Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

"Ficha vyanzo vyako vya mapato. Waonyeshe matumizi."

Usiwe mwepesi wa kutoa toa misaada wakati bado uchumi wako haujakaa sawa,kwasababu hao unaowasaidia hawatakusaidia siku ukiyumba kiuchumi.

Usimuamini mtu kupita kiasi hata kama ni ndugu yako maana adui wa mtu ni wa nyumbani mwake mwenyewe.

Nakupa mfano. Kuna watu walitafuta taarifa zangu lakini wakazikosa, baadaye nikawa ninaona baadhi zinavuja, nikafuatilia na kugundua kumbe ndugu yangu ndiye anayezitoa, kuchimba zaidi nikajua huwa wanamlewesha sana kwasababu udhaifu wake uko kwenye pombe,kila akiulizwa swali anajibu kama anavyolijua.

Nilivyojua nikawa nampa za kawaida sana,kisha nikamuhamisha mkoa,huko aliko hawamjui na wala hajui kinachoendelea huku kwangu.

Kuwa makini na vyakula unavyokula hasa vya kupikiwa kibinafsi,kutengewa chakula chako mwenyewe wakati mpo wengi.

Kuweni wasiri wa mambo yenu,mishe zenu,michongo yenu,kazi zenu.

Mtu akikuuliza unafanya kazi wapi,na wewe muulize natafuta kazi ,vipi huko kwako naweza kupata nafasi?

Wengi ni 'masnitch' msiwaamini kazi yao ni kuharibia wengine.

Ukifanikiwa usiwasahau wazazi,watoto yatima,masikini ,wajane,ndugu na Mungu.
 
Huu nilisha usoma, ni uzi mzuri mno.
 
point no.6
kuwa na demu mmoja utateseka sana.
 
🀣🀣🀣 umeona sio mbaya kumsaidia Rais wako, mi nilikuita ili uje uone ninavyo mgaragaza.
Kamwe siwezi kuwa chini ya raisi mjinga, wewe ukiona kuna raisi wangu kakugaragaza mpaka ukaniita mimi , jua kwanza haunizidi kwa chochote ,naongelea mpka nguvu za kiume , na huwa nikijibu nimekuonea huruma tuπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
haunizidi kwa chochote ,naongelea mpka nguvu za kiume , na huwa nikijibu nimekuonea huruma tuπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
🀣🀣🀣 majoblesi mtabaki hivyo daima yaani tunaongea kuhusu hela wewe unawaza ngono!
Haya hizo nguvu za kiume zinakuingizia pesa kiasi gani kwa dakika?
 
Usikubali lawama/kuumizwa na maneno yoyote ya manung'uniko kuwanyima watu hela ambao ukipata shida hawana msaada zaidi ya neno pole, hasa wanawake

Kingine hela haitumwi, inafuatwa.
Tatu, Hakikisha matumizi yako hayazidi kipato chako.
Ndugu zako ndio watu wako wa karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…