Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote, 28/09/2026

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote, 28/09/2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote, fuatilia mijadala mbalimbali katika kuadhimisha siku hiyo...
photo_2026-09-28_11-28-20.jpg

Ernest Sungura (4).jpeg

Ernest Sungura​

Pia soma ~ Kuelekea Maadhimisho ya IDUAI 2026: Unapataje Taarifa Sahihi katika enzi hizi za Kidijitali?

“Changamoto yetu si uhaba wa taarifa, kwani kuna mafuriko ya taarifa potofu ikiwemo zinazotengenezwa na Akili Mnemba (AI), habari za kupotosha zinasambaa kwa kasi kuliko ukweli, wakati mwingine ni vigumu kutofautisha kati ya halisi na bandia.”

“Hivyo, kupata taarifa pekee haitoshi bali kupata taarifa sahihi na kwa wakati, Wananchi wanahitaji taarifa zinazopatikana kwa wakati na zinazoaminika.”

Ernest Sungura - Mwenyekiti wa Mtandao wa Wadau wa Haki za Kupata Taarifa (CoRI)
Septemba 28, 2026


Sungura: Uongo haufi kwa ukimya, unakufa kwa ukweli mwingi

Ernest Sungura, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wadau wa Haki za Kupata Taarifa (CoRI), amesema “Katika zama hizi, kujidhibiti (self-regulation) si anasa, ni ulinzi wa uhuru wetu. Kama hatutajidhibiti kwa weledi na maadili, wengine watatudhibiti kwa sheria kali.”

Ameongeza “Kwanini tunapaswa kukomesha tabia ya kuficha ukweli? Sababu historia inatuambia, unaweza kukifunga chombo cha habari, lakini huwezi kuifunga historia. Ukweli ukifichwa leo, hujitokeza kesho, ukiwa umeshaondoa imani ya Wananchi.”


Sungura: Kupata taarifa pekee haitoshi bali kupata taarifa sahihi
“Changamoto yetu si uhaba wa taarifa, kwani kuna mafuriko ya taarifa potofu ikiwemo zinazotengenezwa na Akili Mnemba (AI), habari za kupotosha zinasambaa kwa kasi kuliko ukweli, wakati mwingine ni vigumu kutofautisha kati ya halisi na bandia.”

“Hivyo, kupata taarifa pekee haitoshi bali kupata taarifa sahihi na kwa wakati, Wananchi wanahitaji taarifa zinazopatikana kwa wakati na zinazoaminika.”

Jebra Kambole: Mwananchi anajua akienda JamiiForums atauliza atapata taarifa sahihi
Wakili wa Kujitegemea Jebra Kambole anasema "Kutokana na changamoto ya kutopatikana kwa taarifa sahihi ndiyo maana Wananchi wengi wanakuwa na vyanzo vyao wanavyoamini hata kama siyo mamlaka husika.”

Anaongeza “Mojawapo wa Majukwaa ni JamiiForums, anajua nikienda pale nitapata taarifa kwa kuwa nikiuliza watafanya ‘Fact Checking’ na nitapewa majibu. Hivyo, ukifungia vyombo kama hivyo unaonesha jinsi ambavyo utoaji wa taarifa bado upo shakani kwenye Taifa."


Wakili Evordy Kyando: Upatikanaji wa taarifa unaohusisha kutafuta, kupokea au kutoa ni haki ya msingi ya kila Mwananchi
Mwakilishi kutoka Idara ya Habari-Maelezo, Wakili Evordy Kyando akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo, ameeleza utayari wa Serikali kushiriki katika majadiliano ya wadau wa habari, huku akisisitiza kuwa utoaji na usimamizi wa taarifa sahihi ni haki ya msingi na jukumu linalohitaji ushirikiano wa wadau wote.

Wakili Kyando alieleza kuwa katika zama hizi za kidigitali, kupatikana kwa taarifa potofu (misinformation, disinformation, na mal-information) pamoja na matumizi ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence) kumekuwa kikwazo kikubwa kwa uamuzi sahihi wa wananchi na maendeleo ya taifa.

"Upatikanaji wa taarifa unaohusisha kutafuta, kupokea, kutoa au kutumia taarifa za kihabari... ni haki ya msingi ya kila mwananchi. Hii ni haki kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali tuna dhamana tu ya hao wananchi katika kusimamia na kuhakikisha hayo yaliyopo kwenye Katiba na sheria husika yanaenda kama ilivyotegemewa."

Wakili Kyando amesisitiza kuwa ulinzi wa uadilifu wa taarifa haupaswi kuachiwa serikali pekee, bali unahitaji mchango wa waandishi wa habari, taasisi za kiraia, na wananchi kwa jumla.

Amesema "Serikali inapenda kusisitiza kuwa kusimamia uadilifu katika mnyororo wa taarifa ni jukumu muhimu sana na haifai kuachwa serikali pekee yake.

“Waandishi wa habari, wadau wote wa uhuru wa habari wana wajibu wa kushiriki na kuipa ushirikiano serikali katika kupambana na masuala haya ambayo yanaathiri ukweli, usahihi, ubora na uadilifu wa habari."


Wakili Maduhu: Kuzima Mtandao ni utashi sio Sheria, Nchi ni ya Wananchi Wote, sio Mamlaka ya Watu Wachache
Wakili William Maduhu anasema “Juni 2026 nilifanya mafunzo mbalimbali Afrika Kusini, moja ya sehemu tuliyotembelea ilikuwa ni Mamlaka ya Mawasiliano. Tulipokuwa tunazungumzia suala la kuzimwa kwa Mtandao, walitushangaa sana, walisema Nchi yao haipangi, haifikirii na wanadhai hiyo haitatokea kwao."

Akitolea mfano kuzimwa kwa Internet wakati wa Uchaguzi ameeleza kuwa haikuwa matokeo ya ukosefu wa sheria au katiba, bali ni hofu na ukosefu wa dhamira njema ya kisiasa.

"Suala la kuzima mtandao halina majibu ya kisheria na katiba wala mikataba ya kimataifa. Ni suala la integrity na ni suala la political will la waliopo madarakani. Hata tukiwa na sheria nzuri namna gani, watazima tu mtandao."

Maduhu ameeleza kuwa Ibara ya 8 ya Katiba inaweka wazi kwamba Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na utawala nchini, kuzima mtandao kwa hofu ya kile kinachosemwa na wananchi ni kinyume na misingi ya Jamhuri na badala yake kunatengeneza utamaduni mbaya. Wananchi ndiyo wenye mamlaka na utawala wa mamlaka nchini.”

Balile: Nilianza kuvaa suti ili ni-jibrand sababu walikuwa wanazungumza vibaya uandishi
"Wanahabari na watu wa siasa, tumeungana kuua uandishi wa habari... Tumeungana kuua uandishi wa habari hapa nchini. Kila wakati tunawaambia watu, 'uandishi umekufa.' Sisi wenyewe! Tunawaambia watu uandishi umekufa, TV haziangaliwi, magazeti hayasomwi, redio hazisikilizwi.

Sasa nauliza, kama sisi wenyewe tunatoka hadharani kuwaambia hivyo watu, kwa nini bado tunaendelea kuwepo kwenye vyombo vya habari?"

Mfano mimi nilianza safari ya kutangaza umaskini kwa kuanza kuvaa suti, kwa sababu angalau itapunguza unyonge. Maana ukifika sehemu hivi, kila mtu anajua ombaomba ingia. Kwa hiyo kwanza tijibrand kama taaluma."

Jenerali Ulimwengu:
"Kawaida Binadamu ni waoga wa kitu kipya, tusiwe na uoga wa Akili Mnemba (AI), tuchukue tahadhari kama wanavyochukua wenzetu katika mataifa yaliyoendelea Kimataendeleo. Tujifunze teknolojia mpya na tujue namna ya kuimudu."

TBC ni Shirika la Utangazaji la Taifa au Shirika la Utangazaji la Serikali, kwa muda mrefu shirika hilo lmekuwa si mnyamna si ndege, linajinasibisha kuwa la Taifa lakini nikiliangalia naliona ni la Serikali. Linaendeshwa kwa kodi za Wananchi lakini kama kitu hakiipendezi Serikali hukioni kwenye TBC.

Jenerali Ulimwengu: Nadhani kilichotokea Oktoba 29, 2025 chochocte ambacho kilitokea hakikuipendeza Serikali hakikuweza kupelekwa hewani, mwisho wa siku SHirika linakuwa la CCM. CCM iiachie TBC ifanye kazi kama Shirika la Taifa.
 
Sasa hiii inasaidia nini au inaongeza nini katika kuondoa umaskini kwa wananchi je bajeti yake imetumika billion ngapi kuadhimisha siku hiii
 
Back
Top Bottom