Mkuu hakubadilisha kitu. Yeye mwenyewe alisema hakuja kutengua torati bali amekuja kuikamilisha. Yeye alitoa amri moja tu nayo ni UPENDO. Upendo ukitawala mtu hawezzi kumfanyia mwenzie kitu kiovu yaani huwezi kutenda dhambi. Yesu aliona unafiki wa wa Israeli wakati huo hivyo akasisitiza sana kuwa upendo utawale. Hata sasa upendo ukitawala watu hawtatenda dhambi. Hatutaua albino, hatutaiba, hatutazini nk.
Hayo yalikua maagizo waliyopewa wana wa Israeli wakati huo.
Mengine kati ya hayo yalibadilishwa baada ya Yesu Kristo kuja.
Mfano ni agizo la kutoa sadaka ya kuteketezwa ya wanyama, agizo la kutoa adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa, agizo la kutofanya kazi siku ya sabato, n.k.
Yesu Kristo ndio kielelezo chetu, na maagizo yake ndio tunayoyafuata.
Yesu Kristo aliendeleza baadhia ya maagizo ya agano la kale, na kubadilisha maagizo mengine.