N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Kuna jambo nimekuwa nikilitafakari siku hizi kuhusu namna taasisi za umma zinavyowasiliana na umma, hasa kupitia social media.
Kwa kweli naamini kuna haja kubwa kwa maafisa habari kubadilika na kuanza kuelewa vizuri hisia, tabia na matarajio ya audience wanayoihudumia.
Dunia imebadilika, social media imebadilika na hata namna watu wanavyopokea taarifa imebadilika, lakini bado sehemu kubwa ya institutional communication inaonekana kama imetoka kwenye zama za press release za miaka 15 iliyopita.
Mfano mzuri ambao nimeuona hivi karibuni ni NIDA.
Kuna ile post ya koti ambayo admin wa akaunti yao aliweka.
Kitu ambacho kwangu kilikuwa interesting siyo tu lile koti, bali namna post ile ilivyoweza kuifanya taasisi ionekane kuwa ina watu halisi nyuma ya account.
Ilikuwa tofauti na ile style tuliyoizoea ya “Mamlaka inapenda kuufahamisha umma kwamba...” kila siku.
Ghafla unaona watu wana-relate, wanacomment, wanacheka na wana-interact na taasisi.
Na baada ya hapo kitu kingine cha kuvutia kimeanza kuonekana. Unaona maafisa habari wengine nao wanaanza kuingia kwenye style kama hiyo.
Mmoja anaweka koti, mwingine anaingiza humour, mwingine anatumia lugha nyepesi zaidi.
Hapo ndipo ninaposema, siyo vibaya kuiga idea, lakini tusije tukawa tunaiga koti bila kuelewa kwa nini lile koti lilifanya kazi kwa NIDA. Ongezeni ubunifu!!!
Kitu cha msingi hapa siyo koti. Kitu cha msingi ni kwamba audience imebadilika.
Hiki kizazi hakikatai taarifa, lakini hakitaki tena taarifa zote ziletwe kwa lugha ngumu na delivery ya kiofisi.
Mambo ya Folio sijui Kumbukumbu Namba achaneni nayo au punguzeni kama kweli mnataka kuwafikia hawa kizazi cha sasa!!!
Wanataka information lakini pia wanataka connection. Wanataka taasisi izungumze nao, siyo kuwahutubia.
Mtu anaweza kutaka kujua kama NIDA yake imefika, lakini si lazima umwambie kwa paragraph tano zinazoanza na “Mamlaka inapenda kuufahamisha umma...” Unaweza kusema kwa lugha rahisi kabisa.
Hapo ndipo nadhani baadhi ya maafisa habari mnahitaji kubadilisha mindset.
Social media siyo website ya pili ya taasisi!!!
Si sehemu ya kupaste press release kila siku!!!
Social media inahitaji personality, creativity, relatability na zaidi ya yote inahitaji kumuelewa mtu aliye upande wa pili wa screen.
Na hii haimaanishi kwamba taasisi ziache kuwa professional au serious. Hapana.
Unaweza kuwa serious bila kuwa boring. Unaweza kuwa official bila kuwa robotic.
Unaweza kuwa na authority bila kuongea kama unasoma waraka mbele ya wananchi.
Tatizo letu mara nyingi ni kwamba tunafikiria “hard news” ndiyo lazima iwasilishwe kwa “hard language”.
Hapo ndipo tunapokosea. Hiki kizazi hakikatai hard news; kinataka hard information ipelekwe kwa soft communication.
NIDA kawafungua endelezeni sasa!
Usione post imepata likes nyingi halafu ukaiga tu format yake. Jiulize, imefanya kazi kwa sababu gani? Ni humour? Ni timing? Ni visual? Ni lugha? Ni curiosity? Ni kwamba imegusa experience ya watu? Ukielewa hiyo, utaweza kutengeneza content inayofanya kazi kwa taasisi yako bila kuwa copycat.
Kwa hiyo maafisa habari, tusikimbilie kuiga koti. 😄
Tuchukue lesson iliyopo nyuma ya koti.
People want to deal with people. Wanataka kuona upande wa kibinadamu wa taasisi.
Wanataka taarifa, lakini wanataka pia wajisikie kwamba taasisi inawaelewa.
Communication ya leo siyo tena “institution talks to people”. Ni “institution talks with people”.
Na kama bado tunaendelea kuwasiliana na Gen Z na millennials kwa lugha ileile tuliyokuwa tunatumia kwenye press release ya mwaka 2008, halafu tunashangaa kwa nini post ina views chache na engagement ndogo, basi tatizo huenda siyo audience.
Labda ni sisi hatujajifunza kuongea na audience yetu.
Koti la NIDA ni mfano mdogo tu, lakini lesson yake ni kubwa: badilisha delivery, usibadilishe professionalism; kuwa human, bila kupoteza credibility. Hapo ndipo PR na communication ya kizazi hiki ilipo.
Wakatabahu Wabaadu Fakir!!