Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

Usimuwekee Yesu Maneno mkuu. Yesu hakusema YEYE ndio aliruhusu kupitia Mussa. Tuwe makini tusilazimishe mambo.

[7] They say unto him, Why did Moses then command to give a writing of divorcement, and to put her away? [8] He saith unto them, Moses because of the hardness of your hearts suffered you to put away your wives: but from the beginning it was not

Nimeona ugumu WA mjadala kutokana na maelezo Kama haya. Yesu ni Mungu alikuwa anajua nini Musa alisema na kwanini wakati MUSA alikuwepo maelfu ya miaka nyuma.
Yesu ndiye alimtuma Musa kwa kuwa Musa alikuwa mjumbe WA Mungu
Yesu alijibu kadri alivyoulizwa na wale waliokuwa wanaita sheria ya Musa ulitaka aseme sio MUSA ni Mimi ndiyo uelewe yeye ndiye alikuwa nyuma ya Maamrisho ya Musa au kwa uelewa wako MUSA alikuwa na sheria zake mwenyewe ?
 
me nikupe kwa kifupi mno! watu wengi wanachanganya sana haya mambo ya ki biblia.
Biblia imegawanyika mara mbili. kuna agano la kale ambalo lilihusu waisraeli tu! na kuna agano jipya ambalo linahusu kila mtu katika ulimwengu huu.
labda unambie kuwa wewe ni mu israel na unaishi kabla ya yesu kuleta agano la pili(jipya). Vinginevyo hizi sheria ambazo sisi hatupo tena chini yake ziliwafaa sana waisraeli kwa wakati huo!
si hiyo tu uliyoisema bali zipo nyingi tu ambazo hazifai na hazitekelezeki kwa sasa. Ndio maana Mungu alisema wazi kuwa "siku zinakuja nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Yuda. Si kama lile nililofa na baba zao wakalivunja........." Hivyo ndugu yangu hizo sheria na agano la kale kwa ujumla kwa sasa zisome kama story tu.

Hujajibu swali
 
Kuhusu Agano,liliwekwa hata na Adamu Pia. halikuanzia kwa Ibrahim. Naona hausomi Biblia yak vizuri mkuu.

Nimekwambia ni agano la Ibrahim ndilo hilo lililokuja kwa uzao wake kupitia Yakobo / Israel.
Hilo la Adam naomba uliweke hapa na lilikuwa agano kuhusu nini ?
 
Ndio ni story moja tu, zingine zote zinaisupport hiyo hiyo moja.

Hata hayo mambo ya Neema, Upendo na matendo ni vikolombwezo tu. au wewe unaona sisi kujumuishwa ni jambo jipya sana? hiyo ilikuwa issue ya mpangilio wa muda wa Mungu Mwenyewe na sio kwamba kuna wakati wowote katika moyo wa Mungu amekwisha wahi kusema hawa sio wangu na hawa ni wangu. NEVER.

Mungu aliingia Agano hata na Adam pia, unasemaje sasa?

Ni NEVER kwa mtazamo wako. Kumbuka hata namna alivyokuwa anawaadhibu au kuwaamuru kuwapiga wengine wewe unasema wote walikuwa sawa machoni pa Mungu.
Huo usawa unausoma wapi ? Wakati imeandikwa...walipewa uwezo WA kufanyika wana....
Kama walikuwa ni wana tayari huu uwezo WA kufanyika ulitokana na nini ?
 
Nimeona ugumu WA mjadala kutokana na maelezo Kama haya. Yesu ni Mungu alikuwa anajua nini Musa alisema na kwanini wakati MUSA alikuwepo maelfu ya miaka nyuma.
Yesu ndiye alimtuma Musa kwa kuwa Musa alikuwa mjumbe WA Mungu
Yesu alijibu kadri alivyoulizwa na wale waliokuwa wanaita sheria ya Musa ulitaka aseme sio MUSA ni Mimi ndiyo uelewe yeye ndiye alikuwa nyuma ya Maamrisho ya Musa au kwa uelewa wako MUSA alikuwa na sheria zake mwenyewe ?

We vipi?

Kwa nini hautaki kukubaliana na kilichoandikwa kwenye Biblia aisee?

Au unataka kusema Yesu ni MNAFIKI? Kwamba alimpa Mussa maelekezo ambayo yeye mwenyewe anaogopa kuyasimamia hasa akikutana na changamoto?

kwanza hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia Yesu amepata kutumia neno Mimi, wakati wote alikuwa anasema Mungu,sasa alipatwa na kigugumizi gani kusema Maelekezo ya Divorce Mussa alipewa na Mungu kwa sababu Fulani Fulani?
 
Sina access na jukwaa la dini sasa nmeona nitupie huku kwenye Intelligence.
Kuna some parts hua zinanivunja imani muda mwingine nikisoma kwenye bible which is actually a bad thing, sasa leo hili fungu limenichanganya akili

Deuteronomy 22:28-29New International Version (NIV)

28 If a man happens to meet a virgin who is not pledged to be married and rapes her and they are discovered,29 he shall pay her father fifty shekels[a] of silver. He must marry the young woman, for he has violated her. He can never divorce her as long as he lives

Ni wazi kabisa fungu linasema kua mwanaume akikutwa kambaka binti ambaye ni bikra basi atamlipa baba yake huyo mwanamke vipande vya silver alafu atatakiwa kumuoa na hatotakiwa kumpa talaka maisha yake yote.. Sasa hili fungu linachonichanganya, kwa nini mwanamke wa atu abakwe afu tena biblia itake aoane na huyohuyo aliyembaka, si ni mateso hayo ambayo binti hakujitakia, yani anakua kama analipa kosa ambalo hakulifanya tena for life? This is cruel! em nisaideni niondoe mashaka yangu..

Afu kama huna la maana la kuongea usijibu, i dont wish to see watu wanaanza kusema dini yao ndo ya kweli blah blah blah.. ulizaliwa tu huko usiwe mpiga kelele sana

Biblia unaposoma ni tofauti na kitabu cha hadithi.......kuna busara ndani yake lazima utumie...! Hata Yesu alipozungumza kuna kipindi alikazia na kusema MWENYE MASIKIO NA ASIKIE......akimaanisha kuna ufahamu zaidi ya kusikiliza tu.....

Nikirudi kwenye swali lako....ni budi ujue kuna mambo mawili makubwa wakati wa Musa;
1. Kwanza kuna amri za MUNGU ambazo Musa alipokea kupitia mbao zile za mawe.....hizo ndizo amri kuu...ambazo Yesu alipokuja kuitimiliza torati ali-summarize kuwa mbili i.e. Mpende BWANA Mungu wako na pia mpende jirani yako kama nafsi yako.
2. Pili kuna amri za Musa....! Ukumbuke wakati wana wa Israel wakitoka Misri ca. 600,000 people lilikuwa ni taifa tayari lakini watu wale walipokuwa Misri walitawanyika maeneo mbali mbali na walifuata mila na desturi za kimisri. Hivyo wakati wakitoka Misri hakukuwa na kanuni wala taratibu zozote za kuwaongoza kama taifa/jamii, hivyo ilibidi kuandika taratibu zao za kuwaongoza kama jamii ndio maana zimejaa mambo ya kimwili ziadi.....! Angalia zaidi utatambua hilo...mfano mtu akiua...alitakiwa kimbilia kwenye mji wa makimbilio ili kujiepusha na walipizaji kisasi........na haikuruhusiwa kumdhuru mtu huyo iwapo hakukamatwa mpaka ameingia mji huo....! Kwa maana rahisi kabisa amri za Musa zilikusudia kuleta mwongozo wa kiutawala katika jamii kwa ngazi ya chini kabisa.......hivyo wazee katika mahali husika waweze kutatua migogoro kupitia miongozo hiyo.....!

Natumaini nimefafanua kwa kiasi cha kueleweka...!
 
Ni NEVER kwa mtazamo wako. Kumbuka hata namna alivyokuwa anawaadhibu au kuwaamuru kuwapiga wengine wewe unasema wote walikuwa sawa machoni pa Mungu.
Huo usawa unausoma wapi ? Wakati imeandikwa...walipewa uwezo WA kufanyika wana....
Kama walikuwa ni wana tayari huu uwezo WA kufanyika ulitokana na nini ?

Kwani wewe ukimtandika mtoto wako ndio anakuwa sio mtoto wako?
 
Biblia unaposoma ni tofauti na kitabu cha hadithi.......kuna busara ndani yake lazima utumie...! Hata Yesu alipozungumza kuna kipindi alikazia na kusema MWENYE MASIKIO NA ASIKIE......akimaanisha kuna ufahamu zaidi ya kusikiliza tu.....

Nikirudi kwenye swali lako....ni budi ujue kuna mambo mawili makubwa wakati wa Musa;
1. Kwanza kuna amri za MUNGU ambazo Musa alipokea kupitia mbao zile za mawe.....hizo ndizo amri kuu...ambazo Yesu alipokuja kuitimiliza torati ali-summarize kuwa mbili i.e. Mpende BWANA Mungu wako na pia mpende jirani yako kama nafsi yako.
2. Pili kuna amri za Musa....! Ukumbuke wakati wana wa Israel wakitoka Misri ca. 600,000 people lilikuwa ni taifa tayari lakini watu wale walipokuwa Misri walitawanyika maeneo mbali mbali na walifuata mila na desturi za kimisri. Hivyo wakati wakitoka Misri hakukuwa na kanuni wala taratibu zozote za kuwaongoza kama taifa/jamii, hivyo ilibidi kuandika taratibu zao za kuwaongoza kama jamii ndio maana zimejaa mambo ya kimwili ziadi.....! Angalia zaidi utatambua hilo...mfano mtu akiua...alitakiwa kimbilia kwenye mji wa makimbilio ili kujiepusha na walipizaji kisasi........na haikuruhusiwa kumdhuru mtu huyo iwapo hakukamatwa mpaka ameingia mji huo....! Kwa maana rahisi kabisa amri za Musa zilikusudia kuleta mwongozo wa kiutawala katika jamii kwa ngazi ya chini kabisa.......hivyo wazee katika mahali husika waweze kutatua migogoro kupitia miongozo hiyo.....!

Natumaini nimefafanua kwa kiasi cha kueleweka...!

Safi sana.
 
me nikupe kwa kifupi mno! watu wengi wanachanganya sana haya mambo ya ki biblia.
Biblia imegawanyika mara mbili. kuna agano la kale ambalo lilihusu waisraeli tu! na kuna agano jipya ambalo linahusu kila mtu katika ulimwengu huu.
labda unambie kuwa wewe ni mu israel na unaishi kabla ya yesu kuleta agano la pili(jipya). Vinginevyo hizi sheria ambazo sisi hatupo tena chini yake ziliwafaa sana waisraeli kwa wakati huo!
si hiyo tu uliyoisema bali zipo nyingi tu ambazo hazifai na hazitekelezeki kwa sasa. Ndio maana Mungu alisema wazi kuwa "siku zinakuja nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Yuda. Si kama lile nililofa na baba zao wakalivunja........." Hivyo ndugu yangu hizo sheria na agano la kale kwa ujumla kwa sasa zisome kama story tu.

Mahubiri ya Yesu aliyotoa juu ya Mlima wa Zaituni:
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.Mathayo 5.17-20
 
Hakuna Sheria za Mungu na za Musa. Musa alitumika kama chombo cha uwakilishi
Tu.
Sheria zote ni za Mungu kupitia mkono WA Musa.
Agano ni mkataba na mkataba WA Mungu na wana WA Yakobo hauna uhusiano na mkataba WA Mungu na mataifa kupitia Yesu Kristo, hata Kama kuna vipengere vya mikataba vinafanana kwa kiasi bado mkataba WA nyumba ya Yakobo ni halali kwa nyumba ya Yakobo Tu.
Vigezo na Masharti huzingatiwa...

Soma post yangu # 47....ni suala simple la ufahamu tu wala halihitaji nguvu....!
 
We vipi?

Kwa nini hautaki kukubaliana na kilichoandikwa kwenye Biblia aisee?

Au unataka kusema Yesu ni MNAFIKI? Kwamba alimpa Mussa maelekezo ambayo yeye mwenyewe anaogopa kuyasimamia hasa akikutana na changamoto?

kwanza hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia Yesu amepata kutumia neno Mimi, wakati wote alikuwa anasema Mungu,sasa alipatwa na kigugumizi gani kusema Maelekezo ya Divorce Mussa alipewa na Mungu kwa sababu Fulani Fulani?

Ni kipi ambacho nimekikataa, wewe unataka nikubaliane na wewe kuwa Musa alikuwa na uwezo WA kusoma nyoyo za watu alikokuwa anawaongoza na kuwatungia sheria kadri ya ujuzi huo. Nakataa Kabisa Musa alikuwa ni mjumbe Tu aliyekuwa anawakilisha Yale aliyoamriwa na Yesu, Yesu ndiye alikuwa na uwezo WA kusoma mawazo na yaliyo moyoni mwa wana WA israel.
Hata walimwuliza kwa kumtega alijua yaliyokuwa moyoni mwao na ndiyo sababu akawajibu kadri ya hitaji Lao.

Hili la unafiki kwa Yesu linakuhusu wewe zaidi

Mimi siwezi kujadili kwa kuwa hauko tayari kupokea kitu kipya. Umekaririshwa ndiyo sababu hujui hata namna Yesu Kama Mungu alikuwa anajibu watu pasipo kujikweza lakini wenye busara walikuwa wanamwelewa...
 
Hayo yalikua maagizo waliyopewa wana wa Israeli wakati huo.
Mengine kati ya hayo yalibadilishwa baada ya Yesu Kristo kuja.
Mfano ni agizo la kutoa sadaka ya kuteketezwa ya wanyama, agizo la kutoa adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa, agizo la kutofanya kazi siku ya sabato, n.k.
Yesu Kristo ndio kielelezo chetu, na maagizo yake ndio tunayoyafuata.
Yesu Kristo aliendeleza baadhia ya maagizo ya agano la kale, na kubadilisha maagizo mengine.

Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.
 
Mbona mfano mfu huo.? Kwa hiyo kitendo cha kumtandika mtoto ndicho kinaamua awe wako au asiwe wako ?

Kwani uliposema Yesu aliwaamuru waisrael kupiga wengine kujenga hoja kwamba hao waliopigwa sio watu wa Mungu ulikuwa unamaanisha nini aisee?
 
Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.

Hatusemi alibadirisha.tunasema agano / mkataba WA kale ni tofauti na mkataba mpya WA mataifa.
Issue ni privity of contract na sio kubadili au kurekebisha.
 
Hatusemi alibadirisha.tunasema agano / mkataba WA kale ni tofauti na mkataba mpya WA mataifa.
Issue ni privity of contract na sio kubadili au kurekebisha.

Ulichojibu sio sahihi mwenzako hapo nyuma amedai kua Yesu alibadilisha na wewe unakanusha sasa nielewe nini?
 
Kwani uliposema Yesu aliwaamuru waisrael kupiga wengine kujenga hoja kwamba hao waliopigwa sio watu wa Mungu ulikuwa unamaanisha nini aisee?

Nilikuwa na maana Mungu aliua kuwa na mkataba maalum na wana WA Israel huku mkataba huo ukiwa hauwahusu wengine.
Ndiyo sababu aliwapa hata maeneo ya wengine kwa kuuamuru kuwapiga.
Sisimu kuwa wana kwa maana ya kuumbwa Nina maana kwa mkataba/ agano
 
Back
Top Bottom