HUKU M23 wakiendelea na maandamano kuelekea Kinshasa baada ya kupiga hodi leo mjini Bukavu, rais Felix Tshisekedi asafiri kwenda Ulaya ..
13 February 2025
Munich, Germany
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aibuka nchini Germany katika mji wa Munich na kuwepo katika jopo la kuzungumzia usalama dunia
EXCUSIVE - HOTUBA YA RAIS FÉLIX TSHISEKEDI KATIKA MKUTANO WA MUNICH GERMANY KUHUSU USALAMA
View: https://m.youtube.com/watch?v=H5IHTTO3zfM
Rais Felix Tshisekedi watu 7,000,000 wamekuwa wakimbizi wa ndani katika Kongo kutokana na vitendo vya nchi ya Rwanda ...
wana jopo walaumu wadau wakubwa kama UN, EU, Marekani, China wanawajibu gani katika kuleta amani duniani lakin tunao hali hiyo ya wakubwa kushiriki kidakindaki kuleta amani dunia wakubwa hao wanasitasita...
Mwanajopo rais Mahama wa Ghana ahojiwa nguvu ya SADC, ECA, ECOWAS, Peacekeeping Forces na kusema kuna mazingira matumizi ya nguvu ya bunduki na mabomu inayotumiwa na serikali iliyopo madarakani hayaweza kutatua mzozo bali mazungumzo ndiyo njia sahihi ...
Felix Tshisekedi alaumu undumakuwili na unafiki wa jumuiya ya kimataifa inapotokea nchi moja kuvamiwa na nchi jirani, tunaona jumuiya ya kimataifa inaamua tofauti kwa mazingira yaleyale kwa nchi tofauti ikivamiwa, mfano Kongo kuvamiwa hatuoni Jumuiya ya Kimataifa na kikanda wakichukua hatua stahiki... hii ni hatari kwa usalama na raia wanaoathirika na nchi yao kuvamiwa...
Naye waziri wa ulinzi wa Rwanda mheshimiwa Marizamunda Juvenal asema nchi yake haifadiki na kinachoendelea nchi Congo, bali inataka kuona amani inapatikana Congo ili nchi zote kufaidika na biashara za kuvuka mipaka baina ya nchi hizo jirani ..
Bi. Kimani wa Kenya akamuuliza kwanini
Rais Felix Tshisekedi haziamini taasisi za kikanda kama AU, SADC, EAC hivi karibuni kwa kutohudhuria mikutano kama wa Dar es Salaam 8 February 2025 na ule wa Umoja wa Afrika AU unaoendelea 15 February 2025 mjini Addis Ababa, je kususa kuhudhuria hakuondoi fursa ya kuleta Amani kwa njia ya mazungumzo kufanikiwa
Mheshimiwa
Rais Felix Tshisekedi leo tarehe 14 February 2025 kuna taarifa mji wa Bukavu ulipo nchini kwako, je una lakutuambia hali hiyo mpya nchini mwako ?