Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

NullPointer

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
3,461
Reaction score
2,273
Sina access na jukwaa la dini sasa nmeona nitupie huku kwenye Intelligence.
Kuna some parts hua zinanivunja imani muda mwingine nikisoma kwenye bible which is actually a bad thing, sasa leo hili fungu limenichanganya akili

[h=1]Deuteronomy 22:28-29New International Version (NIV)[/h]28 If a man happens to meet a virgin who is not pledged to be married and rapes her and they are discovered, 29 he shall pay her father fifty shekels[a] of silver. He must marry the young woman, for he has violated her. He can never divorce her as long as he lives

Ni wazi kabisa fungu linasema kua mwanaume akikutwa kambaka binti ambaye ni bikra basi atamlipa baba yake huyo mwanamke vipande vya silver alafu atatakiwa kumuoa na hatotakiwa kumpa talaka maisha yake yote.. Sasa hili fungu linachonichanganya, kwa nini mwanamke wa atu abakwe afu tena biblia itake aoane na huyohuyo aliyembaka, si ni mateso hayo ambayo binti hakujitakia, yani anakua kama analipa kosa ambalo hakulifanya tena for life? This is cruel! em nisaideni niondoe mashaka yangu..

Afu kama huna la maana la kuongea usijibu, i dont wish to see watu wanaanza kusema dini yao ndo ya kweli blah blah blah.. ulizaliwa tu huko usiwe mpiga kelele sana
 
Mimi nikupe kwa kifupi mno! watu wengi wanachanganya sana haya mambo ya ki biblia.
Biblia imegawanyika mara mbili. kuna agano la kale ambalo lilihusu waisraeli tu! na kuna agano jipya ambalo linahusu kila mtu katika ulimwengu huu.

Labda unambie kuwa wewe ni mu israel na unaishi kabla ya yesu kuleta agano la pili(jipya). Vinginevyo hizi sheria ambazo sisi hatupo tena chini yake ziliwafaa sana waisraeli kwa wakati huo!

Si hiyo tu uliyoisema bali zipo nyingi tu ambazo hazifai na hazitekelezeki kwa sasa. Ndio maana Mungu alisema wazi kuwa "siku zinakuja nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Yuda. Si kama lile nililofa na baba zao wakalivunja........." Hivyo ndugu yangu hizo sheria na agano la kale kwa ujumla kwa sasa zisome kama story tu.
 
mimi naamini kuwa Mungu alikuwa anakutana na Waisrael kulingana na mazingira, tamaduni, nyakati, uwezo wa ufahamu nk. sisi tunaoishi kipindi cha leo tunaweza kushangaa mambo mengi sana yaliyokua yanaendelea wakati huo na unaweza kuhisi na kumshangaa Mungu .. mfano mzuri kwa sisi wakristo tunaamini katika ndoa moja lakini enzi hizo (agano la kale) walikua wanaoa wake wengi hata wafalme maarufu walikuwa na wake wengi ( akina daud, sulemani nk) na Mungu hakuonyesha kujali sana... vitu vingine alikuwa anawaachia tu kwa sababu ya huruma zake

tukirudi kwenye mada naamini kuwa kulingana na tamaduni za Israel na jinsi walivyo watreat wanawake (Wasomi wanasema kizazi hicho walikuwa wanawachukulia wanawake kuwa wanaakili kidogo kuliko ng'ombe) hiyo sheria ilikua ni msaada sana kwao... kwa jinsi unavyomchukulia mwanamke husika unadhani alikua anaamua nani wa kumuoa au kuishi nae? jamii haikumpa nafasi hiyo au uhuru huo... ilikuwa ni kawaida mwanamme akambaka binti bikira alafu labda akalipa fine tu kwa wazazi husika then ikaishia hapo... kumbuka pia kuwa enzi hizo ilikuwa haiwezekani kumuoa mwanamke ambae sio bikira kwa nanma yoyote ile kwa hiyo huyo mwanamke ndo imeishia hapo HAOLEWI TENA MAISHA YAKE YOTE..

suala kuwa wanawake wanakubali/wanachagua/au wanajisikiaje nani amuoe lilikua halipo na sio la kujadiliwa.. baba na ndugu zake wa kiume ndo wanakubaliana na familia ya muoaji kwa maslah yao.. na ukifiwa na mme wako unachukuliwa na ndugu wa mume SI WEWE unayeamua. kwa hiyo hiyo amri ya Mungu kwao ilikuwa inawafavour sana wanawake wa kipindi hicho na waliona wamekombolewa...
 
me nikupe kwa kifupi mno! watu wengi wanachanganya sana haya mambo ya ki biblia.
Biblia imegawanyika mara mbili. kuna agano la kale ambalo lilihusu waisraeli tu! na kuna agano jipya ambalo linahusu kila mtu katika ulimwengu huu.
labda unambie kuwa wewe ni mu israel na unaishi kabla ya yesu kuleta agano la pili(jipya). Vinginevyo hizi sheria ambazo sisi hatupo tena chini yake ziliwafaa sana waisraeli kwa wakati huo!
si hiyo tu uliyoisema bali zipo nyingi tu ambazo hazifai na hazitekelezeki kwa sasa. Ndio maana Mungu alisema wazi kuwa "siku zinakuja nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Yuda. Si kama lile nililofa na baba zao wakalivunja........." Hivyo ndugu yangu hizo sheria na agano la kale kwa ujumla kwa sasa zisome kama story tu.

Wewe una kichwa kigumu kuelewa, mleta mada anata kujua sababu iliyopelekea agizo hilo likatolewa na sio suala la agano la kale au jipya.
Halafu wewe unajua maana ya agano au unafuata tu waandishi wa biblia walichokisema? Tuchukulie kuwa ni kweli agano la kale halikuwa kamilifu kama ulivyomaanisha, je mwanamke wa enzi za agano la kale alipokuwa akibakwa hasikii maumivu tofauti na mwanamke wa sasa? Au unataka kusema kuwa mungu alikuwa mkatili kipindi cha agano la kale kwa kuwakandamiza watu kwa sheria kali?
 
Sina access na jukwaa la dini sasa nmeona nitupie huku kwenye Intelligence.
Kuna some parts hua zinanivunja imani muda mwingine nikisoma kwenye bible which is actually a bad thing, sasa leo hili fungu limenichanganya akili

Deuteronomy 22:28-29New International Version (NIV)

28 If a man happens to meet a virgin who is not pledged to be married and rapes her and they are discovered,29 he shall pay her father fifty shekels[a] of silver. He must marry the young woman, for he has violated her. He can never divorce her as long as he lives

Hayo yalikua maagizo waliyopewa wana wa Israeli wakati huo.
Mengine kati ya hayo yalibadilishwa baada ya Yesu Kristo kuja.
Mfano ni agizo la kutoa sadaka ya kuteketezwa ya wanyama, agizo la kutoa adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa, agizo la kutofanya kazi siku ya sabato, n.k.
Yesu Kristo ndio kielelezo chetu, na maagizo yake ndio tunayoyafuata.
Yesu Kristo aliendeleza baadhia ya maagizo ya agano la kale, na kubadilisha maagizo mengine.
 
mimi naamini kuwa Mungu alikuwa anakutana na Waisrael kulingana na mazingira, tamaduni, nyakati, uwezo wa ufahamu nk. sisi tunaoishi kipindi cha leo tunaweza kushangaa mambo mengi sana yaliyokua yanaendelea wakati huo na unaweza kuhisi na kumshangaa Mungu .. mfano mzuri kwa sisi wakristo tunaamini katika ndoa moja lakini enzi hizo (agano la kale) walikua wanaoa wake wengi hata wafalme maarufu walikuwa na wake wengi ( akina daud, sulemani nk) na Mungu hakuonyesha kujali sana... vitu vingine alikuwa anawaachia tu kwa sababu ya huruma zake

tukirudi kwenye mada naamini kuwa kulingana na tamaduni za Israel na jinsi walivyo watreat wanawake (Wasomi wanasema kizazi hicho walikuwa wanawachukulia wanawake kuwa wanaakili kidogo kuliko ng'ombe) hiyo sheria ilikua ni msaada sana kwao... kwa jinsi unavyomchukulia mwanamke husika unadhani alikua anaamua nani wa kumuoa au kuishi nae? jamii haikumpa nafasi hiyo au uhuru huo... ilikuwa ni kawaida mwanamme akambaka binti bikira alafu labda akalipa fine tu kwa wazazi husika then ikaishia hapo... kumbuka pia kuwa enzi hizo ilikuwa haiwezekani kumuoa mwanamke ambae sio bikira kwa nanma yoyote ile kwa hiyo huyo mwanamke ndo imeishia hapo HAOLEWI TENA MAISHA YAKE YOTE..

suala kuwa wanawake wanakubali/wanachagua/au wanajisikiaje nani amuoe lilikua halipo na sio la kujadiliwa.. baba na ndugu zake wa kiume ndo wanakubaliana na familia ya muoaji kwa maslah yao.. na ukifiwa na mme wako unachukuliwa na ndugu wa mume SI WEWE unayeamua. kwa hiyo hiyo amri ya Mungu kwao ilikuwa inawafavour sana wanawake wa kipindi hicho na waliona wamekombolewa...

ridhaa ilikuwepo. unakumbuka wakati isaka anatafutiwa mke? rebecca aliulizwa utakwenda na mtu huyu? naye akasema nitakwenda
 
naamini kuwa Mungu alikuwa anakutana na Waisrael kulingana na mazingira, tamaduni, nyakati, uwezo wa ufahamu nk. sisi tunaoishi kipindi cha leo tunaweza kushangaa mambo mengi sana yaliyokua yanaendelea wakati huo na unaweza kuhisi na kumshangaa Mungu .. mfano mzuri kwa sisi wakristo tunaamini katika ndoa moja lakini enzi hizo (agano la kale) walikua wanaoa wake wengi hata wafalme maarufu walikuwa na wake wengi ( akina daud, sulemani nk) na Mungu hakuonyesha kujali sana... vitu vingine alikuwa anawaachia tu kwa sababu ya huruma zake

ndugu suala la wakristo kua na ndoa ya mke mmoja .lililetwa na warumi.wakati ule dola yao ilipokua na nguvu.na uamuzi huo ulitawaliwa na husia binafsi.
tukurudi kwenye mada.kizazi hiki kinafata maagizo ya agano jipya.
 
Sina access na jukwaa la dini sasa nmeona nitupie huku kwenye Intelligence.
Kuna some parts hua zinanivunja imani muda mwingine nikisoma kwenye bible which is actually a bad thing, sasa leo hili fungu limenichanganya akili

Deuteronomy 22:28-29New International Version (NIV)

28 If a man happens to meet a virgin who is not pledged to be married and rapes her and they are discovered,29 he shall pay her father fifty shekels[a] of silver. He must marry the young woman, for he has violated her. He can never divorce her as long as he lives

Ni wazi kabisa fungu linasema kua mwanaume akikutwa kambaka binti ambaye ni bikra basi atamlipa baba yake huyo mwanamke vipande vya silver alafu atatakiwa kumuoa na hatotakiwa kumpa talaka maisha yake yote.. Sasa hili fungu linachonichanganya, kwa nini mwanamke wa atu abakwe afu tena biblia itake aoane na huyohuyo aliyembaka, si ni mateso hayo ambayo binti hakujitakia, yani anakua kama analipa kosa ambalo hakulifanya tena for life? This is cruel! em nisaideni niondoe mashaka yangu..

Afu kama huna la maana la kuongea usijibu, i dont wish to see watu wanaanza kusema dini yao ndo ya kweli blah blah blah.. ulizaliwa tu huko usiwe mpiga kelele sana

Ndio maana wengine tukisoma vitu kama hivyo huwa tunashangaa Biblia kuitwa kitabu kitakatifu.
 
ridhaa ilikuwepo. unakumbuka wakati isaka anatafutiwa mke? rebecca aliulizwa utakwenda na mtu huyu? naye akasema nitakwenda

Mkuu nazungumzia taifa la Israel na tamadumi/mila zao... kipindi cha rebeca hakukuwa na kitu kinaitwa Israel...
 
ndugu suala la wakristo kua na ndoa ya mke mmoja .lililetwa na warumi.wakati ule dola yao ilipokua na nguvu.na uamuzi huo ulitawaliwa na husia binafsi.
tukurudi kwenye mada.kizazi hiki kinafata maagizo ya agano jipya.[/QUOTE]

si kweli kwani dola la kirumi lilikua na nguvu kipindi cha Yesu.. wakati huo ndoa za mke zaidi ya mmoja lilishakuwepo toka zamani sana... mf Daudi alikua na wake wengi na kipindi hicho hakukua na kitu kinaitwa dola la kirumi..
 
ridhaa ilikuwepo. unakumbuka wakati isaka anatafutiwa mke? rebecca aliulizwa utakwenda na mtu huyu? naye akasema nitakwenda
Sikuhizi wanarudi wenyewe mwaya,, tenawanamsemo kukosea wakatiwa kwenda kurudi wanarudiwenyewe tufanyeje tukirudi turudi wotee??
 
Nuru ni matendo Mema na Ethics za kufuata matendo ya MUNGU while giza ni matendo maovo na yakudhoofisha watu wengine..?kwa maana hii Wema na ubaya haviwezi kulandana hata kidogo.
 
acha uwongo hicho kifungu umekisomea hapa tu.. hujawahi soma biblia wewe..

Acha kutoa povu la moto! Umejuaje kama sijawahi kusoma Biblia? Hata kama sijawahi kusoma hiyo verse peke yake inaondoa merit ya Biblia kuwa na utakatifu!
 
Mkuu nazungumzia taifa la Israel na tamadumi/mila zao... kipindi cha rebeca hakukuwa na kitu kinaitwa Israel...
Sawa nimekupata. Israel ilianzia kwa Yakobo, lakini unataka kuniambia kuwa ustaarabu ulikuwa ukipungua kadiri walivyokuwa karibu na Mungu? Si kweli. Hawakuwa punguani kiasi hicho japo ukisoma Kumbukumbu unaona ni jinsi gani walikuwa na akili ngumu
 
... kumbuka pia kuwa enzi hizo ilikuwa haiwezekani kumuoa mwanamke ambae sio bikira kwa nanma yoyote ile kwa hiyo huyo mwanamke ndo imeishia hapo HAOLEWI TENA MAISHA YAKE YOTE..

Nimependa hapo niseme tu kidogo, hapana agano kufanyika pasipo DAMU kumwagika. Ndoa ni agano ndio maana bikra ilihusika kutoa damu ili agano likamilike...by those days.

Ila sasa hakuna bikra na watu wanao kama kawaida, si kama damu haipo katika maagano ya siku hizi lah hasha tunao soma maandiko na kuamini NENO twaamini pia ile Damu aliyomwagika pale msalani ndio twaitumia ama kuihusisha na maagano yote na ndoa ikiwemo.
 
HAOLEWI TENA MAISHA YAKE YOTE[/B]..
...

Nimependa hapo niseme tu kidogo, hapana agano kufanyika pasipo DAMU kumwagika. Ndoa ni agano ndio maana bikra ilihusika kitoa damu ili agano likamilike...by those days.

Ila sasa hakuna bikra na watu wanao kama kawaida, si kama damu haipo katika maagano ya siku hizi lah hasha tunao soma maandiko na kuamini NENO twaamini pia ile Damu aliyomwagika pale msalani ndio twaitumia ama kuihusisha na maagano yote na ndoa ikiwemo.
 
Hapo nafikiri hizo sheria zilikuwa si kamkandamiza mwanamke pamoja na kutendewa hayo. Ila ilikuwa nikutoa nafasi ya mwanamke kuolewa maana katika sheria zao pasipo bikra/bikira hakuna ndoa...hivyi mwanamke aliyebakwa asingeweza kuolewa tena ndio maana pakawepo na sheria ya huyo mbakaji amwoe huyo aliyebakwa na kutolewa bikira na mbakaji.

Jaribu kurejea kisa katika familia ya Mfalme Daudi, Mtoto wa Daudi alimpenda Tamari/Tamali akaamua kumbaka. Ikaleta shida kiasi ila shida kubwa ilikuja pale Tamari sijui Tamali alipomwambia mbakaji ni vyema amchukue kuwa mke wake. Jamaa alikataa ndio shida ilipoanza nenda kasome utaona vyema...
Hapo huyo binti alijua kwamba ndio biashara yake imekwisha asipoolewa na mbakaji.

Hili ndio wazo kuu la sheria hizo wakati huo lakini.
 
Acha kutoa povu la moto! Umejuaje kama sijawahi kusoma Biblia? Hata kama sijawahi kusoma hiyo verse peke yake inaondoa merit ya Biblia kuwa na utakatifu!

Ni vyema uliza wakati mwingine Biblia ni mkusanyiko wa vitabu wajua pana Maandiko na Neno.

Hata shetani pia hutumia hiyo hiyo Biblia kwa maana ya Maandiko ili apotoshe ukweli.

Pia fahamu pana
Sehemu ya Maisha ya Mwili imejitokeza sana Agano la kale na hasa zimetumika Tamaduni za Israel na makabila yake

Na pana Maisha ya kiroho hii utaipata zidi katika Agano jipya

Ndio maana walipo sikia mfalme amezaliwa iliwapashida sana...kumbe si ufalme wa Dunia hii kwa maana ya mwili.

Mtoa maada amepost andiko lijadiliwe, kama lilivyo na si vinginevyo kama alivyotanabaisha mtoa maada.
 
Back
Top Bottom