Ma-TO walipofunikwa na Sylivester Mwageni (True mathematician)

Ma-TO walipofunikwa na Sylivester Mwageni (True mathematician)

Hawa magenious au T.O sijui huwa wanaish maisha gan,
Yan wao unawakuta hawana kabisa na stress za maisha na ata ukimpita ki pesa wao wanachukuloa kawaida tu,

Kama pale kkoo kuna jamaa anaitwa mnegro uyo jamaa hafai, yule n pure talented kila angle (kiswahil tu, ndio mbovu adi mwsho)
Anapiga maths ad unafurah kuanzia kuelekeza ad anapofanya maswal ila anaish simple saaana
Ila kusafiri tu kajitahid kuizunguka dunia, ila ukimuona lazma ukatae
 
Uyu mnegro hakuwa TO ila advance alikung'uta one ya 3, EGM
 
martin chegere kaongoza darasa la 7 taifa wakati anasoma ukonga.Akachaguliwa kibaha hakwenda,akaenda maua seminary akawa t.o o lev,akaenda pugu advance akawa t.o,akaend udsm bachelor akaongoza,masterz udsm akaongoza,akaenda Phd sweden akaongoza.
karudi ud anafundisha.
Kanifundisha agricultural economics UD
 
Niliwahi kupata one ya 3 katika pre national pekee ya advance
 
Write your reply...Gwamaka njobelo, huyu jamaa mi nimepiga naye primary 2005 dom town.jamaa alikuwa mpole sana..bt ni genius hatali..toka tuko madarasa ya mwanzoni mpk darasa la saba G alikuwa anashika nafac ya pili au ya kwanza..then kulikuwa na Ramadhani Suka uyuu ndo alikuwa anaongoza mara nyingi kwenye mitiani ya mwez wa sita na 12..

afu kulikuwa na Athanas Rafael uyu namba tatu...wilaya nzima ilikuwa inajua shule yetu kuna utatu mtakatifu..walimu wa shule za jirani walikuwa wanawajua awa watu..dah maisha yanaenda kasi sana,matokeo ya darasa la saba yametoka:GWAMAKA MZUMBE,RAMADHANI IFUNDA,ATHANAS ILBORU..nau Gwamaka yuko US FRORIDA ANACHUKUA MASTER CIVIL ENGINEERING.
 
SHULE YA SEKONDARI MAURICE inawatangazia wazazi na walezi wote kwamba tunapokea wanafunzi kidato cha kwanza mwaka 2019, nafasi za kuamia kidato cha kwanza na cha pili pia tuna kituo cha mitihani kwa watahiniwa wa kujitegemea na Q.T. Vile vile pia tunapokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa michepuo ya ECA, HGE, HGK, HKL na HGL. ADA ni nafuu sana. Shule ni ya kutwa na bweni kwa wavulana na wasichana. Shule ipo Dar es salaam wilaya ya temeke, eneo LA mbande kisewe. Simu 0785907371. Wote munakaribishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HII POST IWE INSPIRATION KWA WANAFUNZI WOTE WA SEKONDARI NA WAZAZI WA WATOTO HAO

Ma-TO walipofunikwa Na Sylivester Mwageni(True mathematiBite wewe na mimi ni vilaza wa math toka primary cian)

Kuna matukio fulani hutokea kwa namna pekee ya kushangaza na mengine huwa ya kufurahisaha zaidi hasa katika suala letu hili pendwa la ELIMU.

Napenda sana kuhudhuria jukwaa hili na ' ITAPENDEZA ' nikiitwa ' MASTER WA JUKWAA LA ELIMU '

Sasa leo nawakumbushia tu historia ya T.O Maarufu zaidi "GWAMAKA NGOBELO" wa MZUMBE SPECIAL SCHOOL na "JAMALI JUMA aka BABU wa FEZA BOYS au AZANIA au ukipenda ITA Azaboys " walipokutana kwa wakati tofauti na KISIKI katika somo la PURE MATHEMATICS aitwaye 'SILVESTER'

Tukubali tukatae ila kuna watu katika ULIMWENGU huu wamebarikiwa sana kuwa na akili,pamoja na hivyo akili za VICHWA hivi viwili kwa nyakati TOFAUTI walijikuta wakimpigia SALUTE Silvester wa KIBAHA kwa kusema 'Kwa Mathematics sikuwezi'.

Bila shaka humu JamiiForums wapo watu waliosoma KIBAHA au waliofanya EZERB form 6 mwaka 2012 na wakasikia JINA Silvester hivyo wanaweza kuthibitisha hiki ninachokisema hapa.

STORY INAANZIA MWAKA 2009
Tuanzie Azania High School mwaka 2009 alitokea mwanafunzi mmoja aliyeteka sana attention kielimu katika Jiji la Dar es Salaam kwa wakati huo akijulikana kama JAMALI JUMA. Wengi tuliosoma DSM miaka hiyo sio rahisi kulikumbuka JINA hilo la JAMALI JUMA ila tutamkumbuka mwanafunzi huyo huyo kwa jina la BABU.

Jamaa alifanya maajabu katika mtihani wa TAHOSA Form 4 baada ya kunyuka "A" 7 na kupata div 1.7 na kuwa "BEST STUDENT" wa DSM katika mtihani huo huku akiwaacha mbali VIPANGA wa FEDHA wakibaki wanashangaa kuwa Kijana wa AZANIA anayelipa ADA ya elfu 20 tu akionyesha maajabu mbele ya Mamilioni yaliyojaa Fedha kutokana na ADA za wanafunzi.

Jamali Juma aka BABU alikuwa very talented,na alikuwa very very very talented katika somo la MATHEMATICS.Wanafunzi wote wa AZANIA na DSM kwa ujumla waliamini kuwa sasa ENZI za Azania kutoa T.O tena zimerudi hivyo.Shule ya AZANIA ilikuwa na wakali wengi sana KIPINDI hicho ambao walifichwa ndani ya KIVULI cha JAMAL JUMA aka BABU.

Babu pamoja na kuwa alikuwa na uwezo mkubwa sana darasani ila alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi wote wa AZANIA olev wanakuwa katika hali nzuri hivyo akaanza kupita darasani kuwafundisha wanafunzi mada ambazo walikuwa hawazielewi kabisa katika masomo yote kuanzia PHYSICS mpaka wale wazee wa kusoma kama wanasoma "GAZETI"(Hahahahah hili bifu nalibeba).Hakika babu alikuwa ni MFANO mzuri wa kuigwa(Wa Azania ni mashahidi).

Maisha yaliendelea mpaka matokeo ya Form 4,2009 yalipotoka ambapo T.O wetu wa DSM ahakuamini macho yake akijikuta ameangukia PUA na kuambulia DIV 1.10

Jamali Juma aka BABU akapangwa MZUMBE akasome PCM class ambalo atakuwemo T.O(hahahahah) anayeitwa GWAMAKA NJOBELO.

Story ya huyu GWAMAKA NJOBELO aliyekuwa wapili kitaifa

STORY YA MWAKA 2009 ikaishia hapo

Baada ya shule za Advance Kufunguliwa hatimaye SHULE YA "FEZA BOYS" ikafanikiwa kumshawishi JAMLI JUMA akajiunga FEZA na maisha ya ADVANCE yakawa na changamoto nyingi sana kwake hasa ALIPOJIKUTA kwenye KIVULI cha jamaa ZAWADI MDOE ambaye yeye hana kitu chochote anachokifiria zaidi ya KUWA T.O

===
TURUDI KIBAHA HIGH SCHOOL

Alilipoti mwanafunzi aliyekuwa na marks za kawaida tu OLEV aliyeitwa SILVESTER.Silvester alikuwa ni mwanafunzi ambaye 'ANAJUA ' mathematics kuliko mwanafunzi yeyote TANZANIA kipindi hiko,hivyo kwa kujiamini kabisa akatangaza kuwa hakuna MTU ALIYENIPITA Additional Math na Basic Math Olevel japo Sikuwa T.O ila Hakuna wa kushindana na mimi katika mtihani wa MATHEMATICS wowote.Silvester alinikuliwa akisema hata mwalimu wa KIBAHA nafahamu kabisa kuwa haniwezi math(Hahahaha).

Wanafunzi waliotoka MZUMBE na AZANIA Olev wakaenda KIBAHA wakmwambia "Sikia Silvester,wote tunajua hapa KIBAHA kuwa wewe ndio MCHAWI wa namba ila kuna vichwa VIWILI huwezi shindana navyo kabisa ambao ni Jamal Juma aka BABU wa FEZA na GWAMAKA wa Mzumbe maana jamaa wakiliona tu swali wanaona mpaka mwisho wake".Silvester akawajibu simple tu naomba LIGI nao ya MATH tu niwathibitishie tu kuwa Tz Hii hakuna ZAIDI yangu katika Somo hili...Hahahah jamaa akatania kuwa "haya mambo yana wenyewe na wenyewe ndio sisi"

Kwa wa KIBAHA kulikuwa na msemo "TANGO LILIKUSHINDA MPELEKEE SILVESTER ,HAYA MAMBO YANA WENYEWE DOGO."

Dah long time aisee ila japo wote ni VIPANGA ila maswali ambayo yalikuwa VIPANGA kwa VIPANGA yalipelekwa Chemba ya KIPANGA Sivester.

Haikuchukua mda mrefu hatimaye taarifa zikatua MZUMBE kwa MA-TOs kuwa kuna dharau huko KIBAHA hivyo wanahitajika KWENDA KIBAHA kuwasha MOTO.Hahahah wanafunzi wa MZUMBE hawakuwa na presha na SILVESTER maana walikuwa wanafahamu kuwa MZUMBE na KIBAHA wanafanya mtihani mmoja wa MOCK(ezeb) hivyo mwambieni ajiandae vizuri tunakuja kuwasha MOTO.

=====
Hatimaye taarifa zikatumwa kwa BABU aka MCHAWI wa MATH DSM akitokea FEZA na kuamua kuwa YUPO tayari kufanya MTIHANI na SILVESTER Jangwani Sec kwa Manyirizu kama atakuwa tayari.

Kilia jumamosi BABU akawa anaenda kujipima KWA Manyirizu kumsubili SILVESTER,na wakati huo huo SILVESTER anachati tu kwa simu yake akimsubiri BABU siku itakapo fika akaonyeshe kuwa Tz hii hakuna kama yeye katika math.

Siku ilipofika wanafunzi wa KIBAHA waliosoma na BABU Azania wakampigia simu kumwambia nasi tutakuja kufanya mtihani kwa manyilizu hivyo KIBAHA BOYS itahamia JANGWANI GIRLS.Vijana wa KIBAHA wakatimba KWA MANYIRIZU huku Babu akiwa hayupo na walipomtafuta kwenye simu hakupatikana kabisa.Hii tunaitwa "Jamaa alikimbia "..

Vijana wa KIBAHA BOYS wakafanya mtihani na kuondoka na "A" zao huku vilaza wengine wa DSM wakaambulia C na B..

Kama kawaida,week iliyofuata BABU akaripoti kituo cha mtihani JANGWANI kujipima(Hii tunaita unaangalia kwanza usalama then unaenda) na akawa kama anasukuma WALEVI baada ya SPECIAL SCHOOL NIGGAS kuondoka.

Baada ya weeks 3 babu akatoa sababu mbali mbali za msingi za kutoweza kufika siku ile kujipima hivyo akawaomba waje tena awawashie moto..

VIJANA WA KIBAHA wakwambia SILVESTER ajiaandae kesho(Ijumaa) waondoke watafikia HOSTEL za Azania na watamlipia nauli ya kwenda na kurudi na hela ya kula.Jeshi la watu 19 walitoka KIBAHA wakiongoza na SILVESTER kwenda Azania ila katika kundi hili la watu 19 atakayefanya mtihani ni mmoja tu,yaani wengine ni wapambe tu(Hahahahah wanafunzi bhana).

Baada kufika BABU na SILVESTER wakaingia CHUMBA cha mtihani huku nje vijana wa KIBAHA BOYS wanabadilishana mawazo na JANGWANI Dadaz waliokuwepo hapo(Yani vijana wakapata vitonga)..

Baada ya kutoka CHUMBA cha mtihana wote SILVESTESTER na BABU walikuwa na FURAHA kuonyesha kila mmoja anajiamini kuwa HAKUNA wa kumzuia kuwa wa kwanza.

MATOKEO YALIPOBANDIKWA

Matokeo yalionyesha kama ifuatavyo:
1.SILVESTER aliyepata 100%
2.BABU aliyepata 99% na
3.Said aka MSELEM wa Azania aliyepata 71%

Na huo ndio ukawa mwisho wa UBISHI wa Babu na SILVESTER .Kama ilivyo desturi ya MANYIRIZU ambapo MTU anayekuwa wa KWANZA atafanya mtihani ujao bure hivyo nafasi hii ikaangukia kwa SILVESTER amabaye hatokuwepo DAR hivyo akaamwambia MANYIRIZU kuwa nafasi hiyo ampe BABU na manyirizu akafanya hivyo.

VIJANA WA KIBAHA BOYS WAKAONDOKA NA USHINDI

=====
Habari zikafika MZUMBE ambapo ilikuwa ni weeks mbili kabla ya MOCK aka EZEB.Vijana wa MZUMBE wakaongeza moto zaidi kujiandaa na EZEB wakijua kuwa KUTAKUWA na SILVESTER.

MATOKEO YA EZEB YALIKUWA KAMA IFUATAVYO:

Best Student overall alitoka MZUMBE anayeitwa GWAMAKA NJOBELO akipata 1.3 PCM huku akiwa na A ZOTE PCM

NOTE:Silvester alikuwa na Div 1.5 hivyo hakuingia hata TOP 20

Waliongoza masomo PCM ni wafuatao:

1.GWAMAKA JOBELO(Physics-A)
2.GWAMAKA JOBELO(Chemistry-A)
3.SILVESTRE(Advance Math-A)

Na huo ndio ukawa Mwisho wa ubishi wa SILVESTER na GWAMAKA.Dah maisha bhana Kwa mara ya kwanza GWAMAKA AKAKILI KUWA "Simuwezi Silvester Math".Matango yote ya math kutoka mzumbe yakawa yanatatuliwa KIBAHA kwa Genius SILVESTER ambaye kwake hakuna swali linalompa changamoto kwenye TRANTA.
======

Matokeo ya mwisho kitaifa yalikuwa kama ifuatavyo:

1.Jamali Juma aliingia TOP 10 akiwa wa 4 kitaifa

Ikumbukwe kuwa mwaka 2012 div 1.3 kitaifa zilikuwa 4 tu huku jamali Juma akifunga namba nne

(Huyo watatu kitaifa kutoka Minaki Katika mtihani wa MOCK EZEB alikuwa Div 1.5 huku akipata A ya phys na math na C ya Chem,matokeo ya necta alikuwa wa pili chemistry kitaifa)

2.GWAMAKA NJOBELO

Alikuwa wa 8 kitaifa baada ya kupata 1.4

3.SILVESTER MWAGENI

Baada kutoka kwenye mtihan wa math FORM 6,SYLVESTER Alionekana amechukia sana na alipoulizwa mtihani unauonaje akajibu "Mtihani ni mwepesi sana,sijawahi kuona mtihani mwepesi kama ule.Ni bora mtihani uwe mgumu ili tutakaopata 100% tuwe wachache kuliko mtihani ule ambao tutakaopata 100% tutakuwa wengi sana".

Na SYLVESTER hakuingia TOP 10 ila hakuna mtu aliyempita ADV MATH..Yani kwa kifupi ndiye Best Student WA ADVANCE MATH.

=====
TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO

Wale vilaza wenzangu tusivunjike moyo.Sisi math hatuwezi ila tutajitahidi huku huku kwenye MOFIMU na VIHISISHI


Dengue f

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona huu Uzi upo humu,

Umeuiba wap

'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
 
Aiseeee..mi kiukweli niliona madaftari mazito saana. Nikawa nabeba biscuit zangu za eatsome more kwa warembo wangu. Shule ilinisumbua sana saaaana.. Lakini bimkubwa alikua hakati tamaa sijui alijua kuna miujiza kwenye kufaulu..
Du nmecheka mpaka nmelia aisee
 
Back
Top Bottom