"Maadili ya Kitanzania" yameandikwa wapi nikayasome?

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
6,373
Reaction score
16,073
Huwa nasikia tu, ati umevunja maadili ya kitanzania, mara sijui jambo hili limekiuka maadili ya kitanzania!

Hata ukikata uno la mayenu unaambiwa umevunja maadili ya kitanganyika!

Ukivaa mabuti kama ya JAY Z unaambiwa umekiuka sijui MILA ZA KITANGANYIKA!

Kuna wale watu wenye fikra za ujima huwa wamekaa chonjo muda wote wanasubiri ufanye jambo tu wakurukie ati umevunja tamaduni za kitanganyika. Ukikohoa kidogo, ooh umevunja utanganyika!

Hayo maadili ya kitanganyika yako wapi tukayasome? Kuna kijarida labda yaliandikwa na nyerere labda?? Au kulikuwa na azimio labda la kukubaliana kwamba mambo kadhaa ndio mila za tanganyika?

Utajuaje kama jambo fulani ni mila ya kitanganyika au ni fikra za mtu tu mwenye ujinga kichwani?

Kwa mfano nikitaka kurejelea hiyo mila ya kitanganyika nikaangalie kitabu gani cha bunge? Hakuna hata pamphlet lenye orodha ya mila za kitanganyika?

Sasa kama hakuna orodha tutajuaje??

Nitafanya ninalolitaka madhali sivunji sheria, sasa ole wake aje mtu aniambie sijui mila ya kitanganyika!

Ukinivaa nitakuvaa.
 
Afrika tuna maadili yetu ki ujumla ambayo yapo wazi na yametapakaa katika mataifa yote afrika.

Leo hii njo Tanzania, nenda Senegal, Bukinafaso, Zambia, Morocco, Egypt, Kenya Nk. Kote huko Mwanaume kukata viuno sio jambo jema na lipo kinyume na maadili.
 
Unawazungumziaje wakongo mani kwenye hili?
 
Vipi maadili ya watoto chuchu saa sita kutembea wazi bila blazia imekaaje mana Afrika ipo hii??.
 
Hayo maadili yameandikwa wapi?
 
Ni maadili ya mtu mweupe na muarabuπŸ˜‚ sijui kuchana nywele, kusalimia shkamoo, dini yenyewe....

waarabu na wazungu ndo walitupa hayo maadili kwa kisingizio kwamba wanatu 'civilize' (kututoa ushamba).... maadili yetu yalikua kuvaa nusu uchi, kuoa wake wengi, ulevi nk....

mimi hua sichani nywele, maadili ya nyoko
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ
 
Kila kabila Lina Mila na miiko yake tupo kabila 120 sasa lini tulikubaliana kuwa haya ni maadili yetu wote watanzania Nani alikuwa mwenyekiti wa hicho kikao
 
Kila kabila Lina Mila na miiko yake tupo kabila 120 sasa lini tulikubaliana kuwa haya ni maadili yetu wote watanzania Nani alikuwa mwenyekiti wa hicho kikao
Ndo nashangaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

Ni kama vile wote tunaishi kijiji kimoja!
 
Huwa nashangaa sana hata mimi , Ila kwa nijuavyo namna ya kuishi kama mtanzania Ipo wazi kwenye Katiba ya nchi na sheria mbalimbali za nchi na Bylaws za sehemu mbalimbali. Zaidi ya hapo hakunaga cha maadili wala dada yake maadili, kikubwa usivunje sheria Tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…