndoa na Fredrick Mushi katika Kanisa Katoliki la Kristu Mfalme, Tabata mkoani Dar es Salaam na kujaaliwa mtoto mmoja, na baadaye kushindwa kuendelea na maisha ya ndoa baada ya kudaiwa kuwa mumewe aliondolewa kazini na kushindwa kuihudumia vema familia yake.

“Mwaka 2019 mwanamke baada ya kuona kuwa ndiye anayemlea mume, akamkimbia na kwenda kuishi Moshi ambako alifungua biashara ya maua na upishi, hizo biashara zingine alizosema kwa kweli hatuzifahamu,” alisema ndugu huyo.

Hata hivyo ameendelea kueleza kuwa wanashindwa kuelewa lengo la ndugu yao kuolewa na Mrema, hasa ikizingatiwa kuwa bado hajaachana rasmi na mumewe wa awali kwa mujibu wa taratibu za kanisa.

Kwa mujibu wa ndugu wa Doreen, wanasema wameshangazwa juu ya kauli ya Mrema kuwa alifika nyumbani na kukubaliana kuhusu mahari bila wazazi, kaka na dada zake kujua chochote.

“Hilo la mahari hatujui nani kapokea, kwa sababu huyu ni ndugu yetu lazima tujitokeze kushiriki na kufahamu taratibu gani zimefuatwa kuvunja ndoa yake ya kwanza.

Hatujawahi kusikia wala kuhisi kuwa ndugu yetu ataolewa mara ya pili maana alikuwa na uhusiano wa karibu na mumewe wa kwanza,” ameeleza mwanafamilia.

Hata hivyo inaelezwa kuwa katika hafla fupi iliyofanyika baada ya ndoa hiyo iliyofungwa katika Kijiji cha Kiraracha, Marangu, haikuhudhuriwa na ndugu wa damu wa Doreen, isipokuwa marafiki zake wachache.
Dada mmbea wewe
 
Back
Top Bottom