Maadili yameshuka sana ndio maana watu wanachekea matatizo

Maadili yameshuka sana ndio maana watu wanachekea matatizo

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,687
Reaction score
1,111
Niliwahi kuandika kwa kuonya juu ya mmomonyoko wa maadili katika jamii tunayoishi, watu walipuuza lakini leo tunaishi matokeo ya mmomonyoko huo.

Baada ya mihimili mitatu ya kikatiba, muhimili unao fuatia ni media na taasisi za dini. Unapokuwa na mihimili hususani inayo simamia maadili ya umma Kama taasisi za kidini na waandishi wa habari dhaifu, iliyo na upendeleo (biased) ni ngumu Sana kutengeneza jamii yenye maadili mema.

Leo nitazungumzia anguko la mihimili miwili isiyo rasmi ambayo ni DINI na VYOMBO VYA HABARI.

Unapokuwa na viongozi wa dini walio gawanyika kwa makundi kwa kutanguliza maslahi binafsi bila kujali kazi ya kitume ujue jamii inayoongozwa inapoteza mwelekeo.

✓✓Bahati mbaya Sana leo viongozi wetu wa dini wamekubali kugawanywa kwa misingi ya kitume na kuwa watumwa wa Watawala, wameacha maadili ya kichungaji, wamegeuza batili kuwa halali kwa kutengeneza uhalali wa kualikwa kwenye karamu za Watawala.

Ndio maana hawana uwezo wa kukemea maovu yanayo wagusa Watawala kwa kuwa wana maagano nao. Wacheza ngoma wana mpiga nyanga kwa maana ya mshereheshaji wa kunogesha ngoma, viongozi wetu wa dini wamekuwa wapiga nyanga wa Watawala, ndio maana Mtawala anapokuwa na ziara zake lazima uwaone mbele yake wakishangilia maudhui ya mtoa hotuba anapo wananga watawaliwa, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kuionya serikali Wala kiongozi juu ya madhira yanayo ikumba jamii hii.

Kwa mantiki hiyo utaona kuwa mbali na kujenga chuki kwa viongozi wa dini inachochea watawaliwa kuichukia mamlamka ya utawala kwa kuwa imekuwa kandamizi kwao.

Matokeo yake Mtawala akiugua kwao ni furaha na shangwe, mbaya zaidi wanakitumia kipindi hicho kufanya dua za kifo kwa kuomba madhara ya mkumbe mtesi wao Kama sehemu ya kisasi chao kwao.

Hii ina tengeneza mpasuko mkubwa ndani ya jamii, kwa kuwa msuluhishi wa migogoro amegeuka kuwa sehemu ya mlalamikiwa, ni sawa na fisi akiwa hakimu mbuzi hana haki.

✓✓ Vyombo vya habari navyo vimekengeuka na kuingia kwenye mkumbo Kama walivyoingia viongozi wadini. Vyombo hivi vimeacha maadili ya uandishi katika kukemea maovu, vimeingia katika mapambio ya kusifu na kuabudu na kuiacha jamii ikikosa wakuisemea. Sioni habari za kichambuzi zinazo ibua uhalifu wa kimamlaka Kama ilivyo kuwa hapo awali, wameshindwa hata kujitetea kwa kuipinga sheria mpya ambayo ni kaa la Moto kwao. Wanachojali ni posho kwa misafara wanayoalikwa.

Kimantiki wamekubali kuwa silaha ya maangamizi kwa kuficha ukweli.

Hata hao waliojitoa Mhanga kupambania maslahi ya umma wote tunayajua yaliyo wakuta, mathalani Azory Ngwanda, Kabendera na wenzake, Kama baadhi ya viongozi wa dini waliojipambanua kutetea haki za wanyonge mfano Askofu Mwamakula, Askofu Rwemwigizi, Askofu Bagonza na wenzake kugeuzwa wahanga wa maslahi ya haki kwa Taifa.

Hali hii ina limegua Taifa kwa kutamalaki kwa chuki isiyo na mfano. Hii ni dalili mbaya sana inayovunja mshikamano wa kitaifa kwa kuwa walio wengi wamepoteza matumaini dhidi ya wachache waliojitwalia haki kwa kila jambo lao.

Nivizuri sasa kujitazama wapi tumejikwaa Kama Taifa vinginevyo yote aliyo yafanya BABA WA TAIFA kujenga mshikamano wa kitaifa ni bure.

Kila mmoja atimize wajibu wake,upambe haufai kwa maslahi mapana ya nchi,vingenevyo tunakwenda kuangamia kwa kupoteza maarifa.

Watanzania sifa yao kuu ni upendo,lakini upendo umepotea si BAKWATA wala TEC na wengineo wanaweza kukemea yanayo endelea ndo maana miongoni mwao wasiopendezwa na hali hii wamesimama binafsi kusimamia majukumu mazito ya kichungaji kuiokoa jamii,poleni Sana na hongereni Sana Mungu anayatambua majukumu yetu katika kipindi hiki cha #ThE SHARPER THE TONGUE IS EASY TO CUT HIS OWN THROAT THROUGH ON IT.
 
Ni kweli maadili yameshuka wazi wazi.

Ndio maana hata Meko hujitokeza hadharani akitumia magari na nyenzo za umma kutoa kauli zinazoakisi mawazo yake ya ngono hadharani kweupe! "Wewe unataka upanuliwe wapi, nyuma ama kwa mbele??" Hii ni moja ya kauli zake jinsi asivyo jiheshimu.

Ananukuliwa mara kadhaa akiwasilisha mawazo yake ya ngono hadharani.

Kama watawala hawa waovu kutoka chama cha kijani wanaweza kujitokeza hadharani na kutoa kauli hata za kutishia kutoa uhai wa mtu kwanini tusiseme maadili yameshuka?
 
Walipokuwa wanafanyiwa ubaya wapinzani mlikuwa mnachekelea, sasa yamewarudi mnalalamika kuwa maadili yameshuka. Mngeanza kuwakemea vijana wa UVCCM waliokuwa wanakesha kuwatukana wapinzani mitandaoni na kuwatishia kuwaua wakiongozwa na kina musiba na kihongosi (ambaye mmemzawadia ukuu wa wilaya) haya yote yasingekuwepo.
 
Back
Top Bottom