Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili


Nimeona ugumu WA mjadala kutokana na maelezo Kama haya. Yesu ni Mungu alikuwa anajua nini Musa alisema na kwanini wakati MUSA alikuwepo maelfu ya miaka nyuma.
Yesu ndiye alimtuma Musa kwa kuwa Musa alikuwa mjumbe WA Mungu
Yesu alijibu kadri alivyoulizwa na wale waliokuwa wanaita sheria ya Musa ulitaka aseme sio MUSA ni Mimi ndiyo uelewe yeye ndiye alikuwa nyuma ya Maamrisho ya Musa au kwa uelewa wako MUSA alikuwa na sheria zake mwenyewe ?
 

Hujajibu swali
 
Kuhusu Agano,liliwekwa hata na Adamu Pia. halikuanzia kwa Ibrahim. Naona hausomi Biblia yak vizuri mkuu.

Nimekwambia ni agano la Ibrahim ndilo hilo lililokuja kwa uzao wake kupitia Yakobo / Israel.
Hilo la Adam naomba uliweke hapa na lilikuwa agano kuhusu nini ?
 

Ni NEVER kwa mtazamo wako. Kumbuka hata namna alivyokuwa anawaadhibu au kuwaamuru kuwapiga wengine wewe unasema wote walikuwa sawa machoni pa Mungu.
Huo usawa unausoma wapi ? Wakati imeandikwa...walipewa uwezo WA kufanyika wana....
Kama walikuwa ni wana tayari huu uwezo WA kufanyika ulitokana na nini ?
 

We vipi?

Kwa nini hautaki kukubaliana na kilichoandikwa kwenye Biblia aisee?

Au unataka kusema Yesu ni MNAFIKI? Kwamba alimpa Mussa maelekezo ambayo yeye mwenyewe anaogopa kuyasimamia hasa akikutana na changamoto?

kwanza hakuna sehemu yoyote kwenye Biblia Yesu amepata kutumia neno Mimi, wakati wote alikuwa anasema Mungu,sasa alipatwa na kigugumizi gani kusema Maelekezo ya Divorce Mussa alipewa na Mungu kwa sababu Fulani Fulani?
 

Biblia unaposoma ni tofauti na kitabu cha hadithi.......kuna busara ndani yake lazima utumie...! Hata Yesu alipozungumza kuna kipindi alikazia na kusema MWENYE MASIKIO NA ASIKIE......akimaanisha kuna ufahamu zaidi ya kusikiliza tu.....

Nikirudi kwenye swali lako....ni budi ujue kuna mambo mawili makubwa wakati wa Musa;
1. Kwanza kuna amri za MUNGU ambazo Musa alipokea kupitia mbao zile za mawe.....hizo ndizo amri kuu...ambazo Yesu alipokuja kuitimiliza torati ali-summarize kuwa mbili i.e. Mpende BWANA Mungu wako na pia mpende jirani yako kama nafsi yako.
2. Pili kuna amri za Musa....! Ukumbuke wakati wana wa Israel wakitoka Misri ca. 600,000 people lilikuwa ni taifa tayari lakini watu wale walipokuwa Misri walitawanyika maeneo mbali mbali na walifuata mila na desturi za kimisri. Hivyo wakati wakitoka Misri hakukuwa na kanuni wala taratibu zozote za kuwaongoza kama taifa/jamii, hivyo ilibidi kuandika taratibu zao za kuwaongoza kama jamii ndio maana zimejaa mambo ya kimwili ziadi.....! Angalia zaidi utatambua hilo...mfano mtu akiua...alitakiwa kimbilia kwenye mji wa makimbilio ili kujiepusha na walipizaji kisasi........na haikuruhusiwa kumdhuru mtu huyo iwapo hakukamatwa mpaka ameingia mji huo....! Kwa maana rahisi kabisa amri za Musa zilikusudia kuleta mwongozo wa kiutawala katika jamii kwa ngazi ya chini kabisa.......hivyo wazee katika mahali husika waweze kutatua migogoro kupitia miongozo hiyo.....!

Natumaini nimefafanua kwa kiasi cha kueleweka...!
 

Kwani wewe ukimtandika mtoto wako ndio anakuwa sio mtoto wako?
 

Safi sana.
 

Mahubiri ya Yesu aliyotoa juu ya Mlima wa Zaituni:
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.Mathayo 5.17-20
 

Soma post yangu # 47....ni suala simple la ufahamu tu wala halihitaji nguvu....!
 

Ni kipi ambacho nimekikataa, wewe unataka nikubaliane na wewe kuwa Musa alikuwa na uwezo WA kusoma nyoyo za watu alikokuwa anawaongoza na kuwatungia sheria kadri ya ujuzi huo. Nakataa Kabisa Musa alikuwa ni mjumbe Tu aliyekuwa anawakilisha Yale aliyoamriwa na Yesu, Yesu ndiye alikuwa na uwezo WA kusoma mawazo na yaliyo moyoni mwa wana WA israel.
Hata walimwuliza kwa kumtega alijua yaliyokuwa moyoni mwao na ndiyo sababu akawajibu kadri ya hitaji Lao.

Hili la unafiki kwa Yesu linakuhusu wewe zaidi

Mimi siwezi kujadili kwa kuwa hauko tayari kupokea kitu kipya. Umekaririshwa ndiyo sababu hujui hata namna Yesu Kama Mungu alikuwa anajibu watu pasipo kujikweza lakini wenye busara walikuwa wanamwelewa...
 

Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.
 
Mbona mfano mfu huo.? Kwa hiyo kitendo cha kumtandika mtoto ndicho kinaamua awe wako au asiwe wako ?

Kwani uliposema Yesu aliwaamuru waisrael kupiga wengine kujenga hoja kwamba hao waliopigwa sio watu wa Mungu ulikuwa unamaanisha nini aisee?
 
Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.

Hatusemi alibadirisha.tunasema agano / mkataba WA kale ni tofauti na mkataba mpya WA mataifa.
Issue ni privity of contract na sio kubadili au kurekebisha.
 
Hatusemi alibadirisha.tunasema agano / mkataba WA kale ni tofauti na mkataba mpya WA mataifa.
Issue ni privity of contract na sio kubadili au kurekebisha.

Ulichojibu sio sahihi mwenzako hapo nyuma amedai kua Yesu alibadilisha na wewe unakanusha sasa nielewe nini?
 
Kwani uliposema Yesu aliwaamuru waisrael kupiga wengine kujenga hoja kwamba hao waliopigwa sio watu wa Mungu ulikuwa unamaanisha nini aisee?

Nilikuwa na maana Mungu aliua kuwa na mkataba maalum na wana WA Israel huku mkataba huo ukiwa hauwahusu wengine.
Ndiyo sababu aliwapa hata maeneo ya wengine kwa kuuamuru kuwapiga.
Sisimu kuwa wana kwa maana ya kuumbwa Nina maana kwa mkataba/ agano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…