Shukurani kwa habari za ushindani katika kutafuta elimu.
Pongezi kwa vijana, hususan wanaoweza kufanya vizuri licha ya mazingira magumu.
Zaidi, nasikitika sana kuona kwamba tunaweza kushangilia sana hawa vijana wakati baadaye hawasikiki kufanya lolote la ajabu.
Ni kama mtu anayeshangilia kwamba ana gari kali sana Ferrari, lakini hajui kuendesha wala hana dereva wala hana mpango wa kuliuza au kukodisha.
Matokeo yake anaishia kupanda daladala mkweche.
Ukiangalia viongozi wa nchi hii, hiyo ndiyo habari yetu.