"Maadili ya Kitanzania" yameandikwa wapi nikayasome?

"Maadili ya Kitanzania" yameandikwa wapi nikayasome?

Mi niliwahi kualikwa kwa mwanajeshi mmoja kula pilau la idd nikavaa zangu jeans nyembamba sana nikashangaa anaeni mind ni dingi mmoja mstaafu amevaa suruali ina viuno viwili. Yaani kuna kimoja kiko tumboni kina mkanda na kingine kiko chini yake nacho kina mkanda, nikasema dah hata kama ni upedeshee hii hamna. Suruali inakuwaje na sehem 2 za kuweka mkanda, hii nayo si kukosa tu maadili?
😂😂😂😂😂🙌🙌
 
Huwa nasikia tu, ati umevunja maadili ya kitanzania, mara sijui jambo hili limekiuka maadili ya kitanzania!

Hata ukikata uno la mayenu unaambiwa umevunja maadili ya kitanganyika!

Ukivaa mabuti kama ya JAY Z unaambiwa umekiuka sijui MILA ZA KITANGANYIKA!

Kuna wale watu wenye fikra za ujima huwa wamekaa chonjo muda wote wanasubiri ufanye jambo tu wakurukie ati umevunja tamaduni za kitanganyika. Ukikohoa kidogo, ooh umevunja utanganyika!

Hayo maadili ya kitanganyika yako wapi tukayasome? Kuna kijarida labda yaliandikwa na nyerere labda?? Au kulikuwa na azimio labda la kukubaliana kwamba mambo kadhaa ndio mila za tanganyika?

Utajuaje kama jambo fulani ni mila ya kitanganyika au ni fikra za mtu tu mwenye ujinga kichwani?

Kwa mfano nikitaka kurejelea hiyo mila ya kitanganyika nikaangalie kitabu gani cha bunge? Hakuna hata pamphlet lenye orodha ya mila za kitanganyika?

Sasa kama hakuna orodha tutajuaje??

Nitafanya ninalolitaka madhali sivunji sheria, sasa ole wake aje mtu aniambie sijui mila ya kitanganyika!

Ukinivaa nitakuvaa.
Yako impliedly; hayaajaandikwa mahali.

Kwa mfano, nyumbani kwako huwa mnakula mkiwa mmekaa; aidha chini ya sakafu au kwenye meza. Kwa hiyo tuseme kwa mfano, si maadili ya kitanzania mtu kula chakula akiwa amesimama

Issue hii ya m-Tanzania kula chakula akiwa amekaa na si kusimama, haihitaji kuandikwa mahali
 
Back
Top Bottom