KERO Maafisa na Askari wa Uhamiaji tunateseka kwa uhamisho bila malipo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Msemakweli11

New Member
Joined
Feb 20, 2026
Posts
1
Reaction score
2
Habari, naomba kuwasilisha kero inayotukabili sisi watumishi wa Idara ya Uhamiaji, tumekuwa tukihamishwa bila malipo hali iniyopelekea kuteseka kukamilisha uhamisho.

Tunatambua kuwa sisi ni kada ya Askari lakini haiondoi ukweli kuwa sisi ni binadamu, tuna familia zinatutegemea na ni haki yetu ya msingi kulipwa fedha za uhamisho kwa wakati.

Wengi tunadai fedha za uhamisho tangu 2023. Hali hii inachochea vitendo vya rushwa katika utendeji wa Idara.

Tunamuomba Mh Rais wetu-Dr. Samia Suluhu aliangalie suala hili kwani ni tatizo kubwa kwa sasa.
 
Ooho huku tena mboni hatuelewi hizo hela zenu za kuamishwa si wanakula wakubwa zenu mnawaogopa kuwachana za usoni waambie kabisa boss mimi hapa hujanipa changu ******** zako sihami na lolote hunifanyi. Nitoe changu kwangu ndio nihame bila hivyo ******** nabaki hapahapa ukitaka hama wewe ukazibe hio nafasi huko, mnashindwa nini kufanya hivyo unaogopa atakufukuza kazi na unamdai haki yako?
 
Maaskari gani? Sema Sisi mapolisi! Na nyie no watu?
 
Yaani hii nchi Kila sehemu ya kazi kuna malalamiko, rushwa na wizi haiwezi kuisha kabisa.
 
Mngemwandikia Rais barua ya kueleza malalamiko yenu!
Lakini ukiyaleta humu utakutana na majibu ya hasira ambayo watu wanayo kutokana na kilichotokea okt.29-31
 
Ooho huku tena mboni hatuelewi hizo hela zenu za kuamishwa si wanakula wakubwa zenu mnawaogopa kuwachana za usoni waambie kabisa boss mimi hapa hujanipa changu ******** zako sihami na lolote hunifanyi. Nitoe changu kwangu ndio nihame bila hivyo ******** nabaki hapahapa ukitaka hama wewe ukazibe hio nafasi huko, mnashindwa nini kufanya hivyo unaogopa atakufukuza kazi na unamdai haki yako?
Askari sio raia rafiki ,kuna lugha za kuongea sio hizi unazosema wewe .

Pasina kusahau amri uwa inatekelezwa kwanza na malalamiko yatafuata baada ya amri
 
Tukio la Oct29 limetuondelea huruma na faraja. Zamani uzi kama huu ungejaa replies za suluhisho na faraja, sasa imekuwa tofauti kabisa.
Mleta uzi usikimbie, vumilia na uwasome Watanganyika,wana maumivu makali kuliko uhamisho wako unao cheleweshewa malipo.
 
Habari, naomba kuwasilisha kero inayotukabili sisi watumishi wa Idara ya Uhamiaji, tumekuwa tukihamishwa bila malipo hali iniyopelekea kuteseka kukamilisha uhamisho.

Tunatambua kuwa sisi ni kada ya Askari lakini haiondoi ukweli kuwa sisi ni binadamu, tuna familia zinatutegemea na ni haki yetu ya msingi kulipwa fedha za uhamisho kwa wakati.

Wengi tunadai fedha za uhamisho tangu 2023. Hali hii inachochea vitendo vya rushwa katika utendeji wa Idara.

Tunamuomba Mh Rais wetu-Dr. Samia Suluhu aliangalie suala hili kwani ni tatizo kubwa kwa sasa.
Ok nimesoma na nina ndugu yangu mmoja ni boss mkubwa yupo uhamiaji nimeongea nae kwa simu na nimemwambia asome huu uzi na alifikishe kwa wakubwa zaidi,mimi hawezi kunijibu kwa kuwa maadilinyao ya kazi hayaruhusu lakini ndani ya wiki 2 utaona majibu,iwapo jambo hili ni kweli
 
Sasa huku kaja kuandika nini na anajua imetolewa amri?
Ukorudi hapo juu kuna mtu kamwambia kuwa angeendelea kulilia shida zake kwa kutumia neno watumishi wa idara ya uhamiaji walau ingeleta maana sababu wapo wasio askari ila alikosea aliposema sisi watumishi wa idara ya uhamiaji ambao ni askari ni hapo alikanyaga waya aise .

Vipi lakini swaumu inaenda kaka ?
 
Nje ya mada
Nyie rushwa ni jadi yenu msisingizie kucheleweshwa kwa fedha za uhamisho.
Mbona wale wengine ambao hawajahamishwa wembe ni uleule?
 
Back
Top Bottom